Maswali kwa rais Kikwete na yatokanayo

Maswali kwa rais Kikwete na yatokanayo

- Wakuu nasikia Muungwana leo amepiga bao la pele na maneno mengi yanayokubalika, kwa haya niliyopewa sasa hivi kuwa kayasema ninampa credit ila ninataka kuona anayaweka kwenye vitendo, maana the damage iliyofanyika sio ndogo inatia moyo ingawa ndio hivyo tumeonewa vya kutosha na kudanganywa vya kutosha, labda this time ana mean kweli.

Hongera Muungwana kwa hii hotuba, na sasa tunatayarisha majibu rasmi ya kumpongeza Rais, ili yatoke kesho kwenye media maana hii ya leo ni serious, ila tuone matendo.

Respect.

FMEs!
 
I think JK akiendelea hivi sio tu atajua nini watu wanatunza ndani ya roho zao, bali atajifunza kuongoza ni lazima uwe karibu na watu. Viongozi wengi wamekuwa waamrishaji tu kama watanzania wote ni watoto wa shule za chekechea. Na baadhi ya maswali yamekuwa mazuri na yametoa picha ya fikra za watu zikoje juu yake na usanii wa ufisadi

Sifikiri kama JK haelewi matatizo ya Tanzania, JK anaelewa matatizo pengine vizuri kuliko most people hapa, kwa sababu ana access na info.

Issue hana uwezo wala nia ya kutatua. Ndiyo maana unaona circuses kama hizi.Halafu utaanza kusikia watu wanamsifia eti kwa kuwa open.
 
- Ameulizwa kuhusu Kagoda na marafiki zake na amekubali kwamba ni kweli anao marafiki huko, lakini sheria itachukua mkondo wake yaani haya kweli yametoka kwa Muungwana?

- Eti ameulizwa kuhusu Sitta na kufukuzwa, akasema hafukuzwi mtu na kamati ni ya kupatanishana tu na sio kufukuzana, eti wakuu mliomsikia live ni kweli au fix hizi?

Respect.

Field Masrhall Es!
 
- Wakuu nasikia Muungwana leo amepiga bao la pele na maneno mengi yanayokubalika, kwa haya niliyopewa sasa hivi kuwa kayasema ninampa credit ila ninataka kuona anayaweka kwenye vitendo, maana the damage iliyofanyika sio ndogo inatia moyo ingawa ndio hivyo tumeonewa vya kutosha na kudanganywa vya kutosha, labda this time ana mean kweli.

Hongera Muungwana kwa hii hotuba, na sasa tunatayarisha majibu rasmi ya kumpongeza Rais, ili yatoke kesho kwenye media maana hii ya leo ni serious, ila tuone matendo.

Respect.

FMEs!

Sasa wee mzee wa ze dataz, mbona mimi sijasikiliza hiyo spichi na ninaelewa vingine. Wewe hayo umeyasikia wapi? Mbona yanatofauti na michango hii hapa juu?
Are you swaumuringi?
 
RAIS Jakaya Kikwete, amesema kuwa hajawafunga midomo wabunge na badala yake amewataka waendelee kuikosoa serikali kwa misingi iliyo sahihi.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wananchi kwa staili yake mpya ya kujibu maswali ya papo kwa papo kwa kutumia simu, ujumbe mfupi wa simu (sms) na barua pepe kupitia televisheni na redio.

Akijibu swali lililoulizwa kwa njia ya barua pepe kwamba kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kililenga kuwaziba midomo wabunge pamoja na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, Rais Kikwete alisema kilichotokea mjini Dodoma ni mazingira ambayo yameonekana kama vile ni uhusiano usioridhisha kati ya wabunge wa CCM na serikali yao.

Alisisitiza kuwa kamwe serikali yake haina nia na haiwezi kuwaziba midomo wabunge wake.

“Kweli tulikuwa na mjadala mkali sana, wengine wakatajana majina, lakini kilichoonekana ni mazingira ambayo yameonekana kama vile ni uhusiano usioridhisha kati ya wabunge wa CCM na serikali yao. Lingine ni mazingira ya kuchukiana sana kati ya wabunge wa CCM, wanachukiana kiasi kwamba wanashindwa hata kuachiana glasi za maji.

