Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

Rais vipi kuhusu vyama shirikishi ulivipangishia ofisi laki sijui kama vilishaanza kuitumia au ndo hela za cago star zimepotelea hapo maana naona waliopo hapo ni FRAT au ndo waliokupigia kura wakati wa uchaguzi? na hao wengine bado wanavinyongo na wewe?
 
mkuu pole kumbe hujui mikoa inayotoza ada ya ushiriki ya copacocacola basi ni hii hapa ifanyie kazi,
1-Kigoma
2-Mwanza.
ila mkuu kwa kigoma hata jezi mnazowagawia watoto mwisho wa mashindano hunyang'anywa na kuziuza mtaani
nafuatilia
 
Rais vipi mbona kamati zoko hazifanyi maamuzi na kutoa adhabu kwa vilabu/mchezaji wanaofanya vurugu michezoni hasa ligi daraja la kwanza na ligi kuu.
 
Rais tff tafadhari sana mpira kushieikiana na znz NO wao waliomba fifa na caf kuwa wanachama caf wamwaruhusu na waendelee vivyo hivyo na wala sioni sababu ya kushiriki mapinduzi cup
 
Rais vipi mbona kamati zoko hazifanyi maamuzi na kutoa adhabu kwa vilabu/mchezaji wanaofanya vurugu michezoni hasa ligi daraja la kwanza na ligi kuu.

ikizu ni kweli vurugu mpirani hazikubaliki.Leo tumezuia uwanja wa Karume musoma usitumike kwa mechi za ligi wakati kamati husika zinajiandaa kusikiliza mashauri husika.Nakuhakikishia hatua kali zitachukuliwa.
 
Last edited by a moderator:
Rais tff tafadhari sana mpira kushieikiana na znz NO wao waliomba fifa na caf kuwa wanachama caf wamwaruhusu na waendelee vivyo hivyo na wala sioni sababu ya kushiriki mapinduzi cup

Chama cha mpira Zanzibara ZFA sio mwanachama wa FIFA bali ni mwanachama mshiriki wa CAF.Mapinduzi cup ni muhimu katika kuimarisha mahusiano yetu ya kiutamaduni na kimichezo.
 
Majuzi Hollyman alifungua thread ya aina hii.Nia na lengo lake lilikuwa ni zuri,namshukuru.Nimeamua nifungue mwenyewe hii thread ili iwe ni uwanja wa kudumu wa kuniuliza maswali,kutaka ufafanuzi na pia kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya mpira wetu.Kwa ruhusa ya moderators ninaomba uwe ni ukurasa wa kudumu hapa jf.
Jamal Malinzi
Rais wa TFF
Dar es salaam 04/Feb/2014

Mkuu Jamal malinzi una mkakati wowote wa kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa @TFF ili iweze kuwa na matumaini walau ya kupata timu ya Taifa miaka 5 mbele kutokana na jitihada zako za sasa.
 
Last edited by a moderator:
Chama cha mpira Zanzibara ZFA sio mwanachama wa FIFA bali ni mwanachama mshiriki wa CAF.Mapinduzi cup ni muhimu katika kuimarisha mahusiano yetu ya kiutamaduni na kimichezo.

usilete mambo ya siasa kwenye mpira achana nao zanzibar ni mzigo wala usije ukaleta aina furani ya mashindano ya mpira na zanzibar
 
Mkuu Jamal malinzi una mkakati wowote wa kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa @TFF ili iweze kuwa na matumaini walau ya kupata timu ya Taifa miaka 5 mbele kutokana na jitihada zako za sasa.

