Matatizo ya Samsung Galaxy S Series used hasa za kutoka Dubai

Matatizo ya Samsung Galaxy S Series used hasa za kutoka Dubai

Mkuu ukiambiwa Samsung S20, S21, S22 etc zilikuwa na shida ya green lines haimaanishi kila S20 inapata green lines
Halafu mbona mi naona ni simple sana kuelewa. Kama ulitumia S10 na haikupata green lines, tatizo liko wapi. Hakuna anayesema kila simu ya S series inapata green lines, ni kwamba watumiaji wengi wa Samsung walioathirika na green lines walikuwa ni watumiaji wa hizo models. Sio eti ilikuwa inatokea kwenye kila handset
Ok sawa nasema nimeanza kutumia hizo takataka toka S 10 plus mpaka leo tupo na S 23,S24 hizo step za nyuma zote nimesota nazo ndio maana nasisitiza masoko labda yatofautiane hapa nanunua pia hizo simu ila mpya naagiza Tanzania sijasikia kuambiwa kuna hilo tatizo ingawaje lipo kwa baadhi ya simu mnazosema..
 
Kenya kuna official stores za makampuni mengi ya kielektroniki. Walichagua kama "The African hub for electronics" ndio maana bei zake ziko chini kushinda bongo.
Ok sawa sawa sema Kenya kodi kwenye simu sio kubwa pia hata TV tofauti na hapo kwetu ndio maana vitu vingi watu wanafata Kenya wakato wao bandari yao ni ndogo ukilinganisha na sisi..
 
Mistari kwenye kioo kwa kiasi kikubwa hutokana na kuanguka/kugongwa gongwa kwa simu......
Kwa hiyo tatizo sio simu, tatizo ni utunzaji
Na Ujue Samsung S - Ultra, inakioo kikubwa sana na ni nzito; hivyo uwezekano wa kupata madhara ikiangushwa ni mkubwa zaidi. Unaweza kwenda S-plain ambazo ni ndogo kwa size; sijasikia hiyo changamoto kwa hizo ndogo
Japo ni kweli kuwa S20 - S22 zinaonekana kutokushika sana soko.....
Nina S22 nilinunua mwaka 2024 used from Japan miezi miwili sasa ina msitari
 
Back
Top Bottom