Matajiri wakubwa Tanzania si wafanyabiashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Wataje kwa majina,
Mbna unawaogopa
 
Sana. Mawaziri wanapanda mabasi na kuendesha baiskeli, na kuna nafasi za kisiasa hata mshahara hupati
Nafasi gani hio hupati mshahara?
And btw, Scandinavian countries wana utamaduni mzuri sana wa uadilifu, ila % kubwa ya nchi za dunia hii ni utapeli tu, sio USA, sio Uk, German au China, au kenya au Tz
 
Nafasi gani hio hupati mshahara?
And btw, Scandinavian countries wana utamaduni mzuri sana wa uadilifu, ila % kubwa ya nchi za dunia hii ni utapeli tu, sio USA, sio Uk, German au China, au kenya au Tz
China wako vizuri na sababu ni moja tu - ukidokoa hela ya serikali unanyongwa. Hawataki ujinga.

Unajua kwa nini Tanzania hatutakaa tupitishe sheria kwamba mtu akiiba hela ya serikali anyongwe au kufungwa maisha? Itapingwa vibaya na wanasiasa na viongozi kwa sababu karibu kila kiongozi wa Tanzania anaiba hela ya serikali - kuanzia Ikulu hadi mwenyekiti wa mtaa!

Jiulize, kama ni kweli tunauchukia ufisadi, basi tuseme mafisadi wakishikwa wanyongwe - halafu utaona ni nani wanapinga hilo kwa nguvu zote
 
Kuna habari ya mwekezaji wa nje kutakiwa kumpa waziri wa madini dola milioni moja na nusu ili apate eneo la uchimbaji. Sasa ni wangapi watadaiwa hiyo rushwa?
Mikataba isiyoeleweka ya rais na waarabu, haipiti bure! Na kaweka hadharani, kila mmoja ale kwa nafasi yake na kuwaambia ila hawaridhiki!!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Wataje hao wanasiasa wenye hela kumzidi Bakhresa, Mount Meru, Mo au Lake group,

Sometimes tusidanganyane sana, wanasiasa wana hela ila usiseme ndio wenye hela nying nchini, matajiri hii nchi ni wahindi na waarabu
Beberu hujaelewaa mada kabisa. Matajiri wengi ni watu wa serikali achana na awo iliwataja wewe. Sisi tunazungumziaa wengi ni wapigaji viongozi wa serikali ni Matajiri kupitiaa wizi wa pesa za serikali na kujiwekea mifumo ya kujilinda na kuwekaa ndugu zao au watoto
 
Umeeleza vyema sana.

Tanzania matajiri wengi walianzia pale Serikali ilipokuwa inafanya mabadiliko ya sera za kiuchumi kuingia UBINAFSISHAJI. Hiyo ndio ilikuwa Foundation.

Na kingine, hii ni dunia nzima, Matajiri wote wa maana duniani, Political connections ndio zimewabeba aidha kupitia tendering au favors fulani fulani. Ndio maana nchi kama Marekani, Matajiri ndio donors & backers wakubwa kwa wanasiasa kwa sababu kuna favors watarudisha au sera fulani fulani zitalegezwa kwa maslahi yao businessmen.
 
Usisahau kuwa hao kina Aboud & the likes [wahindi na waarabu] mfumo wa kikoloni uliwapa kipaumbele wao kuwa wafanyabiashara. So, business community yao ilikuwa kubwa na powerful kwa muda mrefu, ndio maana hata Ubinafsishaji ulipoanza, ni Waarabu na wahindi ndio waliochukua vipande vikubwa vya keki.

'Ubanifsishaji holela' huo pia hata waswahili walinufaika. Kwetu kule lake zone, SHIRECU & NYANZA CORPORATIVE UNION zimetoa matajiri wa kisukuma miaka ya 1990 hadi 2000. Na waliokuwa timamu, hadi leo wamemantain utajiri huo.
 
Utofauti Mkubwa wa Upendeleo wa Serikali kwa wafanyabiashara kati ya Western World na Afrika ni Manufaa ya Upendeleo huo ni upi. Wenzetu upendeleo anaopewa mfanyabiashara huwa na maslahi ya taifa na sio kumpendelea mmoja dhidi ya wengine kiushindani [Fair Competition]. Mfano, Trump kumpiga ban Huawei na kulinda maslahi ya taifa lake kiusalama na kibiashara, au Magufuli kumpa Shamba la Miwa Bakhresa kwa lengo la kutatua changmoto ya sukari ni maslahi ya taifa. Ila sehemu kubwa huku kwetu huwa ni maslahi ya afisa wa serikali.

Wenzetu walipita hatua hii tulipo sasa hivi sisi ya viongozi kutoa upendeleo kwa maslahi yao binafsi, wakaweka sheria kali zinazozuia Viongozi kunufaika binafsi na Tendering, ndio maana wao Serikali ikitoa tender au upendeleo kwa mfanyabiashara ikaja bainika alikuwa mnufaika binafsi wa maamuzi hayo lazima ashitakiwe. Kinyume na sisi huku ambapo DED anampa mtu tender na 10% ni kawaida. On the same note, nchi za West, kwao kampuni kutoa Hongo ili kupata tender ni kosa, lakini sheria zao ziliwaruhusu kutoa hongo wanapobid tender nchi za nje [and it was accounted kwenye vitabu vya kampuni].
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…