Vp kuhusu timu zinazomilikiwa na Majeshi?? Je mliweka utaratibu wowote kuzihusu??
Manake isifike kipindi Kwenye timu 16 kwenye Ligi za JKT,JW,MAGEREZA,POLISI ni 10..Hapo patakuwa na tatizo kwenye soka letu la Tz...
PILI Ndugu Malinzi hili suala la Ligi yetu kusimama kwa kipindi kirefu katikati ya msimu kana kwamba tunapisha Msimu wa Baridi mnalichukuliaje??
Hapa kama kuna conflict of interests au ni macho yangu? hizo timu zote nne zipo chini ya wizara kama 2, si kuna kipengele cha FIFA/CAF kinachozuia haya?
CC Malafyale, Jamal Malinzi
Nikusaidie Malafyale na born again pagan mshazari na wengine
Awali CAF waliamua Afcon qualifiers for Morocco 2015 ziwe twelve groups na zichezwe Sept to Nov 2014.Ilikuwa kila group winner aende Morocco plus two best losers na host,total 16,na hadi mashindano ya CHAN south africa mwanzoni mwa mwaka huu hali ilikuwa hivyo,kipindi hicho hata website ya CAF ilisema hivyo.Tulipomtoa Poulsen ( kwa sababu ambazo kimaadili si vyema kumsema mtu ambaye hawezi kujitetea jf)tulijua tunajipanga for september 2014,ghafla CAF wakabadili utaratibu na kusema kutakuwa na pre qualifiers and then group stage,hatukuwa na njia zaidi ya kufumua mipango yetu na kujipanga upya,hiyo ndiyo dhamana ya uongozi.
Mpango wa maboresho ya Taifa stars (ambao unfortunately unauita bonanza),ulibuniwa Novemba mwaka jana tukiamini vijana hao tungewaandaa kuelekea qualifiers septemba,haikuwa hivyo.
Neverthe less hakuna kilichoharibika,wapo ambao Nooij karidhika nao amewachukua National team,waliobaki amewatengenezea program maalum ya mafunzo ataitangaza mwenyewe soon.All in all TFF tumeridhika na tulichokifanya.
Utekelezaji wa Hiyo kanuni Itaanza Msimu upi?? Bado tunaona mmiliki mmoja (Mfano JKT) Akiwa na club 3 kwenye Ligi yetu?
PILI; Hongereni Sana kwa kuwa na Website Nzuri...manake bado Taasisi nyingi zinaendeshwa ki-anolojia zaidi Tanzania...Ila Jitahidini ku-update ili tuwe tunapata habari nyingi na Muhimu za masuala ya Soka letu/Timu ya Taifa...Manake nimejaribu kutafuta taarifa kuhusu mechi yetu inayokuja ila nimeambulia patupu...
Hivi sisi wana-Kagera tusio wahaya tulishirikishwaje katika kuchagua jina la timu ya mkoa nasema hivi kwa sababu according to you jina lipo kihaya inaelekea hali-represent wana-kagera wote. Just concerns sio ukabila.
Pili sioni sababu ya kubadili jina la Taifa Stars sababu lipo kiswahili na kiswahili ndo kinachotuunganisha Watanzania (Bara na Visiwani) wote.
CC Malafyale
Maelezo murua kama haya ndiyo huwa tunayakosa kutoka kwa watawala wetu!Umenieleza vyema na nimekuelewa na uwe unafanya hivi kila ukiulizwa na wala usichukulie maswali yetu kama chuki binafsi!
Chukua "like"yangu!
La Lweru eagles hilo nalo neno.Taifa cup ikirudi tutaliangalia,ila kumbuka timu ya mkoa wa shinyanga inaitwa IGEMBENSABO
CAF kwa sasa wanasisitiza tuanze utekelezaji wa kanuni ya club licencing,hasa kwa vilabu vinavyoshiriki champions league na confederation cup Africa.Muda ukifika tuta comply kwa vilabu visivyocheza Africa championship.
