Ongea na serikali hasa wizara ya elimu iteue shule moja ya sekondari na shule moja ya msingi yenye eneo la kutosha kutoka kila mkoa alafu mzitengenezee miundo mbinu ya kimichezo ili ziwe shule maalumu za kimichezo kwa soka la wanaume na wanawake yaani vijana wenyevipaji watakao kuwa wanaimbuliwa kutoka michuano mbalimbali kimkoa wanawekwa pamoja na huku wanaendelea na masomo yao. Shue hizi ndizo zitakazo kuwa mazizi ya wanamichezo lakini mkiwa na lengo la kufika ngazi ya wilaya baada ya ngazi ya mikoa kuimarika.Kwa mtazamo wangu ni kuwa tutakuwa tumelea vipaji vya lika lote kwa urahisi. Wazazi wanaweza kuchangia sehemu ya gharama za chakula na vifaa,TFF mkachangia gharama za wataalamu na michezo na serikali ikabaki na jukumu la uendeshaji kwa ujumla.
Ili wazo zuri..
Tena wanaweza hata amua Shule zenye viwanja zkapewa nafasi ya kukarabatiwa japo viwanja tu ili vikizi vigezo.
Wazo zuri kama likiwekwa chini kitaalam.
Maana mpira wa sasa unaambatana na Elimu.
hii pia itawapa nafas za kupata scholarships za michezo kwa nchi mbali mbali.