Maswali ninayojiuliza kwenye huu mgogoro wa DRC

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Nadhani Kagame anawapa ufadhili wa silaha na wanajeshi ili kumsaidia Mtutsi mwenzake anayebaguliwa Congo.

Pia Nadhani, anawapa msaada waasi kwasababu Congo iliwaunga mkono waasi wa kihutu. Unaiunga mkono FDLR basi Nami nitawaunga mkono M23.

Sasa kama Kama ni kweli Rwanda inahusika
1. Kwanini hatuoni vijana wa kikongoko wakiipigania nchi Yao kwa kufa na kupona? Morale ya vita sio silaha au miundombinu bora bali cha kwanza ni ule munkari wa watu kujitolea kufa na kupona....kwanini Wacongo hawana hili???

2. Au ambayo yamekuwa yanalalamikiwa na M23 ndiyo yanayopitiwa na Wacongo wote?

3. Kwanini Kabila yupo kimya? Anamkono gani kwenye hili. Kumbuka makubaliano yake na Hawa waasi March 2009.

4. Je, Nangaa ni mtutsi?
Hakuna hisia mbaya kama za kukataliwa na nchi yako. MTUTSI ambaye vizazi na vizazi vimezaliwa Congo Kisha serikali inamwambia sio Mcongomani kisa tu anazungumza Kinyarwanda.

Mfano mdogo: Mimi Mama mzaa bibi yangu ni Msomali. Simfahamu hata.

Kwa muonekano ukiniona tu japo hadi uwe mdadisi utagundua ninavinasaba vya Kisomali. Lakini mimi sio msomali na hata sipajui.

Mara nyingi nikikutana na wale wabongo wajuaji wananiambia wewe sio mtanzania. Huwa najiskia Vibaya saana kila sehemu ya mwili wangu husisimka. Sasa huyo ni mtu baki....fikiria serikali iniambie hivyo...unafikiri nini kitafuata???
 
Waasi wana pesa za kununua silaha.

Congo kuna vikundi vingi vya waasi ambavyo huwa vinaibuka na kupoa, M23 na Watusi wamekuwa wanasikika zaidi kuliko makundi mengine kwa sababu ya ukubwa wao na mahusiano yao na Rwanda na Uganda.
 
Mara nyingi nikikutana na wale wabongo wajuaji wananiambia wewe sio mtanzania. Huwa najiskia Vijaya saana kila sehemu ya mwili wangu husisimka. Sasa huyo ni mtu baki....fikiria serikali iniambie hivyo...unafikiri nini kitafuata???
Wasomali watu wabaya ni wabuguzi mno kupita kiasi
 
Kutatua mgogoro wa hapo kongo kunahitaji akili na wala sio mabunduki tu!.
Ila kwanini Watutsi wanabaguliwa/wanaona wanabaguliwa kila sehemu waishio? Labda tatizo ni wao!!!!!
 
Waasi wana pesa za kununua silaha.

Congo kuna vikundi vingi vya waasi ambavyo huwa vinaibuka na kupoa, M23 na Watusi wamekuwa wanasikika zaidi kuliko makundi mengine kwa sababu ya ukubwa wao na mahusiano yao na Rwanda na Uganda.
Rwanda inaibaka Drc...
 
Zinapitia wapi?

Kagame hajawahi kujibu swali la kutowasaidia waasi moja kwa moja....! Uso humbadilika.
Silaha zitakuwa zinapita Rwanda na Uganda, inawezekana pia Rwanda ikawa inawasaidia waasi kwa maslahi yake lakini sio kwamba waasi wakikosa silaha huko Rwanda watashindwa kupigana kabisa. Kama hivi wanajeshi wa Congo walivyokimbia watakuwa wameacha silaha nyingi tu nyuma kwenye makambi. Waasi wana njia nyingi za kujipatia silaha kwa sababu biashara ya silaha za magendo duniani ni kubwa sana pia.
 
Ila kwanini Watutsi wanabaguliwa/wanaona wanabaguliwa kila sehemu waishio? Labda tatizo ni wao!!!!!
Inahitaji intelligence kuchimbua hili maana hapa kuna swala la mali pia!, inaweza kuwa uwepo wa mali ktk hilo eneo ikawa ndio sababu zaidi ya hao watutsi kupataka huku wakisema sababu nyengine!.
Maana kagame hajaanza leo kusontewa vidole kuhusu hili!.
Kama wanataka kulimaliza hili wakadili na vigogo.
 
Nadhani Kagame anawapa ufadhili wa silaha na wanajeshi ili kumsaidia Mtutsi mwenzake anayebaguliwa Congo.

Pia Nadhani, anawapa msaada waasi kwasababu Congo iliwaunga mkono waasi wa kihutu. Unaiunga mkono FDLR basi Nami nitawaunga mkono M23.

Sasa kama Kama ni kweli Rwanda inahusika
1. Kwanini hatuoni vijana wa kikongoko wakiipigania nchi Yao kwa kufa na kupona? Morale ya vita sio silaha au miundombinu bora bali cha kwanza ni ule munkari wa watu kujitolea kufa na kupona....kwanini Wacongo hawana hili???

2. Au ambayo yamekuwa yanalalamikiwa na M23 ndiyo yanayopitiwa na Wacongo wote?

3. Kwanini Kabila yupo kimya? Anamkono gani kwenye hili. Kumbuka makubaliano yake na Hawa waasi March 2009.

4. Je, Nangaa ni mtutsi?
Hakuna hisia mbaya kama za kukataliwa na nchi yako. MTUTSI ambaye vizazi na vizazi vimezaliwa Congo Kisha serikali inamwambia sio Mcongomani kisa tu anazungumza Kinyarwanda.