“Lakini pia NEC iliona kwamba kwenye kamati ya chama ya Bunge, ilitokea hisia kwamba haifanyi kazi ipasavyo, hivyo tukasema tutafanyaje kuondoa hali hii ya kuchukiana sana, na tufanye kamati yetu ya chama ifanye vizuri.

“Basi hatimaye tukakubaliana kwamba lazima mambo hayo tuyashughulikie, tukamwomba Msekwa, Mwinyi na Kinana, tukasema basi waangalie hali hii ili kuondoa tofauti hizo. Hicho kwa kweli ndicho kilichotokea Dodoma. Mimi naamini baada ya wazee wetu hawa tutafika pazuri, nataka wabunge wetu waikosoe serikali ili kukijenga chama na serikali na hakukuwa na juhudi za kuziba watu midomo,” alisema.

Akijibu swali la Solomoni Natal wa mjini Arusha kuhusu kuwapo makundi ndani ya CCM, Rais Kikwete alisema hakuna makundi bali kilichopo ni kwamba kuna uwazi zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

Kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki na ule wa Waislamu uliotolewa na Shura ya Maimamu, Rais Kikwete alisema kuwa umeitisha serikali yake, na sasa viongozi wakuu wa taifa wanafanya utaratibu wa kukutana na viongozi wa dini.

Alisema hayo akijibu swali aliloulizwa kwa njia ya simu na Zombo Kamkala wa jijini Dar es Salaam.

Katika swali lake la msingi, Zombo alihoji sababu za rais kuwa kimya baada ya Kanisa Katoliki na Waislamu kuzindua nyaraka zao zinazoelekeza waumini wao jinsi ya kuchagua viongozi wakati wa uchaguzi mkuu mwakani.

“Mheshimiwa Rais, hawa jamaa mbona wanatupeleka mahala pabaya na nyaraka zao, na mbona serikali imekaa kimya?” alihoji Zombo.

Akijibu swali hilo kwa hisia, Rais Kikwete alisema kuwa waraka wa Katoliki na baadaye mwongozo wa Waislamu, umeishitua sana serikali yake kiasi cha kuleta hofu, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

“Hili jambo ni kweli limetushtua sana na kuleta hofu kubwa, hasa kule tunakoelekea kwenye uchaguzi, kwani kuna hatari ya Watanzania kupiga kura kwa maelekezo ya dini zao, Wakristo na Waislamu.

“Hii inatia hofu sana na hata kwenye kikao cha NEC mjini Dodoma, tumezungumza na kwa pamoja tumeiona hofu hiyo, kwani kama tukiendelea hivi, hatutakuwa na taifa, badala yake kutakuwa na ushindani wa kidini.

“Si mwelekeo mzuri sana, Mwalimu amelijenga taifa hili bila ubaguzi, tutazamane kwa Utanzania wetu na si kwa dini zetu,” alisema.

Rais Kikwete ambaye ni mara yake ya kwanza kuzungumzia suala la waraka wa Wakatoliki na Waislamu hadharani, alisema kuwa NEC, imeagiza viongozi wakuu wa taifa, akiwamo yeye mwenyewe, makamu wake na Waziri Mkuu, kukaa meza moja na viongozi wa dini ili kujadili hatma ya taifa hili kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwakani.

Mbali ya kuagiza kukutana na viongozi hao wa dini, Rais Kikwete alisema NEC pia imeagiza viongozi wa siasa kuacha kulumbana hadharani juu ya nyaraka hizo na kuwataka waumini wa dini zingine kutofanya hivyo kwa sasa.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, tayari serikali imeshaanza mawasiliano na viongozi na kusisitiza kuwa katika kipindi hiki, viongozi wengine wa madhehebu mengine ya dini, wasitoe nyaraka zaidi.

