Maswali magumu: Utetezi wa Jakaya Kikwete dhidi ya tuhuma za chuki binafsi dhidi ya Hayati Magufuli msibani

Maswali magumu: Utetezi wa Jakaya Kikwete dhidi ya tuhuma za chuki binafsi dhidi ya Hayati Magufuli msibani

Mi sioni sababu ya kuhoji aliyoyaeleza JK, yeye ndiyo kasema JPM alikuwa jembe na rafiki yake hadi akatafutiwa kiwanja Chato,sasa unapopinga na kuhoji unamaanisha nini? Yaani unabishana na mtu anaekuelezea yake ya moyoni mwake!Hii nayo ni habari nyingine sasa mkuu.
Hahahaha
Watu Wana ukweli wanaotaka kuusikia... Acha wapeane huo... Wacheze ngoma za adui 😀
 
JK ni Mswahili kama Waswahili wengine tu wa Pwani. Kuna sehemu alisema JPM alikuwa akimshtaki kwa kaka yake (JK) mara zote alipo mkwaza!! Mara alimpenda sana!! 😇
JK mtamchukia na kumtukana kwa kila namna lakini ukweli utabaki kuwa kwa ujanja tu jamaa yuko mbali sana....bila kupenda mtaendelea kulitaja jina lake mpaka siku anaingia kaburini.

kwani kukwazana ndo uhasama?!!!! wanakwazana wanandoa ndani itakuwa wanasiasa waliojuana siasani!!! uzuri mmoja jamaa akishasema anatulia tuliii anajilia zake mananasi msoga huko hana hata muda wa kushughulika nanyi hadi siku anayoamua. na akiamua kujibu siku hiyo (kama alivyofanya leo) anakuacheni na kazi tena ya kujadili kama hivi........mumwache tu hamumuwezi, kuna kitu amepewa lazima tukubali tu!
 
Mkuu kwani si tulitangaziwa kuwa rais alikufa tarehe 17 kama sikosei
Kabla hata ya hiyo tarehe 17, Kigogo alisema ameziona zile Gari za wazi za Ikulu zimetolewa kusambazwa, sasa labda zilienda tu sevice ya kawaida ndio coincidence yakatokea ya kutokea
 
JK mtamchukia na kumtukana kwa kila namna, lkn ukweli utabaki kuwa kwa ujanja tu jamaa yuko mbali sana....bila kupenda mtaendelea kulitaja jina lake mpaka siku anaingia kaburini.

kwani kukwazana ndo uhasama?!!!! wanakwazana wanandoa ndani itakuwa wanasiasa waliojuana siasani!!! uzuri mmoja jamaa akishasema anatulia tuliii anajilia zake mananasi msoga huko hana hata muda wa kushughulika nanyi hadi siku anayoamua. na akiamua kujibu siku hiyo (kama alivyofanya leo) anakuacheni na kazi tena ya kujadili kama hivi........mumwache tu hamumuwezi, kuna kitu amepewa lazima tukubali tu!
Mimi sijawahi kumchukia JK! Maana katika miaka yake ya Urais, alitupatia stahiki zetu zote mihimu kama watumishi wa umma! Nilicho maanisha hapo ni kwamba, mzee ni mswahili na ana maneno na vijembe vingi.

Ni kawaida sana kwake kumpiga mtu kijembe kwa maneno na misemo tofauti, huku anacheka!
 
JK leo tumekusikia ukijitetea kuwa watu wameanza kuzusha mitandaoni eti wewe ulikuwa unamchukia JPM na pengine ukawa mmoja wa maadui zake wakati wa utawala wake. Majibu yako yalikuwa mepesi saana kama kawaida yako "Mswahili" nanukuu "eti kama kweli ningekuwa namchukia JPM nisingeweza kupitisha jina lake katika mchakato wa kuwania Urais 2015 kwani mimi (kama Rais na Mwenyekiti wa chama) ndiye niliyepeleka majina matano (5) Halmashauri" na ukaenda mbele zaidi ukasema katika kuchagua majina matano jina la kwanza lilikuwa la JPM arafu yakafuatia mengine manne. Umeenda mbele zaidi na kusema kuwa alikuwa jembe lako katika baraza lako la mawaziri huku ukajikanganya zaidi na kusema mlipokuwa mnatifuanaJPM alikimbilia kupeleka mashtaka kwa kaka yako mkubwa ambaye ni marehemu sasa

Maswali magumu:

(i) Je, kwani wewe ndiye uliyependekeza hayo majina matano au ni CC ya chama chako ndiyo iliketi na kukuletea wewe kwa ajili ya kuyawakilisha Halmashauri? labda tusaidie kwani hayo majina ulitoka nayo nyumbani kwako kwa kushauriana na familia yako?

(ii) Je, si kweli JPM aliingizwa katika tano bora baada ya kuona mamvi hawezi kuaminika katika chama na wananchi wanataka mchapakazi asiye kuwa na doa ili kukikomboa chama kilichokuwa kinaelekea kuanguka na sio kwa mapenzi yako binafsi?

(iii) Hivi mashtaka aliyokuwa anapelekea JPM kwa kaka yako mara kwa mara yalihusu nini kama kweli alikuwa jembe lako katika baraza lako?
Kuwa na adabu, unamdharau MTU kisa si baba yako kwa kumuita mamvi! Hauna adabu.
 
JK ni Mswahili kama Waswahili wengine tu wa Pwani. Kuna sehemu alisema JPM alikuwa akimshtaki kwa kaka yake (JK) mara zote alipo mkwaza!! Mara alimpenda sana!! [emoji56]
Mme na mke,mtu na ndugu yake wanapendana sana hata hivyo kuna wakati wanatifuana hadi kwa wasimamizi/mashahidi wa ndoa au kea wazazi !! Sembuse JK na JPM!!!
 
Ukiingia kwenye siasa maisha yako yanahesabika,kifo kipo nje nje hauwezi kuwafurahisha wote,hata Kama ni walinzi wako hawezi kukupenda wote wapo watakao tii sheria kwa ajili ya pesa tu lakini mioyoni mwao wapo mbali sana nawewe.usimkabizi mtu uhai wako akushikilie maana siku yoyote anaweza kukugeuka papohapo kwa tamaa ya pesa
 
...." siasa haina adui wa kudumu"....nani alijua kuwa kuna siku watu kama akina Dr. Slaa, Halima Mdee n.k ....wataacha kupinga kila kitu?..
" it is always possible"..
 
Magufuli alikuwa mtu mtata na amefariki na kuacha utata. Hata siku aliyokufa exactly haijulikani. Watu watata hata wakifa mambo yao hayaishi ghafla kwa hiyo wacha watu wajadili kwa uwazi.

Itachukua muda legacy ya ukweli ya huyu kipenzi cha watu fulani fulani kutulia
Magu alikuwa mtata sana, kwa utata wake nahisi ni yeye mwenyewe alikataza viongozi wengine kusema kwamba anaumwa.
 
Kishazikwa na yake yote, conspiracy theories, hazikosekani. Nyingi unaona ni akili za MusibaKiGwajiBashi...
Na hiyo ni katika kugombea madaraka, wameambiwa hawana mvuto kwenye chama chao huko.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom