Mimi uzuri wangu nilivyoondoka Tanzania nilijua naondoka kimoja, sikusema naondoka halafu nirudi.
Kurudi labda kuwe na msiba wa karibu sana nimelazimika, au jambo ka dharula kubwa kama hivyo.
Najua nikirudi nitaanza kugombana na watu tangu ubalozini hukuhuku kabla sijagusa Bongo.
Nikifika hapo huo ukiritimba wa airport tu najua nitagombana na watu.
Sasa kuondoa huo ugomvi ndiyo naona bora likizo niende Turks and Caicos tu 😂😂😂
Sirudi Bongo kwa sababu nimeamua.Haurudi bongo sababu mifumo mgogoro ama sababu hauna hela?
Hapa bongo kuna watu wanatembea na escort na wanamiliki helkopta
Endelea kubeba box kaka ujipatie ridhiki yako
Acha kamba mkuu. Tiba ni ghali sana ila kwenye dharula ndani ya dakika 5 wameshafika na utapatiwa msaada wa kitaalamu haraka. Kama ni stroke au heart attack utakimbizwa hospitali huku ukihudumiwa na huko hospitali utakuta kila kitu kiko tayari ni kwenye operesheni moja kwa moja.USA tiba ni bure,ukipiga 911 ndani ya dakika 0 ,5-0 washafika.
Tulidhani diaspora mlioona ulimwengu bora unafanyaje kazi mngerudi kutusaidia kurekebisha hali ya mambo nyumbani, sasa na nyie mnatokomea huko tena!😁
Rudini wakuu mtupe mambinu na mipango mtukwamue kutoka kwenye minyonyoro ya tawala duni.
Baba Marekani ya wapi hiyo ambayo matibabu ni Bure ukipiga 911?Inasikitisha sana Afrika ni SHIT HOLE Continent.
USA tiba ni bure ,ukipiga 911 ndani ya dakika 0 ,5-0 washafika.
SawaSirudi Bongo kwa sababu nimeamua.
Wewe unaona hela kitu muhimu kwa sababu huna.
Kwa watu wenye hela, hela si kitu muhimu sana.
Wewe hujui tofauti ya riziki na ridhiki sina msamiati wa kuongea nawe.
Hebu kwanza umenirudishia memories za watu wa ubalozi hawa. Yaani wanajikutaga ndo wanamiliki nchi kabisa. Dah! 😆😆
Kwa kweli hii ni lugha natakiwa kuwa nayo.Mimi uzuri wangu nilivyoondoka Tanzania nilijua naondoka kimoja, sikusema naondoka halafu nirudi.
Kurudi labda kuwe na msiba wa karibu sana nimelazimika, au jambo ka dharula kubwa kama hivyo.
Najua nikirudi nitaanza kugombana na watu tangu ubalozini hukuhuku kabla sijagusa Bongo.
Nikifika hapo huo ukiritimba wa airport tu najua nitagombana na watu.
Sasa kuondoa huo ugomvi ndiyo naona bora likizo niende Turks and Caicos tu 😂😂😂
Japan na Korea Kusini kama ziko over-civilized zaidi duniani labda zinashindana na nchi za Scandinavia, njoo bongo yetu sasa majanga matupu, wenye dini zao wanasema tunaishi tu kwa kudra na kadari za mnyazimungu😁Ndugu yangu 😃
Siye waafrika ni kama tumeumbiwa maisha ya purukushani flani hivi. Nchi za wenzetu huduma za kijamii ni jambo nyeti saaana.
Ngoja nikupe mfano: Miaka ya nyuma, niliwai kuishi Japan. Siku moja nimeamka kichwa kinauma sana. Nikaenda pharmacy nikanunua dawa (Japan masuala ya dawa za hospital yana uthibiti mkubwa, Kwahiyo ukienda kununua hata panadol watachukua taarifa zako n.k)
Kesho yake, watu wa pale pharmacy walinipigia simu kujua naendeleaje na kama nahitaji msaada wowote zaidi. Kisheria wanatakiwa kufanya follow up kunijulia hali. Ilinishangaza maana mimi niliitikia kimoyomoyo “ah wazee, kichwa tu mnakaba hivi?”
Kama mdau wa sekta ya afya natambua ni kiasi gani wagonjwa wengi wa saratani wanakufa kwa kukosa uduma za kutambua ugonjwa mapema, mbadala wa tiba kama chemotherapy/radiotherapy na patient care iliyo bora. Kwa wenzetu huku hata wagonjwa wa saratani wanayo matumaini kwa sababu ya huduma bora. Anyway, tumuombe Mungu 🙏😃
Maana yake unatibiwa kwanza kama utadaiwa ni baadaye.Baba Marekani ya wapi hiyo ambayo matibabu ni Bure ukipiga 911?
