Matajili Azam nawakumbusha Ibenge yupo tu. Au Asec wana kocha mzuri sana hawana hela

Halafu Dabo alivyokuwa anajitetea kwa kupokezwa kipigo jana, hakuwa tofauti na kocha Mubiru aliyepigwa mtama kwa kuishusha mchangani mbeya city
 
Pamoja na ubora wa Yanga lakini Azam mbovu ya jana haijawahi kutokea. Hivi kwa kipa yule kwenye michuano ya Afrika si watapigwa kumi. Kama Yanga jana wangetulia Azam angekula 5 bila. Mlio karibu na mmiliki wa Azam mwambieni ukweli amtimue kocha haraka sana timu ampe hata Mwambusi au Julio vinginevyo hii inaenda kuwa aibu ya Tanzania
 
Kwani waliofungwa FA na Azam miezi miwili iliyopita ilikuwa timu gani
Wanalazimisha azam mbovu ili tu kuprove wrong ubora wa Yanga,hata Yanga ilipofika final caf conf walidai alikutana na timu dhaifu,ile dharau tuliyoingia nayo kwenye ligi wakatufunga jumapili ijayo aitokuwepo,na tuliwataka sana fa ili tuwaonyeshe ubora wetu wakafungwa nusu fainali na azam kule mtwara,Inshallah jumapili sio mbali tunawasubiri makolo tuzibe kidomo chenu
 
Hivi kwa mfano wakakandwa na singida, alafu wakakutana na azam kutafuta mshindi wa tatu na azam nae akapiga kwenye mshono, hayo maneno ya azam mbovu yatasikika teena?

Ukiacha makosa ya goli kipa na baadhi ya wachezaji kukamia sana mechi, azam hawakua na mpira mbaya sana hasa kipindi cha kwanza
 
Na ww pia tunaomba tukukumbushe azam fc ni yake n sio ya WANACHAMA. Unawashwa nn?
Asante
 
Mbona pre season walimfunga ibenge na Al halal yake 3-0 na wakamfunga us monastir ya Tunisia 2-0?
Wakati mungine kocha anafundisha Kama wachezaji hawashiki na kuamua kucheza kung fu Nani alaumiwe 🤷🏿‍♂️
 
Azam hiyohiyo unayoichukulia poa ndo ilikubamiza FA na kukusumbua kwenye ligi. Azam amekutana na timu kubwa.
Na hiyo timu kubwa ndio imetoka kupigwa 2-0 na mnyama kwenye ligi
 
Kikubwa hawataki kukubali kama Yanga ni timu nzuri na ndio maana ni vizuri tukutane nao ili tuwanyooshe na kukata mdomo wao
 
Timu mbovu halafu kila mechi inawafunga tu nyinyi wabovu wenzao.
 
Acha kukariri Kuna kina sisi sio wafia simba&Yanga tunapenda mabadiliko ya soka Tanzania haingii akilini watu 65m tushabikie timu mbili.
Kama umezaliwa 2005 siwezi kukupinga kushabikia Azam,maana wamepanda ligi mwaka 2008 ila kama umezaliwa early 1980's mpaka 1990's utakuwa muongo na mnafiki kwamba wewe ni die hard fan wa Azam......kuna timu yako itakuwepo pale Kkoo
 
Maneno mengi unamaliza miti tu
 
We mke wetu tulia, unataka kipigo tena
 
Timu ikifungwa tu na Yanga basi mbovu, watu mna maneno.
 
Uko sahihi binafsi naona ili ligi iwe Bora lazima kuwe na Timu angalau 5 au 6 zenye ubora wa juu
Ndio mkuu, Angekuja Azam akaja Singida FG,Namungo labda na wengine ili soka letu likue....sio nchi nzima iwe na Timu mbili tu.
 
Kweli kabisa,kocha hamna pale yule Jamaa,sijui huwa wanawaza Nini?
Mbona Azam inaimbwa Ni Tajiri lakini hamna utajiri unao onekana kwenye usajili wa Makocha na wachezaji.....wanenda Afrika magharibi wanaokota okota wanaleta huku watu hawana uzoefu na mashindano ya Afrika ngazi ya vilabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…