Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Nawaona CCM na vibaraka wao wanapiga kelele sana kudai No Reform No Election haitafanikiwa kwa sababu vyovyote vile hakuna Watanzania watakaoweza kuwaunga mkono CHADEMA.
Kelele hizi zinapigwa ili kwanza kuwakebehi Chadema na kuendeleza Propaganda za kuwarubuni Watanzania ili waendelee kuwa watumwa wa upuuzi na udhalimu wa CCM.
Pia kelele hizi zinapigwa kwa nia ya kuwakatisha tamaa wapenda mabadiliko ili waone kuwa hakuna namna yeyote kwenye Taifa letu, madai ya haki yatakuja kufanikiwa.
Napenda kuwakumbusha wana CCM na vibaraka wao kuwa, kwenye kufanikisha agenda ya No REFORM NO ELECTION, Chadema watazungumza na makundi mbalimbali ikiwemo Viongozi wa Dini.
Maswali yangu kwa CCM na watu wao!
1. Endapo leo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) wakasema wanaunga mkono NO REFORM NO ELECTION na watashiriki maandamano ya amani kupinga kufanyika kwa uchaguzi. Je kuna Polisi au mwanajeshi yeyote nchi hii anaweza jaribu kufyatua bomu au risasi dhidi ya waandamanaji wanaoongozwa na maaskofu na Mapadre?
2. Endapo leo Viongozi wa dini ya kiislamu wakasema wanaunga mkono NO REFORM NO ELECTION na watashiriki maandamano ya kudai mabadiliko ya Katiba kabla ya Uchaguzi. Je kuna Polisi au Mwanajeshi atajaribu kuwapiga bosi au kuwafyatulia risasi hao waandamanaji?
3. Endapo leo baadhi ya Maaskofu wa Madhehebu mbalimbali ikiwemo KKKT na CCT na hata Wasabato wakisema wanaunga mkono NO REFORM NO ELECTION na wakaamua kushiriki maandamano ya kupinga uchaguzi bila mabadiliko ya katiba CCM wanadhani kuwa mwanajeshi au askari atajaribu kuwapiga risasi au bomu au maaskofu?
Soma Pia: Tundu Lissu na John Heche watangaza kuipeleka ajenda yao ya "No Reform No Election" nje ya nchi
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Nipende tu kuwaambia CCM na vibaraka wao. Ni heri mkae kimya maana Watanzania sio Wajinga.
Kuna maandamano yakifanyika hapa nchini na yakahusisha watu fulani ( Hasa Viongozi wa Dini) hao polisi mnaowategemea na Wanajeshi hawataweza kuzuia hayo maandamano kamwe.
Msiwakebehi CHADEMA maana hamjui nani atawaunga mkono kesho na kutakuwa na matokeo gani baada ya huo uungwaji mkono.
Kuweni na akiba ya maneno. Watanzania sio wajinga na kila siku wanazidi kuchoka kuwa mazezeta kwa Wanasiasa.