Matatizo mengi tuliyonayo nchini leo yameanzia na awamu ya tano; hapakuwepo na uhuru wa kusema wala kurekebisha mambo, sasa tunalipa kwa maumivu

Nafikiri watanzania wengi hamwelewi kabisa mambo yanavyokwenda na ni rahisi mno kudanganyika na siasa nyepesi nyepesi.
Wewe zombokoko taila unaelewa nini
Yaani hii inchi ina mataila mengi ikiongozwa na wewe
 
Mkuu acha uongo, kipindi cha Mwendazake mgao wa umeme ulikuwepo, sukari iliadimika ikapanda bei, kilimo kiliporomoka, ajira zilisimama na biashara zilikufa. Kadanganye kwingine sio humu!
Kama hali ilikuwa hivi kama Ulivyoandika, ilikuwaje Uchumi ukapanda?
 
Wewe zombokoko taila unaelewa nini
Yaani hii inchi ina mataila mengi ikiongozwa na wewe
Uchumi na ustaarabu wa nchi hii uliharibiwa sana wakati Magufuli alipokuwa rais. Wajinga wanafikiri ni uzushi! Watu wameteswa na kuuwawa akina Lissu na Ben Saanane ni vielelezo wazi.
 
Sijaelewa hapo kwa lisu na Ben na uchumi panahusika je kuharibu uchumi ..hatakam wsngekufu waking lisu 100 inahusikaje na uharibu wa uchumi
 
Kuna mambo mengi watanzania wenye akili nyepesi nyepesi hawawezi kuyaona. Matatizo mengi tuliyonayo sasa hivi kama uhaba wa dola, umeme, ukosefu wa sukari n.k. yalitokana na utawala wa kuburuza mambo wa awamu ya tano.

Nawaambia, saa hii tungekuwa kwenye hali ya tahadhari na majanga makubwa kiuchumi na kijamii. Magufuli hakuwa na upeo mkubwa kiuchumi, yeye alilazimisha kila kitu kama alivyopenda bila kujali matokeo yake. Leo tunateswa na matatizo ambayo chimbuko lake ni awamu ya 5 na hakuna kiongozi atakayetuambia ukweli huu!

Kuna vikundi vichache vya wahuni wananufaika na ujinga wa waTanzania (elite capture).
Na hao wahuni walianza toka awamu ya kwanza! Rejea hotuba za Nyerere, Mtikila, Lowassa n.k
 
Hata wangekuwa 100% ni wale wale tofauti ya uongozi ina influence kubwa sana how people behave.

Magufuli alikuwa hands on kwenye domestic challenges, well informed on what is going serikalini saa zingine kabla ya matukio ya upigaji kutokea na anataka maelezo na solution (options) mambo yakienda mrama.

Huyu mama toka sakata la umeme, sukari na report za CAG kama vile sio yake, yeye ni raisi wa Tanzania ya kufirika sio ile yenye ardhi na watu anaotakiwa kuwaongoza na kuwasimamia. Anachojua ni kusafiri, kuteua, kuhudhuria makongamano na kutoa pongezi za mafanikio ya michezo tu. Yale magumu ya nchi hana habari nayo zaidi ya kuwatafutia hela za kwenda kutumbua huko serikalini.
Misingi ya taifa chini ya ccm ilishabomoka kitambo.
Option ni moja tu kati ya mbili!
1. Kuwa chawa uendeleze ujinga
2. Kuwa mzalendo ingia barabarani
 
Leo karibu nusu nzima ya mashine za kufua umeme wa gesi pale Ubungo na Kinyerezi zimeharibika kwa mkupuo baada ya kulazimishwa kufanya kazi zikiwa mbovu! Matokeo yake leo hii tuna mgao ambao hata viongozi wetu hawana lugha nzuri ya kuulezea; watasema ni upungufu wa mvua hata pale ambapo El Nino zilikuwa tele kuanzia mwaka jana mwishoni. Hutasikia wakisema ukweli huu kuhusu ubovu wa mashine zitu, utawasikia wakisema ni ongezeko la matumizi ya umeme, hilo nalo ni uongo tu.
Kwenye hili naunga mkono 100% kuhusu Dola na sukari atasingiziwa mana haya mawili ni mchakato WA uzembe Kwa wahusika.
Hakuna kipindi Taifa/TANESCO liliingia hasara Kama awamu ya 5 hili limebaki kuwa Siri kubwa hata miongoni mwa watumishi WA shirika.
 
