Matapeli wa ardhi Morogoro wanatamba wanavyotaka kwakuwa wanashirikiana na baadhi ya watumishi wa Serikali

Matapeli wa ardhi Morogoro wanatamba wanavyotaka kwakuwa wanashirikiana na baadhi ya watumishi wa Serikali

Old Woman

Member
Joined
Apr 22, 2020
Posts
69
Reaction score
131
Naam hili halina ubishi.

Morogoro kumekuwa na migogoro mingi sana ya ARDHI ambapo chanzo ni matapeli kuuza maeneo ya watu.

Matapeli wa Morogoro wanatamba Wanavyotaka na wanatapeli pesa nyingi sana kupitia kuuza maeneo ya watu, wamekuwa na kiburi Kwa vile mgao wanapeleka Kwa wakubwa wa polisi na polisi wapelelezi. Yaani Hawa Wana mtandao kuanzia RPC, wapelelezi baadhi ya mahakimu na watu wa ARDHI

Morogoro ukitapeliwa ARDHI ukimpeleka mtu wako kituoni kesho anarudi uraiani na anaendelea kutapeli na hakuna kinachoendelea.

Naandika haya nikiwa nimejionea mwenyewe, ni kitendo Cha kusikitisha kuona mtu kama RPC anajihusisha katika vitendo ambavyo vinawaumiza wananchi ambao yeye amepewa dhamana ya kushughulikia usalama wao Huku akishare good time na matapeli.

Pale morogoro polisi pameoza, vyombo vya juu chunguzeni, migogoro ya ARDHI MOROGORO chanzo ni hizi taasisi za umma wanawajua matapeli na wao wanawapa mbinu za kukwepa wakitapeli na kutoa mgao.

RPC wa morogoro ni jibu sana.
 
Ila polisi kiukweli ndio wanaosapoti uhalifu mtaani, IGP mpya inabidi alitazame hili. Maana uwezo wa kuzuia wanao japo wapo wachache waaminifu
 
Mama mrudishe tu LUKUVI no matter what?, ARDHI kumeoza, offcourse waziri anajisikia vibaya sana dada yetu lakini it's too much, huku dar watumishi wanaita kupiga mbata yaani mwenye haki anapigwa la macho, na tapeli ndio anatamba, THIS IS WONDERFUL!,
Waziri awe na dawati la kusikiliza malalamiko tena yeye binafsi ndio awe msikilizaji, kwa mikoa sugu. (sikumuweka naibu kwa maana maalumu)
 
Hata mimi Huwa nashangaa inakuaje Tapeli anatamba mtaani kama vile hatuna vyombo vya sheria
 
Niliwahi kusikia hii wanakuja na full document wasimulia historia ya eneo mpka wakupige
 
Cheo Kama RPC Unawezaje Kwenda Kwa Mtu Wa Kawaida Kumpora Ardhi
Mkuu Mwaga Nondo Tu Hapa Hapa Ili Wote Waone
 
Mama mrudishe tu LUKUVI no matter what?, ARDHI kumeoza, offcourse waziri anajisikia vibaya sana dada yetu lakini it's too much, huku dar watumishi wanaita kupiga mbata yaani mwenye haki anapigwa la macho, na tapeli ndio anatamba, THIS IS WONDERFUL!,
Waziri awe na dawati la kusikiliza malalamiko tena yeye binafsi ndio awe msikilizaji, kwa mikoa sugu. (sikumuweka naibu kwa maana maalumu)
Kwahiyo akifa Lukuvi na wizara ya ardhi haitakuwepo? Maana mnavyomkazania Lukuvi arudishwe utadhani kazaliwa na hiyo wizara nyie wasukuma
 
Mkuu ungeeleza kwa kirefu ina maana mnatapeliwa na hazifikishwi mahakamani au
 
Mwenyewe nimetapeliwa hukohuko naufatilia huu Uzi Kwa ukaribu sana nipate kinachoendelea
 
Ila polisi kiukweli ndio wanaosapoti uhalifu mtaani, IGP mpya inabidi alitazame hili. Maana uwezo wa kuzuia wanao japo wapo wachache waaminifu
Polish polish polish duuh Hawa watu waongezewe tu mishahara
 
Back
Top Bottom