Mfano mdogo: Mimi Mama mzaa bibi yangu ni Msomali. Simfahamu hata.

Kwa muonekano ukiniona tu japo hadi uwe mdadisi utagundua ninavinasaba vya Kisomali. Lakini mimi sio msomali na hata sipajui.

Mara nyingi nikikutana na wale wabongo wajuaji wananiambia wewe sio mtanzania. Huwa najiskia Vibaya saana kila sehemu ya mwili wangu husisimka. Sasa huyo ni mtu baki....fikiria serikali iniambie hivyo...unafikiri nini kitafuata???
Na mimi nauliza. M23 wapo tayari kwa mazungumzo. Je, kwa nini serikali haitaki mazungumzo na M23?

Wanasema if you can't fight them, join them! Je, kuna madhara gani kwa serikali ya DRC kuingia makubaliano ya amani na M23 halafu yatengenezwe mazingira ya kuwa raia wa DRC lakini waishi sehemu tofauti tofauti ndani ya DRC halafu mipaka hiyo ilindwe na jeshi la taifa huku hao M23 wakijumuishwa katika jeshi la taifa pia?
 
Kagame ameingia mkataba na European Union kuwauzia madini, jiulize hao wazungu wanafikiri madini yanatoka wapi, yanapatikanaje? Kuna wengi nyuma ya Kagame mbali na US, naona wakubwa wamesha amua Kongo mashariki aichukue Kagame.
 
Na mimi nauliza. M23 wapo tayari kwa mazungumzo. Je, kwa nini serikali haitaki mazungumzo na M23?

Wanasema if you can't fight them, join them! Je, kuna madhara gani kwa serikali ya DRC kuingia makubaliano ya amani na M23 halafu yatengenezwe mazingira ya kuwa raia wa DRC lakini waishi sehemu tofauti tofauti ndani ya DRC halafu mipaka hiyo ilindwe na jeshi la taifa huku hao M23 wakijumuishwa katika jeshi la taifa pia?
Nadhani ni ego tu ya Rais.

Kwenye kampeni zake aliahidi kuwashughulikia na kutokuridhiana nao....hii ni sababu ya kisiasa.

Ila binafsi nadhani kwasababu Rwanda alikataa kukaa pamoja na waasi wa kihutu na waliungwa mkono na DRC vivyo hivyo Serikali ya Congo haitaki kukaa pamoja na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda.
 
Silaha zitakuwa zinapita Rwanda na Uganda, inawezekana pia Rwanda ikawa inawasaidia waasi kwa maslahi yake lakini sio kwamba waasi wakikosa silaha huko Rwanda watashindwa kupigana kabisa. Kama hivi wanajeshi wa Congo walivyokimbia watakuwa wameacha silaha nyingi tu nyuma kwenye makambi. Waasi wana njia nyingi za kujipatia silaha kwa sababu biashara ya silaha za magendo duniani ni kubwa sana pia.
Munkari mdogo unasababishwa na nini?
 
Inahitaji intelligence kuchimbua hili maana hapa kuna swala la mali pia!, inaweza kuwa uwepo wa mali ktk hilo eneo ikawa ndio sababu zaidi ya hao watutsi kupataka huku wakisema sababu nyengine!.
Maana kagame hajaanza leo kusontewa vidole kuhusu hili!.
Kama wanataka kulimaliza hili wakadili na vigogo.
Ilitokea miaka ya nyuma Loliondo....wamasai wa Tanzania waliambiwa ni wakenya.

Lakini pia hao hao wamasai wa Tanzania walipopigana na makabila jirani walipata msaada kutoka serikali ya county ya kenya iliyoogozwa na mmasai .......you see the tricky part of this game!
 
Nadhani ni ego tu ya Rais.

Kwenye kampeni zake aliahidi kuwashughulikia na kutokuridhiana nao....hii ni sababu ya kisiasa.

Ila binafsi nadhani kwasababu Rwanda alikataa kukaa pamoja na waasi wa kihutu na waliungwa mkono na DRC vivyo hivyo Serikali ya Congo haitaki kukaa pamoja na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda.
Sijajua ipoje huko lakini navyoona, kuna kila sababu M23 wakajumuishwa kwenye jeshi la taifa na hiyo sehemu ya Goma ikawa chini ya jeshi la taifa.

Kama ni kweli hao Watusi wa DRC waliishi hapo miaka mingi kutokea Rwanda, ni ngumu Kagame kukubali warudishwe Rwanda kwa sababu ardhi Rwanda haitoshi.

Turejee historia, baada ya bara la Afrika kugawanywa, kuna jamii za mipakani zilijikuta zipo nchi mbili tofauti mfano Wamakonde wa Msumbiji na Tanzania.

Serikali ikubali kuzungumza na M23 wawekeane mikakati ya kudhibiti Watusi wapya kuingia mashariki wabaki wale wa zamani tu! Lakini kuwakataa itakuwa ngumu mana Kagame anasema hao Watusi nyumbani kwao ni huko DRC mashariki na siyo Rwanda
 
Kwanini Rwanda 🇷🇼? na sio Burundi 🇧🇮?
Jamii gani inaishi mipaka ya Burundi na DRC.....?

Kumbuka hata Uganda nayo alikuwa na mgogoro na ADF mpakani na DRC.
 
Back
Top Bottom