Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

Hunijui lkn unaongea vitu vya ajabu kabisa kama vile low esteem!
Wewe ndiyo mwenye inferior complex kwa kuunga mkono issue yyt ile inayohusu mtu anayetoka ukanda wa kwenu na unajulikana kwa hilo!Mm sina la kuogopa na kama madudu haya ya bosi wako ataendelea kuyafanya nitazidi kuyasema tu!

1.Kumpa team kocha weeks 2 kabla ya mashindano makubwa kachemsha
2.Kupeleka team Tukuyu kwenye baridi kali wakati mechi itachezwa kwenye joto huyu bosi wako kachemsha
3.Priority yake sasa kubadili jina la Taifa Stars kama halina maana yyt lkn asianze kufanya hivyo kwa chama anachokiongoza Kagera na timu yenu Lweru Eagles kachemsha
4.Kuokota vijana mitaani eti ndiyo maboresho kachemsha
5.Kuingilia masuala ya usajili wa Domayo wakati hamna team yyt kati ya hizo 2 zimepeleka issue hii TFF kachemsha!

Tukimsema bosi wenu ajirekebishe mnakuwa wakali kweli kweli na kukimbilia kuwa sina ideas yyt ya soka!
unafahamu zao la idea ya kutafuta hivo vipaji lilitoka wapi? unafahamu kuwa jopo la makocha, wadau na wataalamu wa soka nchini, waliweka kambi zanzibar, walijifungia takribani wiki nzima kuja na mikakati mbalimbali ya kuinua soka huo wa kusaka vipaji vipya kupitia timu za mkoa ulikuwa mmoja wa mikakati iliyozaliwa na hao wataalamu?? wewe unakuja na kumblame tuu Malinzi? ndo mana nikakwambia huna idea ya soka na hujui maamuzi ya TFF yapoje,
 
Malafyale yupo sa hii kuna mambo jaman pale tff yanaenda hovyo sana tena sanaaa mpaka inakera,
I)kuhama toka pale karume kwenda kupanga katikati ya jiji hili nalo linahitaji degree kufikiri??
II)Kumfukuza kocha kim bila sababu ya msingi na pesa za kukatisha mkataba zimetoka mifukoni kwa wachache hii kweli ndio inavyopaswa wadau,embu tuelezane ukweli c kulalamika mh rais hapa unahitaji kulisemea ili wadau tukuelewe unatakiwa utambue tff c yako n ya wadau na wapenzi wa mpira ipo siku wadau watagoma kuingia uwanjani hapo utasemaje.
III) Taifa stars yako haina mvuto mechi mbili angalia mwenyewe watazamaji wamepunguza mwamko kulingana na mipango yako isiyo tekelezeka mh rais.
IV)mpaka sasa mechi na zimbabwe haijulikani itachezwa wapi ili wapenzi wa mikoani tujipange kama n mbeya wekeni wazi wakubwa wa tff
 
Revocatus kaka naona unatetea ukanda sasa ukweli malinzi hana jipya na sitashangaa tbl mkataba utakapoisha wasiongeze tena,sema lile ambalo hata leo tangu malinzi aingie madarakani analo jipi la kujivunia hakuna zaidi ya porojo tupi.

Kubadilia jina??kuleta kocha mpya mda mfp kabla ya mechi kubwa na zimbabwe??mbaya zaidi kocha mpya hakuchagua wachezaji amekuta tayari ameshateuliwa wachezaje huoni na majanga kaka.

Mjulisheni malinzi kwa mfumo wake soka litapotea na kufa kabisaa.
 
Makocha hao unaosema walijifungia Zanzibar ndiyo hawa incompetent akina Mayanga na akina Pondamali?
Ndiyo wakaja na idea ya kuingia mtaani na kutafuta hao mnaowaita maboreshe na ndiyo hawa madudu matupu tulio waona mechi na Burundi?
Ndiyo hawa akina Mayanga wakaja na idea Taifa Stars ikae Tukuyu kwenye baridi kali ili hali mechi inachezwa kwenye joto?
Kama tunaacha kutumia wataalam waliosoma vyema soka la kisasa tukiwategemea akina Madadi wenye elimu za kale za soka basi soka lenu litabaki linadorora kila siku!

Nimemaliza sichangii tena uzi huu maana unaleta tu hasira!Zimbabwe anatuchapa Dar na kwao ingawaje nitaenda Harare just kutembea tu!
 
Revocatus kaka naona unatetea ukanda sasa ukweli malinzi hana jipya na sitashangaa tbl mkataba utakapoisha wasiongeze tena,sema lile ambalo hata leo tangu malinzi aingie madarakani analo jipi la kujivunia hakuna zaidi ya porojo tupi.