Rais Kikwete katika mazungumzo hayo, pia alizungumzia suala la ufisadi na kutamba kuwa katika dunia, Tanzania inaweza kuingia kwenye rekodi ya kuthubutu kwa kuweza kuwafikisha mahakamani zaidi ya vigogo 27 wa serikali.

Akijibu swali la Jacob Mkama wa Ukerewe, kwamba serikali haijafanya juhudi katika kukabiliana na mafisadi, Rais Kikwete alisema madai hayo si sahihi, kwani juhudi ambazo serikali yake imefanya katika kukabiliana na rushwa na ufisadi, zinaonekana.

“Ningeshangaa sana kama nisingeweza kuulizwa swali hili. Mimi natazama suala hili katika hatua mbili, kwanza kujenga chombo cha kuongoza mapambano, yaani TAKUKURU. Usipokijenga, hatutafika mbali. Kwanza tukaanza na sheria, tuliyokuwa nayo ni ya mwaka 71, sasa tuna sheria mpya,” alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alitamba kuwa hivi sasa serikali yake imeimarisha utendaji kazi wa TAKUKURU kwa kuajiri watumishi zaidi na kuwapa mafunzo pamoja na vifaa vya kufanyia kazi.

“Tumejenga mazingira ya kuwataja walarushwa, hivi sasa kuna kesi 578 toka kesi 50 zilizokuwepo mwaka 2005, taarifa nyingi zaidi zinapatikana. Wengine wanasema tunashughulika na dagaa tu, mbona papa hakuna? Tumefanya kesi za EPA, BoT, watendaji wakuu wa serikali 27 wako mahakamani na naweza kusema Tanzania tunaweza kuingia kwenye rekodi duniani ya kuthubutu,” alisema Rais Kikwete.

Alitoboa siri kuwa hivi sasa kuna kesi kubwa tatu ambazo zimekamilika na wakati wowote TAKUKURU itawafikisha wahusika mahakamani.

Alitamba kuwa hakuna rafiki katika vita dhidi ya ufisadi, na kwamba hana ndugu wala rafiki, kwani tayari baadhi ya rafiki zake wa karibu, hivi sasa wako matatani.

Akizungumzia suala la ujenzi wa shule na matatizo ya walimu, Rais Kikwete alisema serikali yake imejenga shule nyingi katika kipindi kifupi, hivyo kusababisha uhaba wa walimu pamoja na vifaa.

Hata hivyo, alielezea mikakati ya kukabiliana na kasoro hizo ili kutoa fursa zaidi kwa wananchi kupata elimu.

Kuhusu matatizo ya madai ya walimu na mradi wa ujenzi wa nyumba zao kama alivyoulizwa na Pascal Justine, Rais Kikwete alisema baada ya muda mfupi matatizo hayo yatakuwa historia.

Alisema atajibu maswali yote aliyoandikiwa kwa ujumbe mfupi, barua pepe na kwamba atatafuta muda mwingine wa kuzungumza na wananchi kwa staili hiyo.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hili kwa kiongozi wa nchi kuzungumza na wananchi wake kwa staili ya kuulizwa maswali.

Hata hivyo, rais alijibu maswali yasiyozidi 15 kutokana na urefu wa majibu kwani alitumia karibu saa mbili kujibu maswali hayo.


Kwa Hisani ya:Tanzania Daima.
 
Sasa wee mzee wa ze dataz, mbona mimi sijasikiliza hiyo spichi na ninaelewa vingine. Wewe hayo umeyasikia wapi? Mbona yanatofauti na michango hii hapa juu?
Are you swaumuringi?

- Mkuu Nzoka vipi mkuu kweli unadhani ninaweza kuwa na habari za uongo mkuu au hukusikiliza hiyo kitu, ndio kwanza hapa nimemaliza kumsaidia kiongozi mmoja hapa kujibu hotuba hiyo kwenye media kwa hiyo cheki tena mkuu na usikie kilichosemwa.

- Huwa sio tabia yangu kuleta uongo JF nimeongea na mwandishi maarufu amenisomea hotuba yote na maswali na majibu na soon nitakuwa na script nzima na tutaichambua hapa kama kawa.

Respect.

FMEs!
 
Lol. Sawa mkuu wa majeshi, ila mimi nilishakwambia wewe na JK hamtofautiani hehee. Its a compliment.
Gudnite. Ngoja niwahi kulala maboksi yananisubiri. Nachangisha nirudi jimboni maana naona hawa wabunge story mingi.
 
Lol. Sawa mkuu wa majeshi, ila mimi nilishakwambia wewe na JK hamtofautiani hehee. Its a compliment.
Gudnite. Ngoja niwahi kulala maboksi yananisubiri. Nachangisha nirudi jimboni maana naona hawa wabunge story mingi.

- Haya mkuu wangu, kesho Mama Maria Nyerere yupo UN ndugu yangu, saafi sana Mwalimu bado anatukuzwa internationally, heshima kubwa sana kwetu wananchi wa Tanzania.

Respect.

FMEs!
 
Akijibu swali la Jacob Mkama wa Ukerewe, kwamba serikali haijafanya juhudi katika kukabiliana na mafisadi, Rais Kikwete alisema madai hayo si sahihi, kwani juhudi ambazo serikali yake imefanya katika kukabiliana na rushwa na ufisadi, zinaonekana.

"Ningeshangaa sana kama nisingeweza kuulizwa swali hili. Mimi natazama suala hili katika hatua mbili, kwanza kujenga chombo cha kuongoza mapambano, yaani TAKUKURU. Usipokijenga, hatutafika mbali. Kwanza tukaanza na sheria, tuliyokuwa nayo ni ya mwaka 71, sasa tuna sheria mpya," alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alitamba kuwa hivi sasa serikali yake imeimarisha utendaji kazi wa TAKUKURU kwa kuajiri watumishi zaidi na kuwapa mafunzo pamoja na vifaa vya kufanyia kazi.

"Tumejenga mazingira ya kuwataja walarushwa, hivi sasa kuna kesi 578 toka kesi 50 zilizokuwepo mwaka 2005, taarifa nyingi zaidi zinapatikana. Wengine wanasema tunashughulika na dagaa tu, mbona papa hakuna? Tumefanya kesi za EPA, BoT, watendaji wakuu wa serikali 27 wako mahakamani na naweza kusema Tanzania tunaweza kuingia kwenye rekodi duniani ya kuthubutu," alisema Rais Kikwete.

Alitoboa siri kuwa hivi sasa kuna kesi kubwa tatu ambazo zimekamilika na wakati wowote TAKUKURU itawafikisha wahusika mahakamani.

Alitamba kuwa hakuna rafiki katika vita dhidi ya ufisadi, na kwamba hana ndugu wala rafiki, kwani tayari baadhi ya rafiki zake wa karibu, hivi sasa wako matatani.
Well, hii itabakia kuwa nakala yangu kichwani... nasubiri huo muda anaotaka JK kutumwagia manyanga!.. heee heee! isije kuwa kabla ya Uchaguzi!
 
Kuna member mmoja alishasema zamani "AKICHEKA, MMEKWISHA".

Sasa inabidi muanze kuamini sahihi yangu na mrudie tena na tena. Yes, Dr. Slaa for President 2010.

Maisha bora kwa Watanzania, sisi Sikonge twaishi hivi:

n1157134975_30483332_3702001.jpg
 
Waungwana, hii njemba imeshakaa madarakani miaka minne sasa na hadi hii leo hajaweza kutimiza hata moja ya ahadi zake alizotuahidi Watanzania katika kampeni ya 2005. Hana jipya huyu kwa maoni yangu.

