Matajiri wakubwa Tanzania si wafanyabiashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Matajiri wakubwa Tanzania si wafanyabiashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Ties za wafanya biashara na wanasiasa zinajulikana, na zinafanya wafanya biashara wawe matajiri kwa biashara halali. Hapa tunaongelea wanasiasa matajiri kupita kiasi sio kwa kuwa wanafanya biashara, kwa kuvuta hela ya serikali inayotkana na kodi za wananchi, ku-inflate manunuzi, au kufanya miradi hewa nk. Huyo aliyenunua hekalu la bilioni 25 Dubai unafikiri yeye kazipata hizo hela kwa biashara?
Wataje kwa majina,
Mbna unawaogopa
 
Sana. Mawaziri wanapanda mabasi na kuendesha baiskeli, na kuna nafasi za kisiasa hata mshahara hupati
Nafasi gani hio hupati mshahara?
And btw, Scandinavian countries wana utamaduni mzuri sana wa uadilifu, ila % kubwa ya nchi za dunia hii ni utapeli tu, sio USA, sio Uk, German au China, au kenya au Tz
 
Nafasi gani hio hupati mshahara?
And btw, Scandinavian countries wana utamaduni mzuri sana wa uadilifu, ila % kubwa ya nchi za dunia hii ni utapeli tu, sio USA, sio Uk, German au China, au kenya au Tz
China wako vizuri na sababu ni moja tu - ukidokoa hela ya serikali unanyongwa. Hawataki ujinga.

Unajua kwa nini Tanzania hatutakaa tupitishe sheria kwamba mtu akiiba hela ya serikali anyongwe au kufungwa maisha? Itapingwa vibaya na wanasiasa na viongozi kwa sababu karibu kila kiongozi wa Tanzania anaiba hela ya serikali - kuanzia Ikulu hadi mwenyekiti wa mtaa!

Jiulize, kama ni kweli tunauchukia ufisadi, basi tuseme mafisadi wakishikwa wanyongwe - halafu utaona ni nani wanapinga hilo kwa nguvu zote
 
Hili lipo hivyo kwa nchi nyingi za Africa.

Biashara nyingi ni za viongozi, mara kadhaa imefanyika kwa kificho kupitia Wafanyabiashara wengine ambao sio viongozi wa serikali.
Kama kiongozi sio mfanyabiashara wa moja kwa moja basi jua anatumika na wafanyabiashara kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara ikiwemo kukwepa kodi na kuwapa dili za serikali.
Ndio sababu hakuna kiongozi anajali kuhusiana na mfumuko wa bei kwa kuwa hizo ni biashara zao ama wana hisa kwenye hizo kampuni.
Jambo baya ni kuwa kadiri miaka inavyokwenda tunatengeza tabaka la watu wenye nacho na mafukara wa kutupwa.

Viongozi wa serikali wana mikono yao katika biashara za usafirishaji( hapa ni mabasi na malori), sekta ya madini (kumiliki vitalu na kuuza madini), sekta ya nishati ( hapa ni uagizwaji wa petrol, disel na kerosene) na kwenye kumiliki vituo vya mafuta(petrol station).
Kwenye sekta ya Ujenzi huku kazi wanayofanya ni ''lobbying'' ya nani apewe mradi upi, halafu yeye anakula tender ya ku-supply kama sio cement basi ni nondo au kupewa sub-contract ya baadhi ya kazi (haswa umeme, plumbing, fire fighting na ICT).

Huwezi kuona majina yao kwa kuwa hizi kampuni zimesajiliwa kwa majina tofauti na wamefanya hivyo makusudi ili waendelee kupiga hela bila bugudha.
Kuna habari ya mwekezaji wa nje kutakiwa kumpa waziri wa madini dola milioni moja na nusu ili apate eneo la uchimbaji. Sasa ni wangapi watadaiwa hiyo rushwa?
Mikataba isiyoeleweka ya rais na waarabu, haipiti bure! Na kaweka hadharani, kila mmoja ale kwa nafasi yake na kuwaambia ila hawaridhiki!!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Wataje hao wanasiasa wenye hela kumzidi Bakhresa, Mount Meru, Mo au Lake group,

Sometimes tusidanganyane sana, wanasiasa wana hela ila usiseme ndio wenye hela nying nchini, matajiri hii nchi ni wahindi na waarabu
Beberu hujaelewaa mada kabisa. Matajiri wengi ni watu wa serikali achana na awo iliwataja wewe. Sisi tunazungumziaa wengi ni wapigaji viongozi wa serikali ni Matajiri kupitiaa wizi wa pesa za serikali na kujiwekea mifumo ya kujilinda na kuwekaa ndugu zao au watoto
 
Nyie ndio mnaamini Bakhresa aliuza kahawa pale msikitini akaanzisha kiwanda cha kusaga nafaka taratibu hivyo hadi akawa bilionea. Upewe mashine ya kusaga tuone kama utapata hata utajiri wa milioni 50. SAS anawatazama uko.