Kubadilia jina??kuleta kocha mpya mda mfp kabla ya mechi kubwa na zimbabwe??mbaya zaidi kocha mpya hakuchagua wachezaji amekuta tayari ameshateuliwa wachezaje huoni na majanga kaka.

Mjulisheni malinzi kwa mfumo wake soka litapotea na kufa kabisaa.

Mkuu mshazari ukisema hivyo hapa unaonekana HAUNA adabu,una wivu,na hujui lolote kuhusu soka!

Ukweli ni kuwa miezi 7 sasa ya uongozi wa Malinzi hamna lolote la maana zaidi ya porojo tu!Team yetu haina maandalizi,Sera zake za soka la vijana kuwaleta kuchezea Taifa Stars hazipo popote duniani na priority ya sasa ya Taifa Stars na watz kwa ujumla sio kubadili jina la Taifa Stars!

Kibaya zaidi juzi katuambia wazi kuwa yy na wenzake wanatoa pesa zao mfukoni kumlipa kocha wa zamani Kim,kwa sisi tunao fanya kazi za utawala,suala la kulipa pesa zenu kwenye kazi za kitaasisi ni kielelezo kuwa TFF haipo organized!
 
Last edited by a moderator:
Kamati ya utendaji ya TFF imemaliza kikao chake,kuanzia msimu wa 2015/16 ligi kuu itakuwa na timu 16.

Vp kuhusu timu zinazomilikiwa na Majeshi?? Je mliweka utaratibu wowote kuzihusu??
Manake isifike kipindi Kwenye timu 16 kwenye Ligi za JKT,JW,MAGEREZA,POLISI ni 10..Hapo patakuwa na tatizo kwenye soka letu la Tz...
PILI Ndugu Malinzi hili suala la Ligi yetu kusimama kwa kipindi kirefu katikati ya msimu kana kwamba tunapisha Msimu wa Baridi mnalichukuliaje??
 
Mkuu mshazari ukisema hivyo hapa unaonekana HAUNA adabu,una wivu,na hujui lolote kuhusu soka!

Ukweli ni kuwa miezi 7 sasa ya uongozi wa Malinzi hamna lolote la maana zaidi ya porojo tu!Team yetu haina maandalizi,Sera zake za soka la vijana kuwaleta kuchezea Taifa Stars hazipo popote duniani na priority ya sasa ya Taifa Stars na watz kwa ujumla sio kubadili jina la Taifa Stars!

Kibaya zaidi juzi katuambia wazi kuwa yy na wenzake wanatoa pesa zao mfukoni kumlipa kocha wa zamani Kim,kwa sisi tunao fanya kazi za utawala,suala la kulipa pesa zenu kwenye kazi za kitaasisi ni kielelezo kuwa TFF haipo organized!

Mkuu malafyale naanza kuamini zile sarakasi za malinzi kukimbilia mahakamani kutaka kuzuia uchaguzi haya ndio matunda yake,kuna mambo yanatia kichefuchefu suala la kuhama ofc ya karume kuwa wanapisha ujenzi??mm watu wa kagera nawatambua sana hapo aliona ofc haiendani na hadhi yake hakuna ka ujenzi nipo na tutakuja kuelezana humu.
A)kutubadilidhia jezi ya timu ya taifa kienyeji na blaa blaa za ufadhili wa adidas porojo.
B)kwa mustakabali wa mpira wetu kim bado alikuwa n muhimu sana ukiangalia jinsi alipotutoa na hata plan zake kulitakiwa apewe mikakati ili aweze kuwa na maandalizi mazuri.
C) Binafsi bila kuficha nina mashaka sana na uongozi wa malinzi kwanza kulazimisha kubakia mwenyekiti wa mpira kagera ina maana hakuna wa kumpokea uongozi wa kagera na yy akabakia na urais wa tff pekee.

Embu tuchukulie masuala kwa upana wake kuna mambo unayaona kabisa hayaendi kama mwanzo kabisa enzi za tenga,tusiache mkuu tupige kelele ni kwa kuwa tunapenda mpira na ndio burudani iliyopo.
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi;umesema kuwa tubadili jina la Taifa Stars sababu halina maana kwetu!

Je si ni vyema ukaanza kubadili jina la Team ya Mkoa wa Kagera ambao wewe ni Mwenyekiti ?Hili jina la Team ya mkoa wa Kagera"Lweru Eagles" likiwa na maana ya "Tai mweupe"lina maana gani kwa wana Kagera?Kuna Tai weupe Kagera?

Nashauri libadilishwe kwanza hili la Kagera then ifuatie Taifa Stars
CC: rubaman MKALIKENYA

Neno LWERU kwa kihaya ni ZIWA VICTORIA lweru eagles ni Tai wa Ziwa victoria,lweru sio "nyeupe".
 
Last edited by a moderator:
Lkn dada Mamndenyi hata hili lililo chini ya uwezo wa Malinzi la kuajiri kocha wa team ya Taifa tusimlamu?Kwa nn kamleta kocha weeks 2 kabla ya mashindano haya makubwa?

Kama alikuwa hana uhakika wa kocha huyu kuwahi na programs za kuikabili Zimbabwe May 16 kwa nn alimfukuza kocha Kim?

Mambo mengine dada yanahusu directly utawala wa Malinzi na ni mapya kabisa!

Nikusaidie Malafyale na born again pagan mshazari na wengine
Awali CAF waliamua Afcon qualifiers for Morocco 2015 ziwe twelve groups na zichezwe Sept to Nov 2014.Ilikuwa kila group winner aende Morocco plus two best losers na host,total 16,na hadi mashindano ya CHAN south africa mwanzoni mwa mwaka huu hali ilikuwa hivyo,kipindi hicho hata website ya CAF ilisema hivyo.Tulipomtoa Poulsen ( kwa sababu ambazo kimaadili si vyema kumsema mtu ambaye hawezi kujitetea jf)tulijua tunajipanga for september 2014,ghafla CAF wakabadili utaratibu na kusema kutakuwa na pre qualifiers and then group stage,hatukuwa na njia zaidi ya kufumua mipango yetu na kujipanga upya,hiyo ndiyo dhamana ya uongozi.
Mpango wa maboresho ya Taifa stars (ambao unfortunately unauita bonanza),ulibuniwa Novemba mwaka jana tukiamini vijana hao tungewaandaa kuelekea qualifiers septemba,haikuwa hivyo.
Neverthe less hakuna kilichoharibika,wapo ambao Nooij karidhika nao amewachukua National team,waliobaki amewatengenezea program maalum ya mafunzo ataitangaza mwenyewe soon.All in all TFF tumeridhika na tulichokifanya.
 
Last edited by a moderator:
Malafyale yupo sa hii kuna mambo jaman pale tff yanaenda hovyo sana tena sanaaa mpaka inakera,
I)kuhama toka pale karume kwenda kupanga katikati ya jiji hili nalo linahitaji degree kufikiri??
II)Kumfukuza kocha kim bila sababu ya msingi na pesa za kukatisha mkataba zimetoka mifukoni kwa wachache hii kweli ndio inavyopaswa wadau,embu tuelezane ukweli c kulalamika mh rais hapa unahitaji kulisemea ili wadau tukuelewe unatakiwa utambue tff c yako n ya wadau na wapenzi wa mpira ipo siku wadau watagoma kuingia uwanjani hapo utasemaje.
III) Taifa stars yako haina mvuto mechi mbili angalia mwenyewe watazamaji wamepunguza mwamko kulingana na mipango yako isiyo tekelezeka mh rais.
IV)mpaka sasa mechi na zimbabwe haijulikani itachezwa wapi ili wapenzi wa mikoani tujipange kama n mbeya wekeni wazi wakubwa wa tff

mshazari michoro ya uwekezaji vitega uchumi Karume karibu inakamilika,muda wowote TFF itatangaza tenda ya ujenzi.Huwezi kuwekeza katika nyumba ambayo unakaa humo humo.
 
Last edited by a moderator:
Vp kuhusu timu zinazomilikiwa na Majeshi?? Je mliweka utaratibu wowote kuzihusu??
Manake isifike kipindi Kwenye timu 16 kwenye Ligi za JKT,JW,MAGEREZA,POLISI ni 10..Hapo patakuwa na tatizo kwenye soka letu la Tz...
PILI Ndugu Malinzi hili suala la Ligi yetu kusimama kwa kipindi kirefu katikati ya msimu kana kwamba tunapisha Msimu wa Baridi mnalichukuliaje??

pachanya tukijaliwa mashindano mapya yataanzishwa karibuni na pia kuwa na timu 16 za ligi itapunguza muda wa break.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu malafyale naanza kuamini zile sarakasi za malinzi kukimbilia mahakamani kutaka kuzuia uchaguzi haya ndio matunda yake,kuna mambo yanatia kichefuchefu suala la kuhama ofc ya karume kuwa wanapisha ujenzi??mm watu wa kagera nawatambua sana hapo aliona ofc haiendani na hadhi yake hakuna ka ujenzi nipo na tutakuja kuelezana humu.
A)kutubadilidhia jezi ya timu ya taifa kienyeji na blaa blaa za ufadhili wa adidas porojo.
B)kwa mustakabali wa mpira wetu kim bado alikuwa n muhimu sana ukiangalia jinsi alipotutoa na hata plan zake kulitakiwa apewe mikakati ili aweze kuwa na maandalizi mazuri.
C) Binafsi bila kuficha nina mashaka sana na uongozi wa malinzi kwanza kulazimisha kubakia mwenyekiti wa mpira kagera ina maana hakuna wa kumpokea uongozi wa kagera na yy akabakia na urais wa tff pekee.

Embu tuchukulie masuala kwa upana wake kuna mambo unayaona kabisa hayaendi kama mwanzo kabisa enzi za tenga,tusiache mkuu tupige kelele ni kwa kuwa tunapenda mpira na ndio burudani iliyopo.

mshazari mkataba kati ya adidas,CAF na TFF upo ulisainiwa kabla sijaingia madarakani,ukitaka njoo ofisini utaonyeshwa,kilichofanywa na uongozi wetu ni kuutekeleza,kumbuka hizi jezi usizozipenda kontena lililetwa zamani mwaka 2012,nililikuta.Unanihukumu kwa hili ndugu yangu,huoni unanionea?
 
Last edited by a moderator:
Mh rais nashukuru kwa majibu yako ila naomba ufafanuzi kidogo.-
I) kulikuwa na ulazima gani wa uongozi wenu kutumia jezi ambazo wenzenu waliona hazina mvuto timu ya taifa inawakilisha nchi n bendera ya nchi husika,naomba ufafanuzi.

II) Mechi kati ya Taifa stars na ZImbwabwe itafanyika wapi n vyema tukajua mapema ss tulioko mikoani tunapenda kuja kuishangilia timu ya taifa.
 
Ya kwangu kajibu moja kati ya yote niliyouliza mh rais jitahidi kujibu hoja zetu angalao upunguze mashaka ambayo wadau waliowengi wameanza kuonyesha kwenye uongozi wako
 
mikataba huwa inasainiwa ili iheshimiwe,TFF ilisaini mkataba,ikaambiwa tupe rangi za bendera,zikapelekwa kuwa ni blue,njano,kijani na nyeusi,wakubwa wakatengeneza jezi wakatia kwenye ndege wakatuletea,unageukaje na kusema mbaya sizitaki?Tuvumilie mwezi January tutaanza kutumia mpya zenye mwonekano bora.
Wapi itafanyika mechi vs Zimbabwe tutajua punde
 
Hujajibu kuhusu timu za majeshi.

FIFA na CAF waliagiza tuingize kipengele cha club licencing kwenye katiba za vyama wanachama,TFF tulitekeleza hili mwaka jana.Moja ya masharti ya club licencing ni kuwa mmiliki mmoja haruhusiwi kumiliki zaidi ya club moja kwenye ligi moja.Ni muhimu wahusika wote tukalielewa hili kwa kuwa ni la kikatiba.
 
Ya kwangu kajibu moja kati ya yote niliyouliza mh rais jitahidi kujibu hoja zetu angalao upunguze mashaka ambayo wadau waliowengi wameanza kuonyesha kwenye uongozi wako
Unategemea 100% perfection katika uongozi wa Malinzi? Duniani humu hakuna kiongozi ambaye ni mkamilifu assilimia mia.We always try our best,kikubwa ni kuwa na nia thabiti na ujasiri wa kutoa maamuzi unayoamini ni sahihi.
 
FIFA na CAF waliagiza tuingize kipengele cha club licencing kwenye katiba za vyama wanachama,TFF tulitekeleza hili mwaka jana.Moja ya masharti ya club licencing ni kuwa mmiliki mmoja haruhusiwi kumiliki zaidi ya club moja kwenye ligi moja.Ni muhimu wahusika wote tukalielewa hili kwa kuwa ni la kikatiba.

Utekelezaji wa Hiyo kanuni Itaanza Msimu upi?? Bado tunaona mmiliki mmoja (Mfano JKT) Akiwa na club 3 kwenye Ligi yetu?
PILI; Hongereni Sana kwa kuwa na Website Nzuri...manake bado Taasisi nyingi zinaendeshwa ki-anolojia zaidi Tanzania...Ila Jitahidini ku-update ili tuwe tunapata habari nyingi na Muhimu za masuala ya Soka letu/Timu ya Taifa...Manake nimejaribu kutafuta taarifa kuhusu mechi yetu inayokuja ila nimeambulia patupu...
 
Neno LWERU kwa kihaya ni ZIWA VICTORIA lweru eagles ni Tai wa Ziwa victoria,lweru sio "nyeupe".

Hivi sisi wana-Kagera tusio wahaya tulishirikishwaje katika kuchagua jina la timu ya mkoa nasema hivi kwa sababu according to you jina lipo kihaya inaelekea hali-represent wana-kagera wote. Just concerns sio ukabila.
Pili sioni sababu ya kubadili jina la Taifa Stars sababu lipo kiswahili na kiswahili ndo kinachotuunganisha Watanzania (Bara na Visiwani) wote.
CC Malafyale
 
Back
Top Bottom