Kabla ya 2015 angalau kulikuwa na uhuru wa kusema,

Andiko lako halina mantiki yeyote.
(1) Kisasa: Kikwete alikuwa anasema "kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala", yaani ulikuwa kumbe wewe unafurahia kupiga kelele hata kama ni wazi kuwa hazisikilizwi? Kuna nchi kama China ambako watu hawasemi chochote kuhusu sericali na CCP lakini wanaendelea.

(2): Kifundi: Service ya machine yoyote ya motoinayofanya kazi masaa 24 inahusu lubrication na cooling system tu. Parts zenye life span kama bearings hubadilishwa baada ya masaa 50,000 hadi 60,000 ambayo ni interval ya takriban miaka saba. Sehemu nyingine zote huwa hazihitaji kubadilishwa labda kama machine haikuwa na lubrication inayotakiwa.

(3)Jumla: Kwa jinsi ulivyoandika, kumbe mweneztu ulitaka angalau Umeme uwe unakatika mara kwa mara hata wakati wa Magufuli pamoja na kuwa mchine zilikuwa ni nzima? Unaleta lugha za jumla jumla zenye lawama kuwa machine zimekufa zote bila hata kujiuliza zimekufa kitu gani. Akili ndogo sana hiyo
 
Uchumi na ustaarabu wa nchi hii uliharibiwa sana wakati Magufuli alipokuwa rais. Wajinga wanafikiri ni uzushi! Watu wameteswa na kuuwawa akina Lissu na Ben Saanane ni vielelezo wazi.
Inaonekana unaliwa kiboga sasa Lisu na huyo ben saanane wanausikaje na uchumi wa Tanzania??
Kwa hiyo kipindi hichi ndio uchumi upo sawa?? Mbona hatuoni hata miradi mipya iliyoanzishwa zaidi ya miradi ileile ya Magufuli??
 
Sorry ni awamu ya 5 ya bullzoda sio ya nne! Awamu ya 4 ilikuwa baba wa demokrasia.

Kabla ya 2015 angalau kulikuwa na uhuru wa kusema, ukweli ulijulikana na uliachwa usemwe kwa kiasi kikubwa, na wataalamu waliachwa watumie taaluma yao kutoa miongozo, lakini alipokuja Magufuli yeye aligeuka kuwa engineer, docta, mchumi, na kila kitu.

Kuna mambo mengi watanzania wenye akili nyepesi nyepesi hawawezi kuyaona. Matatizo mengi tuliyonayo sasa hivi kama uhaba wa dola, umeme, ukosefu wa sukari n.k. yalitokana na utawala wa kuburuza mambo wa awamu ya tano.

Mfano umeme: Wakati wa Magufuli mashine nyingi za kufua umeme kwa kutumia gesi zilifanya kazi na kupitiliza wakati wake wa kufanyiwa ukarabati. Tanesco walilazimika kuendelea kufua umeme na mashine zilizokuwa zinahitaji kufanyiwa ukarabati kwani Tanesco wangeondoa baadhi ya machine ili kufanya ukarabati kungesababisha upungufu wa umeme na mgao kitu ambacho kingepelekea wao kufukuzwa kazi mara moja. Hivyo waliendelea kuzalisha umeme na mashine zilizokuwa hoi.

Leo karibu nusu nzima ya mashine za kufua umeme wa gesi pale Ubungo na Kinyerezi zimeharibika kwa mkupuo baada ya kulazimishwa kufanya kazi zikiwa mbovu! Matokeo yake leo hii tuna mgao ambao hata viongozi wetu hawana lugha nzuri ya kuulezea; watasema ni upungufu wa mvua hata pale ambapo El Nino zilikuwa tele kuanzia mwaka jana mwishoni. Hutasikia wakisema ukweli huu kuhusu ubovu wa mashine zitu, utawasikia wakisema ni ongezeko la matumizi ya umeme, hilo nalo ni uongo tu.

Matatizo ya sukari na dola yana mkondo huo huo. Nani asiyejua namna Magufuli alivyoharibu biashara kwa kuwabambikizia kodi wafanyabiashara, kuwapora mitaji na kuwalazimisha kufunga biashara zao kwa visingizio vya kodi? Matokeo ya hayo ndio leo tunayaona. Biashara kati ya Tanzania na nchi za nje ilidorora mno wakati wa Magufuli. Si mnakumbuka jinsi Magufuli alivyowachukia "mabeberu"? Unategemea nini kibiashara unapowachukia bussiness partners na kufunga biashara zao nchini?

