Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

Sera hii ya Jamal Malinzi na wenzake akina Mayanga HAIJAWAHI kuwepo duniani na inaanzia TZ!Sijapata ona popote duniani nchi ikaendelea kisoka bila kuwekeza!Kama issue ni vijana kuna vijana wengi wanacheza soka la hali juu league zetu!Hawa wa mitaani wameandaliwa lini,wapi na nani?
Tunacheza na Zimbabwe kufuzu mataifa huru baadae mwezi ujao tutegemee kipigo kikali!
Malinzi kashindwa kazi akae miaka yake 4 aondoke!

Kuna yule jamaa mshauli wa ufundi wa bwana malinzi ana jina la asili ya mkoa wa kagera naomba mwenye CV yake juu ya uweledi wake kwenye mambo ya soka hadi kupewa nafasi hiyo nyeti ya kumshauli Rais wa TFF mambo ya ufundi?serious kuna mambo yanaendelea kwenye soka letu mmmmh yangu macho na masikio.
 
Ndugu yangu MKALIKENYA haya ya kuusema uteuzi wa Jamal Malinzi uliongelewa sana hapa!

Mimi napenda na najua misingi ya soka!Kinachofanyika TFF hakipo duniani!Ni kweli soka linaanzia kwa vijana lkn vijana hao hawaokotwi mitaani!
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi tunacheza na Zimbabwe kwenye mtoano wa kombe la Africa weeks 2 zijazo!
1.Kwa nn ulimfukuza Kim bila kumleta kocha mwingine miezi kadhaa nyuma ainoe timu yetu kwa mechi hizi?
2.Maandalizi ya hovyo kama haya ya weeks ndiyo zilikuwa sera zako ulizo ombea kura?
3.Kwa vile kocha mpya ana weeks 2 tu kuifundisha team hii na kucheza na Zimbabwe;Je team aliyorithi imeteuliwa na nani?
4.Mchezaji kama Ivo Mapunda aliyekuwa nyota mashindano ya Challenge miezi 4 tu iliyopita kule Kenya kaachwa ktk teuzi ya Madadi na Mayanga kwa vigezo vipi?
 
Last edited by a moderator:
Timu itacheza Dar es salaam na Zimbabwe mh Rais kuna umuhimu gani wa kuweka kambi mbeya sehemu yenye baridi na viwanja vibovu vya mazoezi ata mechi.
 
Timu itacheza Dar es salaam na Zimbabwe mh Rais kuna umuhimu gani wa kuweka kambi mbeya sehemu yenye baridi na viwanja vibovu vya mazoezi ata mechi.

Tukuyu umefika ukaona quality ya pitch? Unasemaje "viwanja vibovu"? Kumwondoa Kim tuliangalia long term future ya national team na youth football development na sio mechi moja,mpira unajengwa.
 
Mhariri wa gazeti la leo la Nipashe ameuchambua sana uongozi wa Jamal Malinzi tanngu uingie madarakani na maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya, na mhariri alifikia hatua ya kumtaka Malinzi 'aache ushamba'. Baadae kidogo wakiweka hilo gazeti online version nitabandika humu
 
Sijalisoma,nitalitafuta nilisome.All in all hivi ukitaka umkosoe mtu kuna ulazima gani wa kumtukana? Tatizo yeye mhariri wa nipashe amejaliwa kuwa na kalamu na anajua anaowatukana hawana kalamu ya kumjibu,aendelee tu kunitukana,Mungu ni wa wote.Binafsi ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kuwa i am doing my best for Tanzania football tumefanya programme ya uboreshaji timu ya Taifa imetuzalishia wachezaji watano wapya wa National team na watatu wa under 20,uwanja wa karume na Tanga tunamalizia michoro na pesa za kuanzia mradi tumepata,Nyamagana /kaitaba Engineer wa FIFA anakuja wiki ijayo kwa ajili ya nyasi bandia,tukijaliwa January mwakani tutaanza merchandising ya jezi mpya za timu ya Taifa,national youth development plan tunamalizia kuiandaa,tatizo ni nini hasa mpaka mhariri wa nipashe aamue kunitukana?

