Maswali ya msingi kwenu Wana Jukwaa

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Nilikuwa na maswali yangu machache ya msingi kuhusu nchi yangu Tanganyika.

1. Wakati yanafanyika makabidhiano ya uhuru kutoka kwa Muingereza kuja kwetu kwa Watanganyika ni masharti gani Muingereza alitoa kwetu Watanganyika kuhusu uhuru alio tukabidhi December 9, 1961?

2. Mali ngapi bado zipo chini ya Muingereza ( zinamilikiwa na Muingereza moja kwa moja ) hapa Tanganyika licha ya kuwa alitupa uhuru?

3. Ni makubaliano gani waliingia Muingereza na Nyerere kuhusu uhuru wetu?

* Maswali ya nyongeza yatakuwepo tuanze kwanza na hayo matatu ya mwanzo.

N.b
Nipende kusisitiza nahitaji watu smart kujibu maswali haya, sihitaji mizaha isiyo na maana kwenye uzi huu tufahamu hili mapema.

Kama huwezi kujibu kuwa msomaji ili kuepusha shari.

Majibu bora ya haya maswali ni elimu tosha kwetu sote kuhusu nchi yetu.
 
Subiri kidogo

Tanganyika lilikuwa ni Koloni la Ujerumani na Waingereza walipewa usimamizi Wakati tukiandaliwa kujitawala

Inasemekana Wajerumani ndio Wana Baadhi ya Madini yao huko kwenye Makanisa yaliyojengwa maporini

Ikumbukwe pia Mjerumani Karl Peters alikabidhiwa Tanganyika na Sultan wa Oman aliyeishi Zanzibar

Sasa labda wajuzi watufahamishe mkataba wa Karl Peters na Sultan wa Oman ulikuwaje

Maana baadae Karl Peters alitia Mikataba na machifu wakiwemo akina Mangungo wa Msovero Kabla ya kupokea kipigo Kutoka kwa Chifu Mkwawa wa Lugalo, Kalenga mkoani Iringa

Ahsante sana!
 
Masharti hapo kwenye mkataba wa roma. Kipengele cha mafungamano ya siasa na dini (madhehebu ya dini) hasa ukristo na uislam.

Ukristo umepewa nguvu kubwa kuliko uislam, uislam udhibitiwe , umepewa mipaka ktk kupanuka kwake, na udhibiti wake unafanywa kwa njia ya mifumo, hasa kwenye elimu na utawala.

Kwenye elimu..shule na vyuo vyote vya kiislam binaminywa kwenye ufauru.hata wakifanya vizuri vipi lakini shule/vyuo hivyo vitapewa GPA za chini.
Na ndio mana sasa tunaona hata wasomi wakubwa wachache ukiwachunguza wamesoma shule za wakatoriki.

Kwenye utawala nako tunaona, anapokuja Rais mwislam lazima anatakiwa kua na mlengo wa kushoto.lazima awe mpole, watu waluhusiwe kuongea nk. Lakini Rais akitokea kwenye ukristo ana uhuru wa kufanya chochote na hakuna wa kumzuia. Hivyo Rais mkristo yeye atakua wa mrengo wa kulia.nchi kwanza.kwa ufupi ukiisema vibaya nchi kitachokukuta usishangae na hakuna wa kukutetea.

Makubaliano: mwingereza ataendelea kua mlezi wa nchi kwa wakati ote, kwa lolote litakalotokea kwenye nchi iwe vita iwe majanga makubwa iwe uvamizi dhidi ya yeyote mwenye lengo baya na nchi na watakua washauli wa kuu kwa yeyote mkubwa anaetamani kushirikia na nchi, kama watakua na mashaka na mshirika huyo basi wanaweza kukushauri usishirikiane na mtu huyo, na wana njia zao za kukudhibiti..MFANO:- waraka ule.

Vitu ambavyo bado vipo chini yako katika uwekezaji, naamini muhimbili , wazo cement, hata hii bandali. Mpaka leo kwenye miladi hii kuna pasent inaenda..na ukitaka kuleta ushindani kwenye miladi hii wana njia za kukuthibiti MFANO: Kwenye cement tumeona dangote kavurugwa wee mwisho wa siku cement imekua bei moja na ya wazo. Nk, nk, nk, .

NB. JOKA JEKUNDU LILILOTAJWA NA UFUNUO NI UINGEREZA.
 