Ila kwakuwa watanzania wengi wamelishwa uongo na hawana jinsi ya kugundua uongo huo basi wataamini kuwa Magufuli angekuwepo mambo yangekuwa mazuri. Nawaambia, saa hii tungekuwa kwenye hali ya tahadhari na majanga makubwa kiuchumi na kijamii. Magufuli hakuwa na upeo mkubwa kiuchumi, yeye alilazimisha kila kitu kama alivyopenda bila kujali matokeo yake. Leo tunateswa na matatizo ambayo chimbuko lake ni awamu ya 5 na hakuna kiongozi atakayetuambia ukweli huu!
Kwenye ishu ya umeme usiandike kabisa!!

Unakidhalilisha chama changu CCM!!

Tumeshindwa kutengeneza umeme was uhakika tangu 1961 kisa ni kuendekeza biashara za makada Ili wakisaidie chama kana kwamba Chama ni kilema!!

Huo ni uzembe!

Serikali ilipaswa full control kwenye umeme ,maji,matibabu na sekta mtambuka nyinginezo na sio kuwaachia makada wapigaji waliotufikisha hapa!!

Bora usingeandika kuhusu umeme!!
 
Inaonekana unaliwa kiboga sasa Lisu na huyo ben saanane wanausikaje na uchumi wa Tanzania??
Kwa hiyo kipindi hichi ndio uchumi upo sawa?? Mbona hatuoni hata miradi mipya iliyoanzishwa zaidi ya miradi ileile ya Magufuli??
Hata kutetea tu ccm huwezi? Huoni miradi yoyote iliyoanzishwa na chama chako ccm? Au wewe unamtetea tu Magufuli? Panua wigo wako wa kufikiri, umeishia darasa la ngapi?
 
kwa akili hizi mwatawala wataendelea kutuona manyani kila siku
 
Hata kutetea tu ccm huwezi? Huoni miradi yoyote iliyoanzishwa na chama chako ccm? Au wewe unamtetea tu Magufuli? Panua wigo wako wa kufikiri, umeishia darasa la ngapi?
Wewe chizi mimi sina chama natetea yoyote anayefanya vizuri na katika Marais waliofanya vizuri ni Magufuli na laiti angekuwepo bado Tanzania tungekuwa juu na sizani kama East Africa kuna nchi ingetufikia sasa hivi pesa zinaenda kwa majizi badala ya miradi
Maisha yanakuwa magumu na nchi haiendi
Kuhusu elimu yangu ukoo wenu hakuna wa kunifikia
Na kama wewe ndio msomi kwenye ukoo wenu basi ukoo wenu ni machizi wote
 
Sorry ni awamu ya 5 ya bullzoda sio ya nne! Awamu ya 4 ilikuwa baba wa demokrasia.

Kabla ya 2015 angalau kulikuwa na uhuru wa kusema, ukweli ulijulikana na uliachwa usemwe kwa kiasi kikubwa, na wataalamu waliachwa watumie taaluma yao kutoa miongozo, lakini alipokuja Magufuli yeye aligeuka kuwa engineer, docta, mchumi, na kila kitu.

Kuna mambo mengi watanzania wenye akili nyepesi nyepesi hawawezi kuyaona. Matatizo mengi tuliyonayo sasa hivi kama uhaba wa dola, umeme, ukosefu wa sukari n.k. yalitokana na utawala wa kuburuza mambo wa awamu ya tano.

Mfano umeme: Wakati wa Magufuli mashine nyingi za kufua umeme kwa kutumia gesi zilifanya kazi na kupitiliza wakati wake wa kufanyiwa ukarabati. Tanesco walilazimika kuendelea kufua umeme na mashine zilizokuwa zinahitaji kufanyiwa ukarabati kwani Tanesco wangeondoa baadhi ya machine ili kufanya ukarabati kungesababisha upungufu wa umeme na mgao kitu ambacho kingepelekea wao kufukuzwa kazi mara moja. Hivyo waliendelea kuzalisha umeme na mashine zilizokuwa hoi.

Leo karibu nusu nzima ya mashine za kufua umeme wa gesi pale Ubungo na Kinyerezi zimeharibika kwa mkupuo baada ya kulazimishwa kufanya kazi zikiwa mbovu! Matokeo yake leo hii tuna mgao ambao hata viongozi wetu hawana lugha nzuri ya kuulezea; watasema ni upungufu wa mvua hata pale ambapo El Nino zilikuwa tele kuanzia mwaka jana mwishoni. Hutasikia wakisema ukweli huu kuhusu ubovu wa mashine zitu, utawasikia wakisema ni ongezeko la matumizi ya umeme, hilo nalo ni uongo tu.