MeinKempf (my fight) ndio maana tumeanzisha programme ya kitaifa ya maboresho,program hii ni ya kudumu na wakati wote itakuwa inalenga kuibua na kuendeleza vipaji vipya kwa ajili ya Taifa stars na Twiga stars.Kwa sasa timu ya Taifa ya maboresho ina camp mara moja kwa mwezi na kucheza mechi moja aidha local au international.Mwezi huu tar 22/01 inacheza na Rwanda,February itacheza local game dhidi ya timu ya premier league
 
Last edited by a moderator:
Samahani Jamal Malinzi nina swali fupi. Hivi hamuoni kwamba imefika wakati muanzishe soccer academy muanze kuwafunza watoto wa miaka 10 wenye vipaji vya soka? Huwezi kumfunza mtu soka ila unaweza kumuongezea ujuzi wa ziada sana sana nidhamu ya soka. Hivi wewe kama wewe mtukufu rais unajisikiaje ukisikia boban anavuta msuba ama okwi kaonekana kwenye makanda ya ngono? Mwisho hivi utajisikiaje ukisikia taifa stars wameweka kambi kwenye hoteli ya wasomali katikati kabisa ya jiji hali hamna viwanja vya soka? Au hujifunza ulimbwende? Nijibu kwanza hayo mengine yaja! Samahani lakini.
 
hosam ninakuelewa sana na ninashukuru kwa mawazo yako.Badala ya kufungua academy tumeamua kuboresha zilizopo na kuziongezea uwezo tukianzia na Alliance Mwanza na Lord Baden Bagamoyo.Alliance academy watachukua vijana wetu umri chini ya miaka 12 na Lord baden watachukua vijana umri chini ya miaka 14.Angalau tumeanza
 
Last edited by a moderator:
sawa mkuu nimekuelewa lakini mnachelewa kuchua hatua hadi wadau tumekuwa na wasiwasi na utendaji kazi wako na kamati zako.
kwanza-- suala la YANGA kufanya vurugu Shinyanga mpaka sasa hakuna aliyeadhibiwa,
pili --- kuna vurungu zinatokea uwanja wa kirumba mwanza na kusababisha mechi mbili hazikuisha, mechi ya Police Dodoma na Toto haikuisha mpaka sasa hakuna hatua zozote zililizochukuliwa mbali na mwamuzi kupigwa na mechi ya Police Tabora na Toto nayo mechi ilivunjika na wewe umekaa kimya hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na habari zilizoko mtaani inasemekana wewe unaitaka Toto ipande daraja naomba ulitolee taarifa hili kabla halijakuchafua zaidi Rais wangu.
kwa suala la Mara umefanya vizuri maana lilikuweka vibaya maana kuna baadhi ya viongozi wako walichaniwa nguo na kupigwa ni aibuuu mkuu.

NASISITIZA TOA MAAMUZI KUHUSU MECHI ZA TOTO MKUUUUUUUUUUU LITAKUHARIBIA NA ULITOLEE TAARIFA MAANA MPAKA WANASEMA WAKITAKA REFA YOYOTE UNAWAPA KAMA ULIVYOFANYA MECHI YA MWADUI.
 
ikizu mpira haukosi porojo na si Tanzania tu bali dunia nzima.Kamati husika zitakaa soon na maamuzi yatatolewa na ninaamini yatakuwa funzo kwa wengine.
 
Last edited by a moderator:
Jamal malinzi haiwezekani vurugu zitokee mara mbili frequently within a week kwenye uwanja wa ccm kirumba na wahusika kukaa kimya. Hizi ni dalili mbaya kwa chama cha mpira na uongozi wake. Toto haina tofauti na timu ya Stand utd ya mwaka jana. Tunahitaji soka la hapo nyumbani likue ili sisi wadau tupate nafasi ya kuchangia timu za uhakika..!!

maziku masunga nakuomba uvute subira kidogo.Ni kweli vurugu mpirani hazivumiliki.
 
Last edited by a moderator:
wacheni kidogo wachapwe waamuzi nao wamezidi wanaleta kero kwa mfano waamuzi wa mapinduzi cup hovyo kabisa
 
hosam ninakuelewa sana na ninashukuru kwa mawazo yako.Badala ya kufungua academy tumeamua kuboresha zilizopo na kuziongezea uwezo tukianzia na Alliance Mwanza na Lord Baden Bagamoyo.Alliance academy watachukua vijana wetu umri chini ya miaka 12 na Lord baden watachukua vijana umri chini ya miaka 14.Angalau tumeanza

Asante mkuu! Laiti hata rais wa nchi hii angalikuwa kama wewe tungefika mbali! Umenijibu kiufasaha na nashkuru sana.
 
