Matajiri wanazidi kuwa matajiri na masikini wanazidi kuwa masikini

Matajiri wanazidi kuwa matajiri na masikini wanazidi kuwa masikini

Tatizo ni masikini kutokujua huo mchezo, akijua tu atapanda kama uyoga. Angalia vijijini, familia inaishi vijumba vya kimasikini, ila mmoja akijua na kufanya yake, umasikini unakufa. Ila michezo mingi ni kuthubutu.
 
tunasubir kuona maparody nayo hakiwa na verification badge ss unashindwa kujua huyu J Makamba Wenyew au sio
Haitakuwa hivyo, utaomba verification kwa utaratibu wa kawaida ila kwa sharti ukipewa unatakiwa ulipie hiyo verification
 
Tatizo ni masikini kutokujua huo mchezo, akijua tu atapanda kama uyoga. Angalia vijijini, familia inaishi vijumba vya kimasikini, ila mmoja akijua na kufanya yake, umasikini unakufa. Ila michezo mingi ni kuthubutu.
Mkuu umedondosha pwoint moja ya maana sana
 
Jina mkuu jamaa washaifunga
Kwamba haifunguki ,mbona mi kwangu inafunguka ? , jina lipo kwenye screenshot
Screenshot_20221103-153905.jpg
 
Walikuwa wanapata faida gani kuwa verification
 
jamani naomba kuuliza hivi mechi ya dunia inaanza tarehe ngapi /
 
Elon Musk tajiri Mpya wa Twitter amesema watu ambao wako Verified huko Twitter watalipia Tsh 19,000 kwa mwezi na sio Tsh 46,000 tena. Wakishindwa kulipa wataondolewa Verification badge ( Blue tick). Pia amesema mtu yoyote yule atakaye kuwa tayari kulipia kiasi hicho naye atakuwa Verified.

Kwa haraka haraka hii ni mbinu ya Elon kurudisha zile pesa zake ambazo ametumia kununulia Mtandao wa Twitter.

Elon Musk alinunua Twitter kwa $44b.

Ikiwa watumiaji watalipa $ 8/m kwa mwaka itakuwa;

Kwa watumiaji milioni 10 $0.96b

Kwa watumiaji milioni 100 $9.6b

Twitter ina watumiaji 397.5m wanaofanya kazi.

Ikiwa watumiaji milioni 200 pekee watalipa, watazalisha $19.2b kila mwaka

Katika miaka 3 - 4 ijayo itatengeneza zaidi ya $60b kila mwaka.

Sasa kupitia mpango wa Elon musk tunatakiwa kujifunza kuwa kuna pesa nyingi sana imejificha kwenye Technology ( Simu & Mitandao yake).
Kabla ya tozo mpya Twitter ilikua ina mapato ya dola billion 5 kwa mwaka 2021 sawa na Trilioni 11.5 za Kitanzania ndani ya kwaka mmoja.
 
Back
Top Bottom