Au mnakuja kwa mzee Gulam Dewji na mwanae Mo mnasema walipambana, ni sawa walipambana. Ila hata wewe tukikupa vile viwanda vya nguo bure kwenye ubinafsihaji, na ukavitumia kama dhamana kukopea mabilioni nje, na tukakupa mashamba ya mkonge sawa na bure miaka 20 baadae huwezi shindwa kuwa bilionea mkubwa.
Huwezi nipa klabu kubwa kwa hela za "maandishi" billioni 20, alafu nikiulizwa nimeziweka akaunti gani na zimetumikaje nafoka nakulalamika ninavyopata hasara. Baadae ukarudi ukakuta sipo bilionea.

Sasa hayo yote huwezi yapata bila mkono wa kisiasa au kuwa na wanasiasa nyuma. Katafute mmiliki wa Kagera kiwanda cha sukari nani, mmiliki wa Mtibwa nani alafu ujue kwanini sukari Tanzania haitoshelezi kwa uzalishaji ila serikali haitaki kuagiza nje tena kwa bei nafuu.

Nilishtuka baada ya serikali ya Magufuli kukisumbua kiwanda cha Dangote kuhusu either makaa ya mawe au clinker (sikumbuki ni kipi hapo) ghafla Rais mstaafu wa Nigeria, Olisegun Obasanjo akafanya ziara binafsi kwa private jet kuonana na Magufuli. Baada siku chache mambo ya Dangote cement yakatulia. Nikaenda kufuatilia kwanini suala linamhusu Dangote alafu Olisegun ndio aje binafsi wakati ana tiketi ya kidiplomasia anaweza kuja kitaifa.

Kiufupi iko hivi, Dangote alitokea familia ya uwezo ila akaongezea kuwa na political and military connection, Nigeria ilitawaliwa na military rulers. Akafanya awe na haki ya kuagiza mchele na sukari nje na kuuza kwa faida kubwa (sababu kwa kutumia siasa aliua ushindani). Baadae Nigeria ikafanya uchaguzi kutafuta kiongozi wa kiraia iachane na utawala wa kijeshi, Dangote akafadhili uchaguzi mkuu wa Olisegun Obasanjo na akashinda.
Obasanjo akaleta sera ya viwanda kwa kiqsi fulani, ghafla Dangote akaanza kujenga viwanda na ghafla akawa bilionea maradufu. Ukifuatilia biashara za Dangote huwa zinapewa subsidiaries, exclusive rights, mara ndio zinakuwa kipaumbele na sera kuu ya serikali. Kwa sasa ana refinery, ni usanii mtupu unaendelea. Dangote ni GSM wa Obasanjo. Na Marais wa Nigeria huwa wanaachiana na kulindana, mnyororo unaendelea na ukitaka kuingia hapo kati wanufaika wako tiyari muingie vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Biashara za Afrika zina mkono mkubwa wa kisiasa. Hata pale Misri ni hivihivi, Sudan ni hivi, Somalia baada ya kuharibika ile miaka ya 90 waliokuwa wanahamia Nairobi na Dar kujenga mahoteli na kuanzisha biashara kubwa ni wanasiasa wao waliotoroka. South Africa pale hao ndio kabisa wanafanya biashara ikulu.
Biashara ambayo haina innovation nyuma ni vigumu itengeneze utajiri wa haraka. Biashara za kawaida kama unga na simenti inataka uwekezaji mkubwa (sijui hela utapata wapi), sera rafiki kwako mfanyabiashara hiyo (nani ataweka sera za kuku-favour) na ulinzi (dhidi ya sheria, kesi, upinzani, ushindani). Hivyo vyote vinapatikana kwenye siasa za Kiafrika.

Hao wote uwezo mkubwa kibiashara wanao, kisha tag ya kisiasa ndio inakuja.
Umeeleza vyema sana.