Last edited by a moderator:
@Jamal Malinzi

Juzi, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alisema
Chombo pekee chenye mamlaka ya kutolea uamuzi rufaa ya Ndumbaro ni Kamati ya Rufaa ya TFF, ambayo haijakutana hadi sasa kutokana na wajumbe wake kuwa na majukumu yao.

"Kamati ya Rufaa ya TFF ni chombo huru na kinachojitegemea. Wajumbe wake siyo waajiriwa wa TFF hivyo shirikisho haliwezi kuwalazimisha wakutane kujadili rufaa hiyo wakati wao wenyewe wana taratibu zao walizojiwekea kukutana," alisema Mwesigwa

Baadae mwana sheria wa TFF Mbwelezeni akasema

Hata hivyo, jana, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamidu Mbwezelani alisema siyo kweli kwani wao wapo, ila hawajapata taarifa yoyote ya kuitwa kwa ajili ya kukaa na kuijadili rufaa hiyo, hivyo TFF waseme ukweli.

Alisema TFF ndiyo yenye jukumu la kupokea rufaa zote na kuzipeleka kwa kamati husika, kisha kuwaarifu wajumbe wote wa kamati ili wajue lini wanatakiwa kujadili rufaa hizo.

"TFF waseme ukweli kwani sisi tupo mbona na hatuwezi kufanya chochote mpaka tuarifiwe kuhusu uwepo wa rufaa hiyo na kamati iitwe, lakini hatujawahi kupata barua yoyote kuhusu jambo hilo na hata nimewauliza wenzangu kama nao wamewahi kupata barua kuhusu kuijadili rufaa hiyo wameniambia hapana, sasa nashangaa haya mambo yanatoka wapi.

Haya naongea mm
Kwenye sheria tunasema JUSTICE DELAYED IS JUSTICE DENIED!Mpeni Dr Ndumbaro haki yake ya msingi ya kusikilizwa!!Kama ana kosa atatiwa tu hatiani maana naona kama kuna mchezo wa kuogopa kumpeleka mbele ya kamat kujieleza

Malinzi zingatia UTAWALA wa KISHERIA please

Then Wakili Mbwelezeni akachomelea msumari wa mwisho na mchungu zaidi kwa TFF
Kupakaziana si wakati wake na mimi sio mnafiki ni mtu ninayependa ukweli, nipo Dar es Salaam kwa miezi miwili, mwanzoni nilikuwa mgonjwa, lakini mbona sijawahi kuona wametutaarifu kuwa tunatakiwa kukaa na kujadili lolote," alisema.

Aliongeza: "Kama TFF wanasema sie tuko bize (tuna shughuli nyingi), basi wamjibu Ndumbaro kuwa hawa wanaohusika na rufaa yako wako bize, lakini si kumpiga danadana.

"Sijasikia, sijaona hiyo barua kutoka TFF ya kutuita tukae tujadili rufaa ziliopo mezani, hivyo TFF waseme ukweli unafiki siyo sehemu yake."

Malafyale si vyema mimi kujadili masuala yaliyo mbele ya kamati za sheria.Niseme tu haki itatendeka na si muda mrefu kuanzia sasa.
 
Last edited by a moderator:
Sawa Rais unasema kwmba maamuzi yatatolewa ndani ya siku 7 kwa mujibu wa katiba mbona vurugu za toto ya Mwanza zimeisha pita hizo siku saba?
Rais jihadhari sana na hili suala la Toto maana litakuaribia sana kuna ujumbe wa maandishi uliwahi kuutuma kwa mwenyekiti wako wa kamati ya waamuzi ukimwagiza kufanya malekebisho ya waamuzi wa mechi ya Mwadui na Toto baada ya kupata majungu toka kwa RUFANO.
KUWA MAKINI SANAAAAAAAAAAAAA
 
Back
Top Bottom