Maswali na ushauri kwa Malinzi

Rais mkutano mkuu wa kawaida utafanyika lini?

Kamati ya utendaji ndiyo yenye mamlaka ya kupanga tarehe ya mkutano mkuu.Itakaa wiki ijayo na kupanga tarehe ya mkutano mkuu
 
mashindano ya vijana U20 ngazi ya vilabu yatafanyika na hayatafanyika dar es salaam.Punde atatangazwa mdhamini mpya wa mashindano haya ya vijana umri chini ya miaka 20
 
Last edited by a moderator:
Achana na Malinzi, yeye anajali maslahi yake tu si mpira as such, hata akitoa povu kuwa anataka kuendeleza mpira wa vijana. Ndiyo hao hao wakina James Rugemalila, utapeli tu

Thanks
 
Achana na Malinzi, yeye anajali maslahi yake tu si mpira as such, hata akitoa povu kuwa anataka kuendeleza mpira wa vijana. Ndiyo hao hao wakina James Rugemalila, utapeli tu

James Rugemalila anahusika vipi hapa? acha watu wa mpira wazungumze mpira .....
 

Kwa mipango hii..ikifanikiwa...hatua nzuri...hongera. Jamal Malinzi
 
Last edited by a moderator:
rais baada ya kumaliza muda wake aliyekuwa mkurungenzi wa bodi ya ligi tumeshuhudia ofisi hiyo akikaimishwa katibu muhitasi hapa unasemaje?

ikumbukwe ofisi hii ni nyeti sana hasa namna ya kutafuta wafadhiri juu ya kubaoresha ligi daraja la kwanza na ligi kuu, pale ofisini naona kuna baadhi ya vijana wana elimu ya kutosha iweje waachwe achukuliwe mtu kama huyo napata mashaka sana RAIS
 
Rais wakati unaingia madarakani ulitwahidi kuwa mpira utachezwa nchi nzima hapa unasemaje?
Pia Rais ulisema umeagiza vifaa vya michezo kwa ajili ya watoto hasa kuanzia miaka 12 na kuendelea mashuleni na ukasema umepakia kwenye makontena viatu used na mipira size 2,3,4 hapo unasemaje?
 
Suala la CEO wa bodi ya ligi ni nyeti,litajadiliwa wiki ijayo kwenye kikao cha kamati ya utendaji.Kwa sasa ligi imesimama hivyo shughuli za bodi si nzito sana
 

ikizu ni kweli tuna container moja bandarini tunahangaika na ushuru,limetoka UK na punde nusu container nyingine itatoka Belgium.
Jitihada za ku spread the game zimefanywa kwa namna mbili,mosi Ligi daraja la kwanza makundi yamehusisha timu 12 badala ya saba za awali ,pili tumefufua ligi daraja la pili ambalo kila mkoa wa Tanzania umetoa timu.
 
Last edited by a moderator:
Rais naomba nikuulize swali dogo,
Mkuu vipi kuhusu ziara zako za kutembelea wanachama wako ili kujionea utendaji kazi wao imeishia wapi? ikumbukwe ni mikoa miwili tu ninayojua umeisha enda nayo ni Songea na Kilimanjaro.

swali lingine ni kuhusu deni mnalodaiwa na PUNCHLINE lakini nashangaa amekamata basi lako lakini bado unampa kazi kulikoni?
 
Rais vipi kuhusu vyama shirikishi ulivipangishia ofisi laki sijui kama vilishaanza kuitumia au ndo hela za cago star zimepotelea hapo?
 

ikizu ni kweli nimetembelea ruvuma ,arusha,manyara na kilimanjaro.Tukijaliwa mapema mwakani nitatembelea iringa mbeya na rukwa.
Punchline ni kweli kuna kipindi aliendelea kufanya biashara na TFF ilihali tuna kesi naye,nilipopata taarifa nilichukua hatua
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi, umefungwa hata na Burundi tena kwenye sherehe za Uhuru, inabidi uachie ngazi haraka sana.

cc Bushoke
 
Last edited by a moderator:
Kumbuka hizo ni mechi za kirafiki za kukisuka kikos cha taifa stars
 
Ongea na serikali hasa wizara ya elimu iteue shule moja ya sekondari na shule moja ya msingi yenye eneo la kutosha kutoka kila mkoa alafu mzitengenezee miundo mbinu ya kimichezo ili ziwe shule maalumu za kimichezo kwa soka la wanaume na wanawake yaani vijana wenye vipaji watakao kuwa wanaimbuliwa kutoka michuano mbalimbali kimkoa wanawekwa pamoja na huku wanaendelea na masomo yao.

Shue hizi ndizo zitakazo kuwa mazizi ya wanamichezo lakini mkiwa na lengo la kufika ngazi ya wilaya baada ya ngazi ya mikoa kuimarika.Kwa mtazamo wangu ni kuwa tutakuwa tumelea vipaji vya lika lote kwa urahisi.

Wazazi wanaweza kuchangia sehemu ya gharama za chakula na vifaa, TFF mkachangia gharama za wataalamu na michezo na serikali ikabaki na jukumu la uendeshaji kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…