Rais wangu Malinzi,nafikiri hizo ndio changamoto zenyewe za Uongozi...
Hebu ungesoma kwanza hiyo Makala then ujue unaweza ukaona kama kuna matusi au laaah...
Kwa ufupi lakini Watanzania tunataka tuone Matokeo chanya kwenye soka letu....Tumechoka Tumechoka kuwa wasindikizaji wa nchi nyingine kwenye michuoano ya kimataifa....
Hizo National Youth Dvlp Plan tumezisikia sana tokea tawala zilizopita lakini waaaapi..au kuna maslahi huko?? Hao vijana mnaowandaaa miaka yote wapo wapi???
Nendeni hapo Ivory Coast mkajifunze kwenye kituo cha ASEC Muone vitendo na maneno kidogo...
Simamieni sheria kikamilifu hususani kwa klabu zetu ziwe za kisasa ili tupate wachezaji wazuri....
Tunekwama,tumekwama na Hatuoni kama mna dalili za kutukwamua...
 
Tukuyu umefika ukaona quality ya pitch? Unasemaje "viwanja vibovu"? Kumwondoa Kim tuliangalia long term future ya national team na youth football development na sio mechi moja,mpira unajengwa.

Mheshimiwa rais Tukuyu nimefika nimekaa Rungwe kwa project fulani miezi miwili naufahamu huo uwanja wa chuo ni kwamba ubora wa nyasi zake hauwezi kuwa sawa na uwanja wa taifa ambapo mechi itachezwa lakini mheshimiwa mbona hujajibu issue ya weather sababu kiukweli mbeya hiki ndio kipindi cha baridi kali.
 
Kitu kikubwa nakuomba sana ndugu Rais usipachoke hapa kuwa mvumilivu jibu hoja kama unavyofanya usiwe na jazba naamini wote tuna lengo moja la kujenga soka letu nauona mchango wa jukwaa hili utapata mengi hadi yale ya uvunguni kuliko watu waongelee chumba acha waongee hapa na wasio wastaarabu watukune lakini usichoke kuwajibu wote mwisho wa siku utapata matokeo chanya kwenye mipango yako TUKO PAMOJA.
 
Kamati ya utendaji ya TFF imemaliza kikao chake,kuanzia msimu wa 2015/16 ligi kuu itakuwa na timu 16.
 
Rais wangu Malinzi,nafikiri hizo ndio changamoto zenyewe za Uongozi...
Hebu ungesoma kwanza hiyo Makala then ujue unaweza ukaona kama kuna matusi au laaah...
Kwa ufupi lakini Watanzania tunataka tuone Matokeo chanya kwenye soka letu....Tumechoka Tumechoka kuwa wasindikizaji wa nchi nyingine kwenye michuoano ya kimataifa....
Hizo National Youth Dvlp Plan tumezisikia sana tokea tawala zilizopita lakini waaaapi..au kuna maslahi huko?? Hao vijana mnaowandaaa miaka yote wapo wapi???
Nendeni hapo Ivory Coast mkajifunze kwenye kituo cha ASEC Muone vitendo na maneno kidogo...
Simamieni sheria kikamilifu hususani kwa klabu zetu ziwe za kisasa ili tupate wachezaji wazuri....
Tunekwama,tumekwama na Hatuoni kama mna dalili za kutukwamua...

pachanya inakera kuona mhariri wa gazeti linalo heshimiwa na kuthaminiwa na jamii kama nipashe kwa makusudi mazima anaamua kunidhalilisha tena kwa jambo ambalo ninaamini ukweli anaujua ila anaamua,for some reasons,kutukana na kupotosha umma,why? Hoja zako hapo juu majibu ninayo nitakujibu.Believe me we are on a right path.
 
