kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mechi kati Simba vs US Gendamarie itachezwa saa 4 usiku siku ya jumapili kuamkia jumatatu siku ya kazi.
Hii ni mara yetu ya kwanza kuwa na kitu kama hiki nchini kwetu. Inafahamika kuwa Uwanja wa Mkapa uko pembeni mwa jiji hasa kwa watu wanaotoka Ilala, Kinondoni, Ubungo, Kawe, Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe, Mlandizi na sehemu nyingine nchini.
Inafahamika kuwa maeneo yale ya Keko, Tandika, Mbagala na vitongoji vinavyouzunguuka uwaja kuna vibaka wengi hata siku za kawaida tu mchana sembuse usiku wa saa 6? Hawa ni watu ambao wanapora, wanachomoa mifukoni, ndani ya magari na hata vifaa vya magari kama taa, power window, rims, redio, nk.
Inafahamika pia usafiri wa umma kwenye routes zote ndani ya jiji na vitongoji vyake haufiki saa 6 usiku, na hata kama utalazimisha ufike saa 6 usiku basi utahangaika na madereva waliochoka sana wenye usingizi, au sivyo madaladala yataendeshwa na madei waka na kusababisha ajali.
Hivyo uhakikisho wa usalama wa watanzania watakaokwenda kutizama mechi saa 4 usiku na kutoka saa 7 usiku ni vizuri utolewe na serikali kupitia waziri wa michezo, mambo ya ndani, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya Temeke, IGP, RPC na kiongozi wa umoja wa madaladala Dar badala ya kuachiwa Simba kupitia msemaji wao Ahmed Ally kusema ooooh usalama utakuwepo, oooo usafiri mpaka kibaha utakuwepo, oooo msiwe na hofu, oooo hivi oo vile.
Ni vizuri watu wakashauriwa wale ambao hawana usafiri binafsi wakachanga kukodi magari kwa bei ya makubaliano ili wawe na uhakika wa kuja na kuondoka na usafiri wao bila kulazimika kugombania magari ambayo obvious yatakuwa machache sana, baadhi ya maeneo hayatakuwa na usafiri kabisa. Na vibaka wanapendelea sana watu wanapokuwa kwenye msongamano wa kugombea kuingia uwanjani au kwenye magari. Badala ya Ahmed kuwaaminisha yeye watu kuwa usalama na usafiri utakuwa wa kutosha ni heri tu kuwaambia ukweli watu waangalie mechi kwenye luninga zao nyumbani na vibanda umiza.