Ahadi hizo za maisha bora kwa kila Mtanzania, tunaona zimekuwa ni za maisha bora kwa kila fisadi na Watanzania maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha. Ahadi za kuipitia tena mikataba ya kifisadi kuchimba madini yetu mbali mbali ambayo tumeipigia kelele kwamba haina maslahi kwa Watanzania na Tanzania hadi hii leo hakifanywa chochote kile cha maana. wachukuaji bado wanachukua 97% ya mapato yanayotokana na madini yetu na kutuachia sisi 3% huwezi kupata mikataba kamaa ya wizi nchi yoyote duniani bali kichwa cha mwendawazimu Tanzania

Anasema mafisadi wamejificha hivyo inakuwa vigumu kuwashughulikia! Hawa akina Rostam Aziz, Chenge, Manji, Subhash, Lowassa, Karamagi, Mkapa, Jeetu, Makamba na wengineo mbona bado tunawaona wanapeta mitaani na mapesa yao ya kifisadi!? Au njemba itanaka kutufanya Watanzania ni wapumbavu kiasi hicho!

Kwa mara nyingine tena kathibitisha kwamba hastahili kugombea 2010. Uongozi wa nchi umemshinda na ni ufisadi wa hali ya juu kung'ang'ania kuendelea kubaki madarakani hata kama kuna ushahidi wa kutosha unaonyesha kwamba Uongozi umemshinda.

Kuna haja ya kurudia tena huu usanii wa leo lakini safari hii kwa masaa 6 toka saa saba mchana mpaka saa moja usiku hakuna matangazo ya biashara bali tumuweke kiti moto ajibu maswali mbali mbali ya Watanzania ndani na nje ya nchi na hii tabia yake ya kutupigia hadithi aachane nayo, jibu swali kama huna jibu sema sina jibu siyo kuanza blah blah bla zisizo na kichwa wala miguu.

Na huku kucheka cheka wakati unajibu maswali yenye kero kubwa kwa Watanzania kunaudhi sana. Mwalimu Nyerere alikua hakenui kenui ovyo ovyo wakati anazungumzia jambo lenye uzito mkubwa kwa Watanzania. Onyesha uzito wa jambo unapoongea angalau kwa masaa hayo mawili. Si ajabu ndio maana uliingia mitini kwenye debate 2005 maana ulijua umejaa pumba tupu na Lipumba angekuaibisha.

Tunataka Kiongozi mpya wa nchi 2010. Kikwete uongozi wa nchi umemshinda na upo ushahidi wa kutosha kuthibitisha hili.
 
Last edited:
As always, once again ladies and gentlemen.

Bread and circuses, what am I talking about, no bread, and plenty circuses, bad circuses at that.
 
...Kuna mtu kamuuliza hili swali – 'mh. Rais ulituahidi maisha bora kwa kila mtanzania, mbona hatuoni?" –

Jibu: Ni kweli niliahidi na ndiyo ilani ya chama changu. Kwetu sisi maisha bora yana sura mbili, kwanza kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana, kama vile barabara, maji, afya, elimu- wananchi wakipata vitu hivyo maisha yao yatakuwa bora, naiyo maana tumeongeza ujenzi wa barabara, wanafunzi wanaofaulu kwenda sekondari, mishahara ya wafanyakazi imeongezeka.

Hivyo vitu vitapatikana lini? 2010 au ndio njia anayotaka kupewa tena urais hapo mwakani.
 
JK anasema mapapa wa ufisadi kuwapata ni ngumu kwasababu wana maarifa makubwa ya kujificha.

Kiwete hawezi kufanya lolote jamani, yupo busy saloon na hana capacity. Tulifanya kosa hatuna jinsi zaidi ya kufanya mabadiliko 2010. Ukimuona facebook yupo anachat tu na network yake ni kina Wema Sepetu na warembo wenzake
 
Hivi, kwa nini mh. Rais aliamua jana tarehe 09/09/09 ndio iwe siku ya kufanya hicho alichofanywa.... au ndio yale yale?
 
- Ameulizwa kuhusu Kagoda na marafiki zake na amekubali kwamba ni kweli anao marafiki huko, lakini sheria itachukua mkondo wake yaani haya kweli yametoka kwa Muungwana?

- Eti ameulizwa kuhusu Sitta na kufukuzwa, akasema hafukuzwi mtu na kamati ni ya kupatanishana tu na sio kufukuzana, eti wakuu mliomsikia live ni kweli au fix hizi?

Respect.

Field Masrhall Es!