Club licencing regulation lengo lake ni kuboresha uendeshaji wa vilabu vyetu kwa kuvilazimisha viwe na viwanja vya mazoezi,viwe na ofisi,viajiri mtunza fedha,viwe na youth programme nk
La Lweru eagles hilo nalo neno.Taifa cup ikirudi tutaliangalia,ila kumbuka timu ya mkoa wa shinyanga inaitwa IGEMBENSABO
La Lweru eagles hilo nalo neno.Taifa cup ikirudi tutaliangalia,ila kumbuka timu ya mkoa wa shinyanga inaitwa IGEMBENSABO
Unategemea 100% perfection katika uongozi wa Malinzi? Duniani humu hakuna kiongozi ambaye ni mkamilifu assilimia mia.We always try our best,kikubwa ni kuwa na nia thabiti na ujasiri wa kutoa maamuzi unayoamini ni sahihi.
mzee Ndolanga mchango wake kwenye mpira wa Tanzania ni mkubwa na ninamuheshimu sana.Kumbuka pamoja na kutokuwa na udhamini kwenye 90's Tanzania ilifikia namba 65 kwenye FIFA rankings.
Mkuu hujajibu ni sababu au kanuni zipi ambazo TFF imetumia katika suala la Domayo ku-sign Azam iliyopeleka wewe kama Rais kuajiri lawyer kuchunguza hilo suala.je ni kosa kisheria mchezaji kusajiliwa akiwa timu ya taifa? Je tutaamini vp kwamba hujaongozwa na mahaba yako binafsi kwa maana ya conflict of interest since you are Yanga member ?
sasa JAMAL MALINZI huku ndiko unapaswa kuelekea;
mambo ya majaribio tupunguze: Timu ikae pamoja muda mrefu, itazoea kucheza kwa pattern fulani. Kama mnafanya maboresho mnaboresha kidogo kidogo.
huwezi kuongeza wacheza 10 kwa wakati mmoja. inavuruga pattern ya timu.
MIFANO:
Brazil iliyocheza kombe la Mabara na Brazil iliyoteuliwa juzi ni ileile.
Hispania imeendelea kuwa ileile: Xavi, Iniesta, Fabregas, Ramos, Cassilas, Pique, ..huwezi kuona wanabadili timu nzima. Hiyo itasaidia kuwa na 'stability' kwenye timu.
π
timu ya taifa ni tofauti na klabu.
Mh rais mpira wa Taifa stars na Zimbabwe unacheza mbeya hii n kulingana na taarifa zilizopatikana baada ya kufanyika ukaguzi kwenye uwanja wa sokoine mjini mbeya,labda unitoe mashaka nn hasa kigezo ulichotumia mh rais? Unahis timu ikicheza dar itakosa mapato kwa kuwa haina mvuto??
Kaka Jamal; sasa nafasi ya #122 au sivyo?
Mkakati ungefanywa angalau timu ifike # 100 alaf mambo mengine yazungumzwe wakati huo.
Kwa sasa punguzeni kufanya majaribio na team ya taifa. Mpira wa timu ya taifa ni matokeo ya muda mfupi. RAha ya mashabiki ni ushindi.
Kinyume na hapo timu itakosa support!
Mwacheni kocha achague wachezaji 'the best' for the job.
Haiwezekani mtu anawekwa benchi kwenye yake; akija timu ya taifa anapata namba.
let's be serious kidogo.
Aliyekutangulia amewahi kuifikisha hii timu karibu na #100.
Be focused. mambo mengine mtafanya muda ukiruhusu. Kwa sasa irudishe 'timu' #100.π
born again pagan kinachogomba hapa sio usajili wa mchezaji (hilo ni suala la players status commitee) na muda wa kushughulikia usajili bado,kinachochunguzwa na wakili ni kwamba je kulikuwa na ukiukwaji wa miiko ya maadili ya National Team camp? Ni hilo tu.
Na tusubiri matokeo ya uchunguzi wa wakili na adhabu itakayotolewa kama ni kwa player au timu (Azam).