Last edited by a moderator:
Mimi naona rais wa TFF anafanya juu chini kukwepa maswali mengi ya msingi kwa kuongea kazi kadhaa zilizofanywa na TFF, nakupa pongezi kwa hili kwa kutumia tricks za wanasiasa. Unatuambia vitu tusivyotaka kuvisikia wakati tunavyokuuliza huvijibu. Mkalikenya kauliza swali la weather ambalo nadhani ni la msingi ikizingatiwa mechi vs Zimbabwe inaweza kuchezwa Dar-es-salaam kwenye joto la kati ya 28C- 30C lakini kambi inafanyika mbeya kwenye joto labda la 16C-20C sijui hii kambi itawasaidiaje wachezaji wetu zaidi ya utalii. Kama mechi itafanyikia Mbeya labda naweza kuona umuhimu wa kuweka kambi Mbeya. Rais wa TFF na crew yako naomba upay attention jinsi wenzetu wanavyojiandaa na kombe la Dunia uone wanavyoweka kambi na kucheza mechi za kirafiki katika miji mechi zitakapofanyika ili wazowee hali ya hewa hutaona nchi ya ulaya inakwenda kupiga kambi sehemu yenye baridi kujiandaa na kombe la dunia katika geographical zone yenye joto kali. Afu jambo la kuajiri kocha karibia na pambano la muhimu kama hili halitasaidia hii nchi hata siku moja. Jambo la maana mngesubiri mechi ipite ndo mumtimue Kim au mngemwajiri kocha mpya mapema zaidi ili awe na muda wa kujua viwango vya wachezaji na kutafuta jinsi ya kusahihisha mapungufu waliyonayo wachezaji wetu, ambayo ni mengi wewe mwenyewe na wapenzi wote wa soka la Bongo tunayajua na kuyaona. Anyway, naona hutaki kujibu maswali ya Malafyale kwa sababu zisizojulikana
 
Anyway, naona hutaki kujibu maswali ya Malafyale kwa sababu zisizojulikana
Ndugu rubaman agandi gandi?
Mkuu wala haina haja ya kumuambia chochote Jamal Malinzi kwani ipo confirmed kuwa huyu Mlangira mwenzako ni mbambaishaji tu;Katurudisha enzi za utawala wa hovyo hovyo wa Ndolanga na Rage!

Wkt tuna mechi ngumu na Zimbabwe within a weeks lkn jana anatuambia tujiandae kupiga kura kuchagua jina jipya la kuipa Taifa Stars!Huyu mtu sielewi hata alimshinda vipi Nyamlani

Unamfukuza kocha Kim mapema lkn unamleta mbadala wake weeks 2 kabla ya mechi ngumu na Zimbabwe na akirithi chaguo la wacgezaji toka kwa incompetent Mayanga na Madadi!Miaka 4 mingine ya maumivu kwenye soka letu

Mechi inachezwa Dar kwenye joto lkn unaipeleka team Tukuyu kwenye baridi kali hadi usiku inadondoka barafu!Wakili Mtingojela alikuwa sahihi kukata jina la Malinzi kwa mustakabali wa TZ!Maneno aliyoniambia Rukambura sasa yananiingia akilini!
 
Last edited by a moderator:
Hoja zako hapo juu majibu ninayo nitakujibu.Believe me we are on a right path.

We are on a right course kumpa kocha team ajiandae na mechi ngumu bado weeks 2?
Kocha wa Team ya Taifa kusimamia team asiyoichagua?
Kipaumbele chako kuwa kupiga kura kuchagua jina la Taifa Stars?
Kuiweka Taifa Stars kwenye baridi Tukuyu badala ya Dar sehemu watakayo cheza mechi zao
Kung'ang'ania madaraka na kuhisi ni wewe tu mwenye uwezo kuongoza KRFA?
Kutoa pesa mfukoni mwenu kulipa madeni ya TFF?
Top cream yote ya uongozi wa TFF kutoka Kagera?
Kuingilia internal affairs za vilabu kama vile usajili kabla suala lenyewe kuletwa TFF kwa usuluhshi?
Na bado unataka tuamini kama tupo kwenye mstari sahihi na soka letu!Malinzi maliza muda wako salama uondoke
 
Ndugu rubaman agandi gandi?
Mkuu wala haina haja ya kumuambia chochote Jamal Malinzi kwani ipo confirmed kuwa huyu Mlangira mwenzako ni mbambaishaji tu;Katurudisha enzi za utawala wa hovyo hovyo wa Ndolanga na Rage!

Wkt tuna mechi ngumu na Zimbabwe within a weeks lkn jana anatuambia tujiandae kupiga kura kuchagua jina jipya la kuipa Taifa Stars!Huyu mtu sielewi hata alimshinda vipi Nyamlani

Unamfukuza kocha Kim mapema lkn unamleta mbadala wake weeks 2 kabla ya mechi ngumu na Zimbabwe na akirithi chaguo la wacgezaji toka kwa incompetent Mayanga na Madadi!Miaka 4 mingine ya maumivu kwenye soka letu

Mechi inachezwa Dar kwenye joto lkn unaipeleka team Tukuyu kwenye baridi kali hadi usiku inadondoka barafu!Wakili Mtingojela alikuwa sahihi kukata jina la Malinzi kwa mustakabali wa TZ!Maneno aliyoniambia Rukambura sasa yananiingia akilini!

