Je, tutafika! KIpindi cha Makwaiya, cha leo (1 mosi) saa mbili na nusu kilikuwa kinajadili ujio wa uchaguzi mkuu wa ccm kwa kutizama taswira ama visioni ya chama katika kuendesha chama kwa maslahi ya wananchi. Waalikwa kwenye kipindi walikuwa Balozi Daudi Mwakawago 2), Dr. Kamata (Idara ya Siasa UDSM) Yusuphu Khalimoja (Mwandishi)
Mambo mengi yaliibuliwa katika mjadala, lakini yanayokuja akilini haraka haraka, ni mambo makuu matatu: uanachama, itikadi, na visioni ya taifa
A: UANACHAMA
1. Kunamsemo maarufu, mara nyingi unatumika katika nyimbo ama misemo ya chama cha mapindizu nayo husema CHAMA KINAWENYEWE NA WENYEWE ndio SISI.
*Swali la msingi lililoulizwa wenyewe ni kinani?
Majibu:
a. Watu wa kawaida ni rahisi kusema ni wenye chama lakini sio viongozi- Yusuphu Khalimoja
b. Maneno hayo yanatumika kama kauli mbiu, kiasili, msingi wa chama ni watu, yaani wakulima na wafanyakazi. Msingi huu ndio uliisaidia TANU na CCM kuleta mapinduzi ya kijamaa, wanachama wakiwa askari wa mbele wa mabadiliko. leo swala ni ushindi wa uchaguzi, hakuna mafunzo ya kiitikadi wala historia ya chimbuko la chama. Hatari Kamata
c. Wanachama bado ni wakulima na wafanyakazi, ila kuna mkanganyiko. mkanganyiko unaletwa na historia ya mabadiliko ya dunia ya kiuchumi na kisiasa, ikitenganisha kati ya waasisi wa chama na wananchama wapya ama ambao wamebadilishwa na mabadiliko ya kihistoria, au kati ya wanachama waliopita katika tanuru ya itikadi na ambao hawakupitia- lazima migongano na mapambano yatokee katika fikira, mikakati, oganiizisheni - balozi
B: ITIKADI
2. Kunamkanganyiko kati ya itikadi ya chama na sera mbalimbali za nchi. Ukiangalia katiba ya nchi na katiba ya ccm toleo la 2005, lengo ni kujenga ujamaa na kukitegemea wakati nchi imejikita katika uchumi wa kidunia wenye maslahi ya kibeberu na utegemezi.
Maangalizo yaliyotolewa:a) kuna mkanganyiko kati ya itikadi na sera mbalimbali za nchi. Hii ni hatari ni sawa na dereva anayeonyesha ishara ya kukata kulia kumbe anaendelea mbele ama anakata kushoto, na hawa madereva ni wengi, matokeo yake ajali.
b) chama kimeacha taratibu zake za msingi ambazo zilikuwa zinaanda makada wa chama, viongozi na wanachama wa kawaida kikiwajenga kujua maslahi ya chama kwa taifa na kuwapa misingi ya kulinda maslahi ya nchi kwa manufaa ya taifa. Hatari yake ni kwamba vijana wa leo hawajui historia, misingi, itikadi wala visioni ya chama. Hili si tatizo la ccm tu ni vyama vyote vya siasa.
c
3. Ujamaa lengo lake ilikuwa kutengeneza fursa sawa kwa wanachi na kujenga uchumi wa kitaifa, taswira ama visioni iliyosahihi kabisa, haina kosa.
Swali: kama hatutaki usawa na uchumi wa kitaifa tunataka nini?
Misemo iliyokumbukwa.
Pale ambapo chama cha mapinduzi kitakapoacha ilikadi ya ujamaa na kujitegemea haitabaki- Nyerere
Chama changu kimetekwa nyara na Matajiri- Mkapa
Misemo iliyoibuka kwenye mjadala
Chama cha ccm kimebaki kama ganda la yai lakini ndani liko tupu- Kamata
Utabiri uliotolewa
Sitashangaa kuona viongozi wanochaguliwa katika mwaka huu wa uchaguzi kuweka mawazo yao kimaandishi Balozi
HATARI zilizobainishwa
Tabaka lawaliojuu linajizalisha lenyewe, linaanza kuachana na wabangaizaji, na walioko madarakani wameanza kujizalisha wenyewe.
CCM inabaki kuwa chama cha Uchaguzi, ili kubaki madarakani kinahitaji wakulima na wafanyakazi, si kwa nasaba, kwa kupata kura.
Kwa mtazamo wangu mimi, mjadala huu umeibua maswali ya msingi nayojiuliza kila siku na kichwa kinapata moto kidogo. Ningependa nasi tujiulize maswali hayo kwani ndio msingi wa mabadiliko yoyote yale tunayoyataka kwa taifa hili.
kwanza tujitambue sisi ni watanzania ndivyo tunavyotambulika., na tutaendelea kutambulika hivyo
pili tukubaliane matatizo yetu ya msingi ni yapi
tatu, ni lazima tukubaliane mbinu za kuondoa matatizo yetu
lakini la msingi kuliko yote ni kukubaliana itikadi ambayo ndio itajenga msingi wa mapambano yetu.
Historia yetu, inamafundisho mengi sana ambayo tukirudi nyuma na kutizama tutajifunza na kuendelea. Sioni haya kusema, kama kunawakati ambapo naona taifa hili lilipata kutoa mwelekeo thabiti na kutuonyesha sisi kama taifa sera za ujamaa na kujitegemee kupitia azimio la arusha na mwongozo. Sikujaliwa kuishi enzi hizo, ila niyasomapo maandiko hayo leo ninaona tungefika tu.
pamoja