Uchaguzi 2020 Matarajio ya Lissu yalikuwa ni kuona Kampeni zinajikita kwenye vijembe na vurugu

Kumbe matajiri huwa wanawekeza kwa ccm kwa kuwa inalipa, sasa huwa mnawapa nini hao matajiri in return?

Halafu mwenyekiti wenu anajitapa kwamba atawakomesha mafisadi na wala rushwa wakati mafisadi ndio wanaoendesha kampeni za ccm na watoa rushwa wakubwa ni wanachama wa ccm

Mpaka sasa mahakama ya mafisadi haijawahi kumuhukumu mtu hata mmoja, hamuoni kama mnatia aibu?
 
Hakuna mtu wa kumakamata huyo mtu wenu ndio maana unaona alipofika tu akaanza kuhangaika akamatwe ili yule beberu wake apate cha kusema.
[emoji3][emoji3][emoji3]
Ningekuwa Mimi JPM kura zingehesabiwa kwa wazi kabisa mbele ya watu kila kituo , cha msingi ulinzi uwepo wa kutosha ili kichaka wanachojifichia kila mwaka cha kuibiwa kura kichomwe Moto 😀😀, Lissu mweupe Sana
 
Mbowe anazunguka naye shingo upande kwenye uzinduzi tu wa jimbo moja moja kwenye Kanda akishamaliza hapo anambwaga aendelee mwenyewe yeye atarudi jimboni kwake kupambana na hali yake

Hapo sasa Lisu kazi kwake na Salum Mwalimu wake

Taarifa zilizopo ni kuwa mbunge atakayemtaka Lisu aende kwake invoice inamsubiri.Amtumie kwanza mheshimiwa mgombea Lisu nauli na posho ili aende,asipotoa Lisu haendi sababu pesa hana na chama hakina!! Mbowe kaamua kuwatupia wagombea kila moja ajitwike Lisu kichwani anayemtaka akamfanyie kampeni kwake.Chama hakina mbeleko ya kuendelea kujitwika yeye Lisu si muda mrefu Lisu tutamuona akipaki gari ya kampeni kimya kimya akisubiri mialiko ya wagombea !!!

Sasa ndio watakumbuka waliyomuzomea Lijuakali kuwa ile michango uliyokuwa Mbowe ukikata madiwani na wabunge ukisema ni ya kampeni 2020 pesa iko wapi mbona tunatakiwa kumkodi hata mgombea uraisi kuja kwetu?
 
Tuliza akili ndio ujibu posts zangu.
Mwaka 2015 mlipata fedha za wafanyabiashara wachache wakiamini lowassa angeshinda mwaka huu hakuna mfanyabiashara atakayeweza kujitoa ufahamu kumsupport lissu kwani hauziki kama mgombea urais.
Pili mlitegemea fedha za wahisani ambao nao wapo hoi kwa covid 19 ...
 
Ningekuwa Mimi JPM kura zingehesabiwa kwa wazi kabisa mbele ya watu kila kituo , cha msingi ulinzi uwepo wa kutosha ili kichaka wanachojifichia kila mwaka cha kuibiwa kura kichomwe Moto [emoji3][emoji3], Lissu mweupe Sana
Kabisa mkuu!

Hiki kichaka lazima kitafyekwa tu! Hata hivyo lazima waje na visingizio vingine
 
Mkuu huwezi ifananisha ccm na chadema
Ccm wana mtaji wa fedha, vyombo vya dola, vyombo vya habari nk

Chadema wangekuwa sawa kwa rasilimali hizo, pasingetosha
 
UMENIWAHI DAKIKA MOJA TU,nilikuwa namalizia kuandika post kama hii, nimeamua kuifuta na kukuunga mkono kwa maoni yako TRUE SAID MKUU 100%
 
unafanaisha watu wanaotumia magari ya na facilities zote za serikali dhidi ya wanaotegemea michango ya wananchi wanyonge wanaotoa kwa moyo? kweki we mjinga sana.
 
Naombeni ratiba za hashimu rungwe, huyo ndo amenikosha na ahadi za kufukirika nampa kura yangu,
 
Tuliwahi kuhoji hizi fedha zinaenda wapi wakatunanga sana
 
Ngoja waanze kukatana mitama hao watoa burudani. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Upeo wako ni zero kabisa, nimekuuliza what do you really pay those business tycoons in return baada ya uchaguzi?

Huna jibu, unakuja na habari za lissu hauziki, kwani wapiga kura ni wafanya biashara? Ni wananchi tena wa hali ya chini mliowabomolea nyumba zao na kutafuna pesa za majanga
 
unafanaisha watu wanaotumia magari ya na facilities zote za serikali dhidi ya wanaotegemea michango ya wananchi wanyonge wanaotoa kwa moyo? kweki we mjinga sana.
Magari gani kwa mfano?ni yale malori mnayosema yanasomba watu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…