Japan na Korea Kusini kama ziko over-civilized zaidi duniani labda zinashindana na nchi za Scandinavia, njoo bongo yetu sasa majanga matupu😁
Bodaboda umezitaja. Zinaua sana watu hizi.Ndio maana wajapan wanaishi hadi miaka 90+. Huduma za kijamii zikiwa safi inaboresha sana quality of life ya watu. Sasa bongo bodaboda kapata accident mbaya anakimbizwa hospital wanaanza kumdai sijui pf3, mara damu hakuna, mara sijui nini. Hapo akirudi nyumbani anakuta maji yamekatika 😆😆. Frustrations tupu.
Ali Mufuruki aliwahi kusema katika moja ya talks zake hapa bongo hata ukiwa tajiri uko na milioni 100 cash kwenye gari ukipata ajali mkoa wa pwani tu nje kidogo tu ya mji ambako hata sio mbali na jiji la Dar es Salaam sio ajabu kufa kwa kukosa huduma ya ambulance helicopter tu kwa wakati ikuwahishe hospital.Maana yake unatibiwa kwanza kama utadaiwa ni baadaye.
Siyo habari za kulazimishwa utoe oesa kwanza kabla ya huduma.
Na unaweza kufa kwa kukisa ambulance tu.
Au ambulance inaweza juwapo lakini unaishi uchochoroni haifiki.
Umasikini hauwezi kuisha Afrika kwa sababu Waafrika wameukubali umasikini.Ili tujikwamue kutoka kwenye umasikini huu lazima tukubali na kukiri kuwa SISI NI MASIKINI,ukishajua na kukiri hivyo lazima pia tukae chini tujiulize UMASIKINI WETU UNATOKANA NA NINI? baada ya hapo tujiulize JE NI NJIA GANI TUZITUMIE KUONDOKANA NA UMASKINI HUU? baada ya hatua moja baada ya nyingine tunapambana na umaskini huo. Lakini kwa hapa Afrika umasikini hauwezi kutoka kamwe ikiwa tu nchi za bara ulaya,amerika asia na kwingineko bado zitakuwa zinategemea raw materials kutoka kwetu. lazma tujue umasikini wetu unatokana na ukoloni mambo leo na ukitaka kupambana na ukoloni wa aina hii basi wewe utakuwa umeweka rehani maisha yako. so,afrika yatupasa tuukubali ukweli na tuishi nao, afrika ikiungana,kuwa kitu kimoja,sauti moja tutaushinda umasikini,lakini kwa kila nchi kupambana kivyake itachukua miaka 500 kuuondoa umaskini huu. cc HAYA LAND HOV
Halafu kuna masikini hata humu wamo utawasikia UKIWA NA PESA POPOTE ULAYA/USA.Naunga mkono hoja,
Unaweza ukawa tajiri na una Gari kali ila utapita kwenye Barabara mbovu,risk ya ajali coz watu wengi hawafuati sheria za barabarani,huduma ya uokoaji wakati wa dharura,
Ndio maana watu wengi wanaoenda abroad sio tu kwamba wanaenda kutafuta maisha bali pia kufuata huduma bora.
"In Japan a corrupt person kills himself. In China, they will kill him. In Europe they jail him. In Africa, he will present himself for election." ~ Prof. PLO LumumbaUmasikini hauwezi kuisha Afrika kwa sababu Waafrika wameukubali umasikini.
Hawafanyi jitihada za kitosha kuukataa umasikini.
Kuanzia viongozi mpaka wananchi wa kawaida.
Viongozi wana lawama kubwa, wana wajibu mkubwa, wanafungwa na kanuni ya "noblesse oblige" kwa sababu wao ndio wana wajibu wa kuongoza, na najua mara nyingine kuwasema wananchi inakuwa kama "blaming the victim" lakini hili ni tatizo la jamii nzima na hata hao viongozi ni zao la hii jamii.
Jamii ingejitambua na kusimamia kuupiga vita umasikini hata hao viongozi wabovu wasingeweza kuwapo.
Ndiyo maana kwenye tamaduni nyingine kiongozi akikumbwa na kashfa anaanza kujiondoa mwenyewe katika uongozi.
Hawa elites huwa wanajidanganya kwamba wanaweza kujitenga na matatizo ya nchi kwa kujijengea ma kasri yao, kuyafungia nyaya za umeme kiyalinda, kununua ma V8 yao, na ujinga mwingine mwingi kama huo, wakifikiri wanaweza kujitenga na matatizo ya kijamii.Ali Mufuruki aliwahi kusema katika moja ya talks zake hapa bongo hata ukiwa tajiri uko na milioni 100 cash kwenye gari ukipata ajali mkoa wa pwani tu nje kidogo tu ya mji ambako hata sio mbali na jiji la Dar es Salaam sio ajabu kufa kwa kukosa huduma ya ambulance helicopter tu kwa wakati ikuwahishe hospital.
Haurudi bongo sababu mifumo mgogoro ama sababu hauna hela?
Hapa bongo kuna watu wanatembea na escort na wanamiliki helkopta
Endelea kubeba box kaka ujipatie ridhiki yako