Maswali yenye Utata Kifo cha Balozi C. Mushi. Nini kipo nyuma yake?

Maswali yenye Utata Kifo cha Balozi C. Mushi. Nini kipo nyuma yake?

sasa utata unatokea wapi hapo?
hizo ni stress tu.

lakini pia jambo muhimu la kujifunza ni kwa wateule wa nfasi za juu lazima wawe na maadili yasiyotiliwa shaka.
ukosefu wa maadili ni tatuzi kubwa sana kwa viongozi wetu, VITENDO VYA RUSHWA NA NGONO, NGONO, NGONO maofisini ni tatizo sana sana, Ngono ngono
Ha ha ha
 
Yap nakumbuka jamaa alikuwa katibu/msaidizi wa waziri mkuu lowasa.
Jamaa mtu wa totozi sana alikuwa anamkula hoisi temu akamuunganisha kazi UN zen akamconect kwenye ubalozi.
Jamaa alikuwa muhunimuhuni flani
Marehemu alikuwa anakojolea pazuri.
R.I.P
 
Huyu jamaa taarifa nilizonazo ni kweli kuwa alirudishwa home kwa kuwa pale Swiss alituhumiwa kubaka.Na kwa mujibu wa watu wa karibu na marehemu aliyemtuhumu marehemu kwamba alitaka kubakwa ni mwanamke ambaye walikuwa nae katika mahusiano.Ingawa taarifa hiyo haikuweka wazi kuwa mwanamke huyo alikuwa wa Uswis au nchi nyingine.Taarifa zinasema kuwa ,mtu huyo alifikisha taarifa kwa mamlaka za nchi hiyo ya bara la Ulaya kuhusu kutaka kubakwa na marehemu balozi.Aidha taarifa zinasema kuwa ,inawezekana' kabisa kuwa marehemu Balozi alikuwa katika mahusiano na mtu huyo lakin baada ya mahusiano kuvunjika na vurugu za hapa na pale ndio mwanamke huyo alipofikisha taarifa za kubakwa kwa mamlaka za huko Ulaya.Taarifa hizo zinadai kuwa mwanamke huyo alikuwa na ushahid wa picha na video za vitendo hivyo vya balozi.Aidha imedaiwa kuwa mwanamke huyo alifanya kitendo hicho baada ya kuona mawasiliano ya balozi na mke wake .Ingawa balozi alimdanganya kwanza kuwa hana mke.Kwa mujibu wa taarifa hizo ,mke wa balozi ambaye pia anaishi Ulaya ni mtanzania ,mwanasheria na ni mfanyakaz wa shirika la umoja wa mataifa.Kwa upande mwingine kifo cha balozi kimeleta simanzi na huzuni kwa kuwa amekufa kwa utata.
Kwamba mapenzi yana run dunia?
 
Yale yale ya Imran Kombe,

Huyu balozi kama kweli alikuwa na kesi ya ubakaji huko ughaibuni ndio maana akakimbilia nyumbani,aliisha kuwa "compromised"sasa inawezekana waliotaka ku "mrecruit"waliona Bora wamuondoe,au Kuna Siri alivujisha,Idara ikaona huyu hafai Tena,Bora atulizwe milele.

Kwa idara yetu,ambayo ipo bize kuiba kura,na kuilinda ccm,nchi haipo salama,Nina hakika,wanadiplimasia wetu wengi,wapo compromised sana,wanavujisha Siri za nchi,kwa kujua ama kutokujua!!

Sasa sijuhi ni kwa kiwango gani,nchi yetu na systems zipo penetrated.
Kwahiyo idara ya usalama wa taifa ni idara ya usalama wa cccm
 
KUTOKA KWA MALISA GJ

Nimejiuliza maswali kadhaa nikakosa majibu;

1. Balozi Mushi alikua anajiendesha mwenyewe? Tena usiku wa manane? Protocal za kidiplomasia zinasemaje, Balozi anapokua na safari binafsi? Je alikua peke yake?

2. Kama ajali ni uso kwa uso means lori lilikua linatoka ielekeo wa Segera na Balozi alikua anaenda uelekeo wa lori lilipotoka. Kama ndivyo hayo makaa ya mawe yalitoka wapi? Tanga, Kilimanjaro, Arusha hata nchi jirani ya Kenya hakuna makaa ya mawe. Makaa ya mawe yapo Mbeya, Rukwa na sehemu za Njombe. Kenya wanatumia makaa ya mawe kuendesha mitambo yao ya viwanda, lakini wanayachukua Mbeya (Kiwira). Hakuna lori linalotoka na makaa ya mawe Kenya kuja Tanzania, bali malori yanayotoka na makaa ya mawe Tanzania kwenda Kenya. Kwahiyo kama Lori lilikua limebeba makaa ya mawe it means lilikua linaenda uelekeo mmoja na Balozi Mushi. Sasa ilikuwaje wagongane uso kwa uso?

3. Gari iliteketea na Balozi Mushi aliungua kiasi cha kutotambulika. Ndugu walimtambua kwa nguo zake. Je hizo nguo zilipatikana sehemu gani ya gari? Ni moto gani unaweza kuchoma gari ikateketea, lakini nguo zikabaki?

4. Inadaiwa mashuhuda walijua ni Balozi Mushi baada ya kuingiza namba za gari kwenye mifumo ya TRA ndipo ikaonesha mmiliki ni Celestine Mushi. Hizo namba walizionaje kama gari iliteketea?

5. Kwanini usiku huo wa ajali kuna ujumbe ulizunguka sana kwenye mitandao ya kijamii, ukisema aliyepata ajali ni mwanamke lakini gari ni ya Balozi Mushi? Nani aliandika ujumbe huo? Lengo lake lilikua nini? Kuiandaa kisaikolojia familia ya Mushi au?

6. Ajali imetokea Mkata, Handeni Vijijini. Wakazi wake wamepata wapi "exposure" ya kuingiza namba kwenye system za TRA ili kumjua mmiliki wa gari? Je huwa wanafanya hivyo kwenye ajali zote au ni hii tu?

7. Kwanini mamlaka za serikali zilikimbilia kutoa pole kabla ya mwili haujafanyiwa uchunguzi. Je ingebainika kuwa sio Balozi Mushi bali alimwazima mtu gari yake, serikali ingefanyaje na ilishatoa salamu za rambirambi?

Anyway; Mungu ampumzishe kwa amani Mhe.Balozi Celestine Mushi. Laa ko oforo mangi.!
Nchi ni ngumu hii kuielewa
 
Back
Top Bottom