Zinapitia wapi?
Kagame hajawahi kujibu swali la kutowasaidia waasi moja kwa moja....! Uso humbadilika.
Mi si mwanasiasa, lakini nakujibu kwa mfano hai: Russia wakati inaanza vita na Ukraine, kila mtu aliamini haitakaa hata wiki kabla Russia haijaiponda Ukraine. Mpaka leo hii, ni vuta nikuvute. Lakini, hatimae, ukweli ulijulikana, na hakika Russia inapigana na USA, na EU. Russia ingekuwa ya kawaida, tayari.
Sasa kwa hili, kabla ya kujiuliza swali hilo, anzia kwenye historia ya miaka ya 1885. Miaka zaidi ya 200 ni kipindi kirefu sana. Kumbuka watu wanafarijiana, wanaoana na kuzaliana. Hivyo unajikuta mtu sehemu moja ameshapata ukoo sehemu nyingine. Jiulize, wanauliwa wakwe labda mkoa x. Utakaa kimya!?
Mimi(ni kwa uelewa wangu si kwa uhalisia wa kidiplomasia au kisiasa):
-uwezekano wa kuungwa mkono upo. Ila tatizo la huu mgogoro ambalo baso linawachanganya vichwa watu, ni kwamba wanyarwanda wa Congo na wa Rwanda, asilimia kubwa yao, ni lugha moja. Hivyo, kumtambua mtu wa M23 umtofautishe na wa Rwanda, ni jambo lisilowezekana. Ndio maana, wanaosema yawepo mazungumzo ya amani, ndo naona wana tija.
- wanyarwanda wa Congo(kumbuka ni mchanganyiko wa wahutu na watutsi). Baada ya migogoro hiyo, wengi wao waliweza kupata visa permanent nchi za nje. Diaspora yao, hakika inafadhili pakubwa. Tofauti yao na watu wengine, hawa watu wana upendo wa dhati kati yao. Hivyo kuumia alipo lakini asaidia kutafutia wenzake amani, lazima.
-Kama ilivyo kwa makundi mengine, haiwezekani M23 isimiliki machimbo. Tunalishwa tu matango, lakini kwenye biashara, tutadanganyana. Hakunaga uadui. Pesa ipo, wanaokufa watajua wenyewe, we nipe mzigo na mi nikupe pesa.
-Viwanda vingi, vilipiga marufuku kununua madini ya ukanda wa mashariki mwa DRC kutokana na mzozo huo. Majuzi serikali ya DRC, iliishitaki apple. Je, unadhani watu watafunga viwanda vyao kisa vita!? Haiwezekani. Na siraha mkitaka mtapata, kikubwa yeye apate mzigo, aendeshe viwanda vyake.
-Watutsi na Wahutu, kiuhalisia si makabila kama ilivyo kwa jamii nyingine duniani ukiondoa tu Rwanda na Burundi. Hivyo, watu wa Congo huko, baada ya wanajeshi wa serikali iliyoondolewa mwaka 1994, na waliouwa watutsi, walimuinda kila anaeitwa mtutsi ili auwawe nae. Kumbuka, haya makabila mara nyingi hutambulika tu kimaumbile. Hivyo, kuna wengine walipoteza maisha pasi na kuwa watutsi hao.
- ni nadra sana kwa mwanajeshi kuamini kama kweli ameshindwa. Atakufa na mipango akilini ya kurudi alikokuwa. Baada ya miaka yote hiyo, waliohusika na mauaji au na wanajeshi hao, hawapo tena. Watoto waliozaliwa mapolini huko, leo hii ndo wapiganaji. Walishaambiwa characteristics za mtutsi. Wanajua akikuwahi anakuua. Kwa hiyo wao ndo huhakikisha wanamuua.
Hawa watu(wahutu au FDLR), wao wana siraha. Kuua na kupora mifugo ni kugusa.
-Hii jamii, kabla ya miaka ya 1994, ilikuwa sawa na jamii nyingine nchini, hivyo jeshini walipokelewa. Ambao kwa sasa, wengi wao wana vyeo vya juu jeshini. Wengi wao waliamua kujitenga na serikali, na kuanzisha makundi yao ya kujihami. Baada ya kuamua kujiunga na kuwa M23, ni kundi lenye uzoefu wa kijeshi. DRC hasa mashariki, ni mapoli. Hivyo mafunzo ni rahisi kupata. Kupata warimu wa kijeshi kimataifa, halikuwa jambo gumu, kikubwa pesa wanapata. Hapa jambo la kujiuliza tu litakuwa siraha zinawafikiaje. Lakini mwanajeshi ni mwanajeshi na ana mbinu zake.
Kupeleka watu kujifunza, ni kazi ndogo.
-Leo hii ukiangalia arsenal ya siraha walizopola serikali, huwezi amini. Na kila aina ya siraha, kuna watu wanajua kuzitumia. Hii ina maana zilizotoka china, hakika kuna watu walijifunza huko au wengine waliletewa wataalam wa kuwafundisha. Russia hivo hivo, na mataifa mengine yanayotengeneza silaha.
Kwa hiyo, wakikamata silaha 10, wakasema zimepatikana 1000, utakubali. Nani ataenda kuhakikisha!? Na kumbuka, vitani kila silaha uliyoweza kupola, ni mali yako.
Je, mfano, SADC na wengine nani aliekubali kuwa vitani na M23!!! Lakini mwishoe wote wameumbuka.
Kwa kuhitimisha, vita bya Congo viangaliwe kwa masirahi ya mataifa makubwa pia. Kama yanapata chochote, kuuwana kwa watu si shida kwa wanaojitaji mali. Isimgelikuwa hivyo, huu mzozo usingekuwepo.