Matani

Matani

ati unafanya kazi kwenye kiwanda cha unga...ukioga unanukia ugali ulioiva!
 
- Mentor, inaonesha wewe mjinga kiasi ulimwuliza Bill Gates kwa nini anauza Windows (madirisha) badala ya milango.
- Uko mweusi mpaka ukisimama mbele ya "Blackboard" ikiwa hukucheka huonekani.
- Una sura mbaya mpaka mama yako anakiri kuwa wewe mbaya.
- Unaharisha mpaka unatembea mbele ya mabata ili kujizimua.
 
Unajifanya mfanyabiashara mzuri mpaka ulienda Iceland kuwauzia mafriji Waeskimo.
 
Dada yako ni mshamba kiasi hujitia manukato anapotaka kupiga picha ili picha yake inukie!!
 
Asprin: Mwangalie kwanza, una machunusi mpaka ukipigwa picha inatokea kama msasa
Daughter: (natanguliza samahani)..wewe una MEWATA kubwa mpaka unavaa bra long-sleeved!!!!lol
Hashy: Nyie kwenu ni maskini mpaka mnakula ugali na hadithi za nyama..
Gongotamu: kwenu ni kuchafu mpaka wewe hutoa viatu ukitoka nje..hahahahahahaha (got u..)
Afrodenzi: wewe ni mfupi mpaka voters ID card yako ina picha yako ukiwa umesimama...teh teh teh...
The next reader: Wewe ni mbaya mpaka siku za cha mama na baba wewe ulikuwa mbwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:smile-big::smile-big::smile-big:
Twende twende kwenye ukoo wenu wewe ndio mrefu kama chupa ya vimto
 
Duh! Washikaji mmenikumbusha mbali saaana! Salute Mentor! Paka wako noma mpaka akishika panya anaomba uma, chumvi na pilipili.
 
Kwenu ni wakristo mpaka mbwa wenu wakiona mwizi anaiba, wanawaambia "wee iba tu Mungu anakuona".

 
Duh! Washikaji mmenikumbusha mbali saaana! Salute Mentor! Paka wako noma mpaka akishika panya anaomba uma, chumvi na pilipili.

(Natanguliza apology)
Demu wako ni mshamba mpaka bra yake imeandikwa, "WEKA MATITI HAPA!"
 
Back
Top Bottom