Tanzania matajiri wengi walianzia pale Serikali ilipokuwa inafanya mabadiliko ya sera za kiuchumi kuingia UBINAFSISHAJI. Hiyo ndio ilikuwa Foundation.

Na kingine, hii ni dunia nzima, Matajiri wote wa maana duniani, Political connections ndio zimewabeba aidha kupitia tendering au favors fulani fulani. Ndio maana nchi kama Marekani, Matajiri ndio donors & backers wakubwa kwa wanasiasa kwa sababu kuna favors watarudisha au sera fulani fulani zitalegezwa kwa maslahi yao businessmen.
 
Mkuu, utajiri sio kuangalia source,
Kina Abood walimeza viwanda vingap leo iko wapi, baba na babu zetu walikuwa wapi wakati hao wanameza viwanda,

Hayo yote ndio yanayotutofautisha, hakuna utajiri wa bahati, ni kutumia fursa zilizo mbele yetu, wazee wetu nao walikuwepo kipindi hicho cha ubinafsishaji, je walifanya nini?
Usisahau kuwa hao kina Aboud & the likes [wahindi na waarabu] mfumo wa kikoloni uliwapa kipaumbele wao kuwa wafanyabiashara. So, business community yao ilikuwa kubwa na powerful kwa muda mrefu, ndio maana hata Ubinafsishaji ulipoanza, ni Waarabu na wahindi ndio waliochukua vipande vikubwa vya keki.

'Ubanifsishaji holela' huo pia hata waswahili walinufaika. Kwetu kule lake zone, SHIRECU & NYANZA CORPORATIVE UNION zimetoa matajiri wa kisukuma miaka ya 1990 hadi 2000. Na waliokuwa timamu, hadi leo wamemantain utajiri huo.
 
Sijasema dunia ni fair play wala sijasema kudhamini kampeni alikuwa hana hela. Mbona hujajibu kwanini Rais mstaafu Obasanjo alikuja kutatua mgogoro wa kiwanda cha Dangote?

Kwanza unalinganishaje Marekani wakati wadhamini wa Marekani ni kisheria inatambulika na mgombea anataja amepokea kiasi gani kutoka kwa nani. Wakati kwa Dangote na Obasanjo ni makubaliano binafsi sio kisheria.

Nilichosema ni kwamba biashara za Kiafrika zina mkono wa kisiasa, hapa unapinga kisha unasema Bakhresa alipewa ekari alime sukari kisa "ana uwezo". Tena mtu huyohuyo alipewa NMC miaka ya nyuma. Kampuni ya Mayanga Construction kipindi cha Magufuli ilikuwa inapewa tenda za ujenzi za fedha nyingi hadi inaheremewa, napo utasema "ina uwezo". Magufuli kafa na kampuni hatuisikii.

Kikwete alipoondoka kampuni ya Home Shopping Centre ikafunga biashara, wakati enzi za Kikwete ilikuwa inapiga hela sana. Hutaki kuelewa unakomaa wote hao wana uwezo.
Utofauti Mkubwa wa Upendeleo wa Serikali kwa wafanyabiashara kati ya Western World na Afrika ni Manufaa ya Upendeleo huo ni upi. Wenzetu upendeleo anaopewa mfanyabiashara huwa na maslahi ya taifa na sio kumpendelea mmoja dhidi ya wengine kiushindani [Fair Competition]. Mfano, Trump kumpiga ban Huawei na kulinda maslahi ya taifa lake kiusalama na kibiashara, au Magufuli kumpa Shamba la Miwa Bakhresa kwa lengo la kutatua changmoto ya sukari ni maslahi ya taifa. Ila sehemu kubwa huku kwetu huwa ni maslahi ya afisa wa serikali.

Wenzetu walipita hatua hii tulipo sasa hivi sisi ya viongozi kutoa upendeleo kwa maslahi yao binafsi, wakaweka sheria kali zinazozuia Viongozi kunufaika binafsi na Tendering, ndio maana wao Serikali ikitoa tender au upendeleo kwa mfanyabiashara ikaja bainika alikuwa mnufaika binafsi wa maamuzi hayo lazima ashitakiwe. Kinyume na sisi huku ambapo DED anampa mtu tender na 10% ni kawaida. On the same note, nchi za West, kwao kampuni kutoa Hongo ili kupata tender ni kosa, lakini sheria zao ziliwaruhusu kutoa hongo wanapobid tender nchi za nje [and it was accounted kwenye vitabu vya kampuni].
 
Back
Top Bottom