Matatizo ya sukari na dola yana mkondo huo huo. Nani asiyejua namna Magufuli alivyoharibu biashara kwa kuwabambikizia kodi wafanyabiashara, kuwapora mitaji na kuwalazimisha kufunga biashara zao kwa visingizio vya kodi? Matokeo ya hayo ndio leo tunayaona. Biashara kati ya Tanzania na nchi za nje ilidorora mno wakati wa Magufuli. Si mnakumbuka jinsi Magufuli alivyowachukia "mabeberu"? Unategemea nini kibiashara unapowachukia bussiness partners na kufunga biashara zao nchini?

Ila kwakuwa watanzania wengi wamelishwa uongo na hawana jinsi ya kugundua uongo huo basi wataamini kuwa Magufuli angekuwepo mambo yangekuwa mazuri. Nawaambia, saa hii tungekuwa kwenye hali ya tahadhari na majanga makubwa kiuchumi na kijamii. Magufuli hakuwa na upeo mkubwa kiuchumi, yeye alilazimisha kila kitu kama alivyopenda bila kujali matokeo yake. Leo tunateswa na matatizo ambayo chimbuko lake ni awamu ya 5 na hakuna kiongozi atakayetuambia ukweli huu!
Nimesoma tu ulivyoelezea suala la umeme nikaona unachoongea hakina mashiko.
Baada ya kifo cha Magufuli aliteuliwa J. Makamba kuwa Waziri wa Nishati. Hoja yake ya kwanza ilikua ni mgao ili kukarabati mashine. Jiulize toka Septemba 2021 bado wanakarabati mitambo tu ?
Yaani miaka miwili na nusu wanafanya ukarabati tu. Kama ni kweli basi ilipaswa wafukuzwe wote kwa kuwa hawawezi kazi.
Jiulize mitambo inaweza kumtii mwanadamu kuwa hata ikiwa imechoka ifanye tu kazi kwa kuwa boss atatumbuliwa ? Tumia fikra pevu kuwasilisha hoja maana utaonekana unaongea pumba.
 
Magari yanatapaswa kufanyiwa service kila baada ya kilometer kadhaa, lakini wapo wanaooitiliza hata mara 2 ya muda uliopangwa. Ndivyo ilivyofanyika kwa mashine za kufua umeme zililazimishwa kufanya kazi bila service leo nyingi zipo juu ya mawe. Magufuli aliagiza hivyo; sitaki kusikia umeme umekatika nikisikia nitakutumbua. Watu wameua mashine zetu kwa mtindo huo.
 
Wewe chizi mimi sina chama natetea yoyote anayefanya vizuri na katika Marais waliofanya vizuri ni Magufuli na laiti angekuwepo bado Tanzania tungekuwa juu na sizani kama East Africa kuna nchi ingetufikia sasa hivi pesa zinaenda kwa majizi badala ya miradi
Maisha yanakuwa magumu na nchi haiendi
Kuhusu elimu yangu ukoo wenu hakuna wa kunifikia
Na kama wewe ndio msomi kwenye ukoo wenu basi ukoo wenu ni machizi wote
Magufuli akitumia propagandists kutangaza eti Tanzania tupo uchumi wa kati; unajua uhalisia wa jambo hilo? Ulikuwa ni uongo wa Magufuli kama ilivyokuwa kusema tunajenga miundombinu kwa fedha za ndani kumbe tunakopa. Leo ndio ukweli unazidi kujulikana kwani dikteta hayupo na watu wanasema bila woga. Je elimu yako imekusaidia kuona makosa ya Magufuli au na wewe umedanganyika kama kama mjinga?
 
Magari yanatapaswa kufanyiwa service kila baada ya kilometer kadhaa, lakini wapo wanaooitiliza hata mara 2 ya muda uliopangwa. Ndivyo ilivyofanyika kwa mashine za kufua umeme zililazimishwa kufanya kazi bila service leo nyingi zipo juu ya mawe. Magufuli aliagiza hivyo; sitaki kusikia umeme umekatika nikisikia nitakutumbua. Watu wameua mashine zetu kwa mtindo huo.
Kwa hiyo toka September 2021 mpaka leo February 2024 bado wanaendelea na service tu ?
Kumbuka hiki kisingizio Januari Makamba ndiye alikuja nacho alipoteuliwa. Inawezekana vipi kufanya service ya mitambo kwa miaka miwili na nusu ?
 
Ile mitambo ya kufua umeme sio kama hivi vigenerator vya mtaani ni custom made ni mikubwa mno na spea zake hazipo madukani hata huko Ulaya, unapaswa kuweka order utengenezewe. Hivyo hugharimu mabilioni ya fedha. Mingi ipo kwenye hali mbaya ndio maana ikiharibika huchukua muda mrefu kutengamaa.
 
Back
Top Bottom