Asante na kwa kumgusia mjerumani
 
Tusubiri wataalamu waje kujazia nyama zaidi kuhusu huyo Mjerumani na Muingereza hasa hasa Muingereza kutokana na maswali yanavyo uliza
 
Asante kwa majibu yako.

Ningependa unifafanulie kila swali na jibu lake lililo shiba ushahidi wa kutosha.

Sote tupo kujenga karibu
 
Badala ya kujibu maswali yako kidogo kidogo nimeona niulete hapa mswada uliosomwa na bunge la Uingereza unaohusiana na uliopitishwa ili Tanganyika ipewe uhuru wake:

Tafsiri kwa msaada wa Google:

HANSARD 1803–2005miaka ya 1960 1961 Novemba 1961 8 Novemba 1961 Commons Sitting

MSWADA WA UHURU WA TANGANYIKA​

HC Deb 08 Novemba 1961 vol 648 cc986-1041986
§Agizo la Kusoma Mara ya Pili.
§3.43 usiku
§3.57 usiku
§4.12 jioni
§4.19 jioni
§4.28 jioni
§4.40 jioni
§4.46 jioni
§4.56 jioni
§5.10 jioni
§5.22 jioni
§5.33 jioni
§5.40 jioni
§5.50 jioni
§5.57 jioni
§6.7 mchana
§6.17 mchana
§Swali liliwekwa na kukubaliwa.
§Mswada ipasavyo usome mara ya Pili.
§Mswada uliokabidhiwa kwa Kamati ya Bunge zima—[Bw. JEB Hill. ]
§Kamati Kesho.
  1. c1041
  2. UHURU WA TANGANYIKA [PESA] 166 maneno
Rudi kwenye ORDERS OF THE DAY
Sambaza UHURU WA TANGANYIKA [PESA]
Umeona hitilafu? | Ripoti masuala mengine | © Bunge la Uingereza
 
Ukiona watoto wanaanza kuuliza zilipo hati na vyeti vya NDOA vya wazazi, stuka!!

Muungano wetu ni tunu tuliorithishwa na waasisi wetu.

Muungano utalindwa Kwa gharama yoyote.

Hautavunjwa, utaboreshwa tu.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
 
Vya kushangaza. Kwenye mswada huu, kinyume na tunavyoaminishwa kwenye siasa zetu za propaganda za kujazana ujinga.

Mswada upo wazi kabisa na unausifu mshikamano wa Tanganyika na umoja wa kitaifa waliokuwa nao.

Waingereza humu wanashangaa kuwa hawajakuta chuki (naamini za kikabila na kidini) "ama za kwengine" nje ya Tanganyika.

Kwa hiyo tusidanganyanekuwa "legacy" hiyo ililetwa baada ya uhuru.
 
Fungulia uzi wake tuje tukupe dqrsa la Mjerumani na Sultani.

Tusiuharibu huu uzi wa watu kwa kuchanganya mada.
 
Ukiona watoto wanaanza kuuliza zilipo hati na vyeti vya NDOA vya wazazi, stuka!!

Muungano wetu ni tunu tuliorithishwa na waasisi wetu.

Muungano utalindwa Kwa gharama yoyote.

Hautavunjwa, utaboreshwa tu.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
Kumbuka tu mtoa mada ameuliza masuala kuhusu Tanganyika
 
Asante sana wacha niipitie yote kwanza nitarudi kama kutakuwa na maswali ya nyongeza
 
Ukiona watoto wanaanza kuuliza zilipo hati na vyeti vya NDOA vya wazazi, stuka!!

Muungano wetu ni tunu tuliorithishwa na waasisi wetu.

Muungano utalindwa Kwa gharama yoyote.

Hautavunjwa, utaboreshwa tu.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
Tujikite kwenye uzi hakuna mahali muungano umehusika hapa, zingatia niliyo sisitiza.
 
Asante. Nitarudi kwa mengi zaidi
 
Hakuna pahala mtoa mada ameuliza maswala ya muungano, na ukae ukijua muungano sio Biblia Wala sio Quran kwamba hawezi kuvunjwa, jikite kwenye mada
 
Hayo maswali yako matatu yote mwenye majibu sahihi ni Nyerere, wengine hapa ni kuleta story walizookota kila mmoja kwenye kijiwe chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…