Sijajua ipoje huko lakini navyoona, kuna kila sababu M23 wakajumuishwa kwenye jeshi la taifa na hiyo sehemu ya Goma ikawa chini ya jeshi la taifa.
Kama ni kweli hao Watusi wa DRC waliishi hapo miaka mingi kutokea Rwanda, ni ngumu Kagame kukubali warudishwe Rwanda kwa sababu ardhi Rwanda haitoshi.
Turejee historia, baada ya bara la Afrika kugawanywa, kuna jamii za mipakani zilijikuta zipo nchi mbili tofauti mfano Wamakonde wa Msumbiji na Tanzania.
Serikali ikubali kuzungumza na M23 wawekeane mikakati ya kudhibiti Watusi wapya kuingia mashariki wabaki wale wa zamani tu! Lakini kuwakataa itakuwa ngumu mana Kagame anasema hao Watusi nyumbani kwao ni huko DRC mashariki na siyo Rwanda