Matapeli wamekuwa wengi tuwe makini ndugu zanguni

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Miezi kadhaa iliyopita kuna jamaa nilikutana nae kwenye mgahawa, alinifuata kwenye meza yangu wakati napata

Kifungua kinywa, akaniambia anaomba nimsaidie chochote kwani mke wake amejifungua kwa operation na bado

Yupo hospital hana msaada wowote.

Kwa kifupi niliguswa na maneno yake ukizingatia jamaa alikuwa anaongea kwa hisia hadi anataka kulia,

Ikabidi nimpe chochote kitu na pole nyingi pamoja na maneno ya kumtia moyo.

Sasa baada ya miezi kama 3 kupita nikakutana nae tena akanisimamisha, hapo inaonekana alishanisahau kabisa,

Cha ajabu akawa ananieleza the same story, kuwa mkewe amejifungua kwa Op na hana msaada, sikumjibu nikaondoka na hamsini zangu.

Umewahi kukutana na utapeli wa namna yoyote? share experience tujifunze.
 
Huyo siwezi kumuweka kwa kundi la matapeli moja kwa moja

Inaonekana ni mtu tu mwenye shida huku mjini pengine hana kibarua hivyo anatafuta namna ya kuishi; japo sio vizuri kudanganya
 
Mkuu hata kusema uongo ni utapeli pia
 
  • Hao wapo wengi sana maeneo ya hosptali.
  • Nilivyoona matapeli nikadhani ni wale wa "ile hela tuma namba hii...". Maana kuna wadau nasikia wamempiga mtu 120m siku chache zilizopita
 
Miezi kadhaa iliyopita kuna jamaa nilikutana nae kwenye mgahawa, alinifuata kwenye meza yangu wakati napata

Kifungua kinywa, akaniambia anaomba nimsaidie chochote kwani mke wake amejifungua kwa operation na bado

Yupo hospital hana msaada wowote.

Kwa kifupi niliguswa na maneno yake ukizingatia jamaa alikuwa anaongea kwa hisia hadi anataka kulia,

Ikabidi nimpe chochote kitu na pole nyingi pamoja na maneno ya kumtia moyo.

Sasa baada ya miezi kama 3 kupita nikakutana nae tena akanisimamisha, hapo inaonekana alishanisahau kabisa,

Cha ajabu akawa ananieleza the same story, kuwa mkewe amejifungua kwa Op na hana msaada, sikumjibu nikaondoka na hamsini zangu.

Umewahi kukutana na utapeli wa namna yoyote? share experience tujifunze.
Ungemfungukia tu mkuu
 
Baada ya miezi mitatu? 😀
Ungemwambia huyo mkeo anajifungua kila baada ya miezi 3, maana nilishakusaidia kuhusu hili tatizo miezi 3 iliyopita.

Dar, watakuomba nauli, ukimwambia panda gari nikulipie uondoke atakuambia basi ili umuache
 
Wanatembea hadi na picha za marehemu eti yuko mortuary wameshindwa kuchukua mwili sababu ya gharama za matibabu kumbe matapeli
 
Siku Moja natoka maeneo ya nyumbani kama saa 1 asubuhi nafanya jogging kuelekea gym, nikakutana dada mmoja smart sana mzuri tu akanisimamisha, akaniambia sijui katapeliwa anahitaji nauli ya kurudi kwao mkoani, binafsi kwa muonekano wake sikutilia shaka story yake, kwenye track suit nilikua nimebeba elf 10 kwa maana ya kulipia gym elf 2, ikabidi tutafte mahali nikampa elf 8 nikabaki na elf 2 nikaenda zangu gym...nikamwambia ndo ninayo Hio

Fast forward ikapita kama miezi 6 nipo naelekea home, nakutana nae tena(hapa nikawa simkumbuki) akanipa same story, sasa sijui Nini nahisi kama hii sauti mbona sio ngeni... Kumcheki vizuri nikamkumbuka ni yeye, nikamtazama nikamuuliza unanikumbuka, dada hakunijibu akasepa zake kwa spidi, nikasema tu ile elfu 8 nilipigwa na watoto wa town
 
Miezi kadhaa iliyopita kuna jamaa nilikutana nae kwenye mgahawa, alinifuata kwenye meza yangu wakati napata

Kifungua kinywa, akaniambia anaomba nimsaidie chochote kwani mke wake amejifungua kwa operation na bado

Yupo hospital hana msaada wowote.

Kwa kifupi niliguswa na maneno yake ukizingatia jamaa alikuwa anaongea kwa hisia hadi anataka kulia,

Ikabidi nimpe chochote kitu na pole nyingi pamoja na maneno ya kumtia moyo.

Sasa baada ya miezi kama 3 kupita nikakutana nae tena akanisimamisha, hapo inaonekana alishanisahau kabisa,

Cha ajabu akawa ananieleza the same story, kuwa mkewe amejifungua kwa Op na hana msaada, sikumjibu nikaondoka na hamsini zangu.

Umewahi kukutana na utapeli wa namna yoyote? share experience tujifunze.
Yes,
nshakutana nao huwa hawakumbuki kabisaa 🐒
 
Hivi hapa mjini mtu humjui anakusimamishaje na kuanza kukuelezea upuuzi kama huo. Wacha muibiwe Tu.
Kanuni ya kwanza mtu akikupa salamu respond kwa ishara hakuna kujibu kwa neno wala kushikana mikono. Mjini hapa shauri zenu. Kuna watu vigagula Kwanza wananusa pesa hata kama elfu 10 unaibiwa.
 
Back
Top Bottom