@Jamal Malinzi
Juzi, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alisema
Chombo pekee chenye mamlaka ya kutolea uamuzi rufaa ya Ndumbaro ni Kamati ya Rufaa ya TFF, ambayo haijakutana hadi sasa kutokana na wajumbe wake kuwa na majukumu yao.
"Kamati ya Rufaa ya TFF ni chombo huru na kinachojitegemea. Wajumbe wake siyo waajiriwa wa TFF hivyo shirikisho haliwezi kuwalazimisha wakutane kujadili rufaa hiyo wakati wao wenyewe wana taratibu zao walizojiwekea kukutana," alisema Mwesigwa
Baadae mwana sheria wa TFF Mbwelezeni akasema
Hata hivyo, jana, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamidu Mbwezelani alisema siyo kweli kwani wao wapo, ila hawajapata taarifa yoyote ya kuitwa kwa ajili ya kukaa na kuijadili rufaa hiyo, hivyo TFF waseme ukweli.
Alisema TFF ndiyo yenye jukumu la kupokea rufaa zote na kuzipeleka kwa kamati husika, kisha kuwaarifu wajumbe wote wa kamati ili wajue lini wanatakiwa kujadili rufaa hizo.
"TFF waseme ukweli kwani sisi tupo mbona na hatuwezi kufanya chochote mpaka tuarifiwe kuhusu uwepo wa rufaa hiyo na kamati iitwe, lakini hatujawahi kupata barua yoyote kuhusu jambo hilo na hata nimewauliza wenzangu kama nao wamewahi kupata barua kuhusu kuijadili rufaa hiyo wameniambia hapana, sasa nashangaa haya mambo yanatoka wapi.
Haya naongea mm
Kwenye sheria tunasema JUSTICE DELAYED IS JUSTICE DENIED!Mpeni Dr Ndumbaro haki yake ya msingi ya kusikilizwa!!Kama ana kosa atatiwa tu hatiani maana naona kama kuna mchezo wa kuogopa kumpeleka mbele ya kamat kujieleza
Malinzi zingatia UTAWALA wa KISHERIA please
Then Wakili Mbwelezeni akachomelea msumari wa mwisho na mchungu zaidi kwa TFF
Kupakaziana si wakati wake na mimi sio mnafiki ni mtu ninayependa ukweli, nipo Dar es Salaam kwa miezi miwili, mwanzoni nilikuwa mgonjwa, lakini mbona sijawahi kuona wametutaarifu kuwa tunatakiwa kukaa na kujadili lolote," alisema.
Aliongeza: "Kama TFF wanasema sie tuko bize (tuna shughuli nyingi), basi wamjibu Ndumbaro kuwa hawa wanaohusika na rufaa yako wako bize, lakini si kumpiga danadana.
"Sijasikia, sijaona hiyo barua kutoka TFF ya kutuita tukae tujadili rufaa ziliopo mezani, hivyo TFF waseme ukweli unafiki siyo sehemu yake."