watu kama nyie ndio tunawahtaji sana katika bara hili. Lakini nyie ndo kwanza hamjali,mmekimbia na kuendelea kulidharau bara hili. Rudini tuanze ukombozi sasa.
Waafrika tunategeana sana.
Tunafikiri kuwa kuna "watu fulani" ndio tunawahitaji, na hao ndio watatutoa hapa.
Wakati hii ni kazi ya watu wote.
Nitakuoa story moja ya jamaa yangu yupo Ofisi ya rais Dodoma hapo sasa. Jamaa alisoma nje, akarudi Tanzania miaka hiyooo ya nyuma. Alirudi na moto sana akitaka kubadili mambo.
Alivyofika akakaa ofisi ya Makamu wa Rais (amekaa hapo mpaka Samia akahama naye kwenda Ofisi ya Rais).
Jamaa aliingia na moto sana wa kubadili vitu, lakini akakutana na institutional malaise. Anasema alitaka kubadili mifumo lakini akajikuta kakaa na wazee ambao huwezi hata kuwabadilisha watoke kwenye kile kiti physical wanachokalia. Washirikina kichizi.
Kuna mwingine alikuwa activist wa elimu, kasoma mpaka Harvard, kafanya kazi mpaka na watoto wa mitaani. Ana connections za kitaa na za Ivy League.
Kapigana sana kwenye u activism. Kikwete akamuona. Akamteua kuwa mshauri wa rais. Jamaa akasema sasa hapa nimepata kazi, nitashauri tubadili mambo kimfumo.
Akawa anamshauri Kikwete hapa tufanye hivi na vile. Basi akimshauri Kikwete, Kikwete anamwambia hilo tunalijua, ukienda Wizara ya elimu Katibu Mkuu atakupa studies tulifanya miaka mitano iliyopita ana data nzuri kuliko zako. Jamaa akishauri hapa tufanye hivi, anaambiwa hapo tulishapita miaka saba iliyopita, nenda kwa Naibu Waziri atakupa makabrasha yote.
Jamaa akashangaa, akasema mimi nilifikiri hawa watu wanashindwa kwa sababu hawana taarifa, kumbe wana taarifa kunipita mimi, wanakosa nia tu.
Akaondoka serikalini akaenda zake New York City kupiga kazi za kimataifa.
Tuna matatizo ya mfumo, tuna matatizo ya utamaduni, haya hayamaliziki na mtu mmoja hata awe mzuri vipi. Tunahitaji critical mass, paradigm shift, ya kijamii.
Mimi hata nikiwa mzuri vili sina uwezo wa kuibadili hii jamii. Jamii inatakiwa kubadilika kwa nguvu za wengi ndiyo tupate mabadiliko ya maana.
Na sasa hivi kwa uchawa huu unaoshamiri sioni nguvu hiyo.