Malafyale una hoja nzuri lakini jitahidi kubadili njia ya uwasilishaji wa hoja zako kwa jinsi unavyowasilisha kwa shutuma na kumuhukumu waziwazi malinzi sidhani kama ni lengo la jukwaa hili na mimi nadhani usipobadilika mkuu utaharibu utamu na maudhui ya ukurasa huu mahususi please please uungwana ni matendo badilika tusonge mbele.
 
Tutegemee makubwa zaidi ya haya mkuu maana hii sera yake mpya Jamal Malinzi sijui team ya maboreshe HAIJAWAHI KUWEPO sehemu yyt duniani zaidi ya TZ

Mpira ni sera za muda mrefu sio kama hizi za TFF!Hawa vijana wa Tukuyu kabla hawajaenda Tukuyu walikuwa wapi?Walifundishwa na nani?Maneno ya kaka yangu Rukambura kuhusu mategemeo mengi ya watz kuhusu Malinzi naanza kuyakumbuka sasa!

Malinzi ni mbabaishaji tu kamaure you akina Rage enzi zile

Ahsante.....let me assure you Malafyale i am not a fool,i know exactly what i am doing and where i am leading football into,katika uongozi wa mpira toka nikiwa katibu mkuu Yanga nimekutana na characters difficult to deal with nyingi tu hivyo comments zako,rough as they are,i can deal with.Tusubiri tuone who will laugh last.
 
Last edited by a moderator:
Huyu Mainzi bora ya Ndolanga!
Hakuna kitu hapo, ni ujinga tu!

mzee Ndolanga mchango wake kwenye mpira wa Tanzania ni mkubwa na ninamuheshimu sana.Kumbuka pamoja na kutokuwa na udhamini kwenye 90's Tanzania ilifikia namba 65 kwenye FIFA rankings.
 
Kaka Jamal; hoja yangu kwako kwa sasa ni ndogo sana.

timu ya Taifa isiwe mahali pa kukuzia vipaji.
Kila timu ya Premier League (ya Tanzania) si inayo timu ya vijana?

Tena bado kuna timu za vijana za Taifa?

Timu ya taifa inafaa iwe ni mkusanyiko wa wachezaji waliofanya vizuri kutoka katika timu zao.
Kujaza machipukizi taifa kutachelewesha sana mafanikio.🙂

agosti 8 (birthday yangu!),lazima kuwe na mahusiano ya karibu kati ya National senior team coach na makocha wa vijana,vinginevyo vijana hawatapata fursa ya ku break into National team.Lakini pia kumbuka programme ya vijana ni gharama,sasa kama timu za premier zinashindwa hata kununua viatu vya wachezaji,dawa,posho,mishahara,usafiri shida watapata wapi pesa ya kutunza timu ya vijana,ni mtihani kwa kweli.Tunahitaji mpango wa kitaifa wa youth development,tunauandaa
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa rais Tukuyu nimefika nimekaa Rungwe kwa project fulani miezi miwili naufahamu huo uwanja wa chuo ni kwamba ubora wa nyasi zake hauwezi kuwa sawa na uwanja wa taifa ambapo mechi itachezwa lakini mheshimiwa mbona hujajibu issue ya weather sababu kiukweli mbeya hiki ndio kipindi cha baridi kali.

MKALIKENYA aliyekuambia Tanzania vs Zimbabwe itachezewa uwanja wa Taifa ni nani?
 
Last edited by a moderator:
Kitu kikubwa nakuomba sana ndugu Rais usipachoke hapa kuwa mvumilivu jibu hoja kama unavyofanya usiwe na jazba naamini wote tuna lengo moja la kujenga soka letu nauona mchango wa jukwaa hili utapata mengi hadi yale ya uvunguni kuliko watu waongelee chumba acha waongee hapa na wasio wastaarabu watukune lakini usichoke kuwajibu wote mwisho wa siku utapata matokeo chanya kwenye mipango yako TUKO PAMOJA.

huu ukurasa niliufungua kwa nia njema tu,ya kujenga,ila mkiamua kuugeuza uwanja wa fujo sijui itakuwaje.
 
Back
Top Bottom