Suala la ufisadi bado linampa kigugumizi. Anatafuta na kutafuna maneno, anazungumza sera zaidi badala ya kujibu swali. Aliulizwa kuhusu Kagoda na Richmond, na kwamba anashindwa kuwashughulikia wahusika kwa sababu ni rafiki zake. Alijibu kuhusu Richmond, akimtetea kiaina Lowassa, huku akisema hakukuwa na ushahidi wa wazi kuhusu rushwa, na kwamba, ikihitajika, basi tushirikishe hata watu wa nje kupata ukweli.

Hakusema neno kuhusu Kagoda. Aliishia kusema kwamba hakuna urafiki kwenye masuala ya kushughulikia rushwa, akitoa mifano ya kesi zinazoendela, na kwamba kuna kesi kama mbili tatu hivi karibia zitatinga mahakamani.

Tido Mhando alimuuliza kuhusu Sitta. Akarejea maelezo yake kuhusu kilichotokea kwenye hiyo NEC yao. Kwamba mjadala ulikuwa wa wazi na mkali. Watu walitajana na walitupiana maneno makali. Kuna mama kutoka Singida alimuuliza swali kwa nafasi yake kama mwenyekiti wa CCM, kwamba kulikoni, chama kina makundi, na kwa nini wabunge wanazibwa mdomo. Akasema NEC haiwafungi mdomo wabunge, ila wana wajibu kwa serikali yao ya CCM.

Kwa ufupi, majibu yake yanathibitisha tulichokisikia kuhusu yaliyotokea NEC. Kuna wakati alionekana kusema wale waliotoa taarifa za hicho kikao hawakuleta picha sahihi ya kilichotokea. Kinachonishangaza kwa nini walikaa kimya bila kurekebisha kumbukumbu kuhusu upotoshaji? Inaonekana wanajaribu kusafisha hali ya hewa baada ya kuanikwa yaliyojiri na jinsi JK alivyochekelea Sitta kusulubishwa.
 
Aliniacha hoi alipojibu suala la madai ya walimu.

Anashangaa kila baada ya miezi mitatu yanaibuka madai mapya!!! Anadai wameweka mkakati wa kupita kila shule timu ya wataalamu wakiwemo wahasibu na watawala na kumuuliza "mwl Tido na wakilridhika wanamlipa", "mwl Kikwete na wakilridhika wanamlipa", "mwl Mariamu na wakilridhika wanamlipa".

Mungu wangu!!! una walimu wangapi nchi nzima hata ushangae kuja madai mapya kila baada ya miezi mitatu? Na hiyo gharama ya jopo la wataalamu kumpitia kila mwl si kubwa kuliko hizo nauli za likizo wanazodai walimu? Kwa kweli hatuna kitu hapa
 
JK alinishangaza wakati anajibu swali aliloulizwa kwa nini safari za nje ni nyingi? Alijibu kuwa huwa anaenda kutafuta msaada (Kuomba omba) na ni lazima aende yeye mwenyewe physically ili aweze kupewa hiyo misaada.

Hivi kwa kweli rais kama anamtazamo wa kuomba omba na ndio kiongozi wa juu kabisa wa nchi sasa anategemea nini kwa wananchi wake. Ndio maana kila siku atasikia kuna njaa vijijini kwa sababu watu hawataki kujishughulisha.

Rais JK anapaswa aache kabisa hiyo dhana ya kuomba omba na akae na wataalamu wa fedha na uchumi ili waweze kumpa strategic plan ambazo zinaweza kuliokoa taifa letu kwenye ili janga la kutegemea misaada kutoka nje. Nchi hii ina Resources nyingi sana na haipaswi kuwa omba omba.
 
Tido anatuchezea, haya ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma. Ni maswali yale tu yaliyoandaliwa majibu ndiyo yaliyokuwa yanajibiwa, hata yaliyoulizwa toka Sengerema, Mwanza, Arusha yanaashiria waulizaji walipangwa. Mtanzania karne hii anaona kupelekewa umeme Sengerema ni zawadi na si jukumu la serikali!!! UPUPU MTUPU
 
Back
Top Bottom