Nilikuwa ughaibuni kitambo kidogo na kwanza nimerejea 'nyumbani' hali inasikitisha hasa ukiangalia maendeleo ya kiuchumi,kisiasa na kijamii ya nchi za wenzetu.Nimegundua wao ni binaadamu kama sisi kimaumbile ila tunatofautiana kwa kiasi kikubwa kwenye utashi kwa kujikomboa na kuwa na maendeleo endelevu,nimeweza kung'amua yafuatayo
- Waliopewa dhamana ya kuongoza wengi hawana utashi bali wamegubikwa na ubinafsi katika kuleta maendeleo.
- Hakuna uwajibikaji bali ni kulindana tu, viongozi wetu hawajifunzi kutoka nchi za wenzetu jinsi viongozi wanavyolazimishwa kujiuzulu wakiboronga..nilidhani kujiuzulu kwa raisi wa benki ya dunia kutawasaidia kufikiri vizuri
-
- Watanzania wengi ni wajinga ((kie limu) wanashindwa kufikiri vizuri ni vipi wajikwamue kutoka kwenye makucha haya.Ili tuwe na maendeleo ya kweli nadhani wananchi wapewe dhamana ya kuamua nchi iendeshwe vipi, lakini hili litafanikiwa ikiwa tu kama Uongozi wajuu utakubali wananchi ndio wawe na mamlaka ya kutaka nchi yao iongozwe vipi!
ahsanteni.
Nilivyokariri kama wananchi ni wajinga na uongozi wajuu lazima uwe tayari kufanya ujinga huu wa wananchi uondoke ili kuleta maendelo ya kweli ni wazi. Jana tu katibu mkuu wa CCM Luteni mstaafu Makamba akijibu hoja kama katika kinyanganyiro kwenye chaguzi za NEC ya CCM tayari harufu ya Rushwa imeshaanza kutawala na akasisistiza kama lazima wanaojihusisha na Rushwa wabainishwe...huu ndo ujinga nilioumaanisha na wananchi lazima wajengwe kifikra kama pesa,fulana,kofia,kanga,pilau nk zisiwe ushawishi wa kuchagua viongozi badala ya uwezo na utashi hasa wa kuleta mabadiliko. Wanzanchi walio wengi bado hawajaelemishwa haya, na nathubutu kuuita ujinga wa wananchi waliowengi.
Je kuna utashi wa kutosha kuwafanya wananchi waondokane na ujinga huu au waachwe tu walale?
YANGU MACHO kwani kama rais mwenyewe anawaogopa hao wala rushwa ni mwandishi yupi ataweza kuwataja?
Ni mwandishi yupi huyo ilihali huwa anapanda daladala na hana ulinzi wowote mwenye uwezo wa kuwataja waziwazi?kama rais mwenye ulinzi wote anasema wajirekebishe hii maana yake ni kuwa hawa watu ni WAKUMBWA.
Ilongo,
Utaumiza kichwa chako sana pasipo jawabu!
Binafsi mwanzo nilikuwa nikifikiria sana kuhusu wananchi kuli-shake Bunge na hata kuna wakati nimekubali kuwa labda wapinzani wajaribu maandalizi ya kuwa na wawakilishi wengi Bungeni, lakini mjomba nimegundua kuwa tatizo letu liko deep sana zaidi ya Bunge.
Ikiwa waziri mmoja tu anaweza kusimama Bungeni na kusema swala fulani halihusiani na Bunge ama Bunge halina mamlaka ya kupitia Mikataba ama kuitisha uchunguzi fulani mahala ambapo wameona kuwa sheria imepindwa! well hapa tuna tatizo kubwa.
Kusema kweli sioni kabisa mbele zaidi ya kujiuliza hivi kazi ya Bunge ni kitu gani?.. hata kama iwe utunzi wa sheria, je watawezaje kutunga sheria mahala ambapo hawaruhusiwi kutazama chanzo cha maovu?..ati sii kazi yao! sasa tunahitaji bunge la nini?
Je, kesho wapinzani wakichukua Bunge hivi kweli tunategemea kutakuwepo na mabadiliko iwapo leo hii Bunge ni chombo chini ya maamuzi ya serikali na sii kazi yao kupitia, kutazama matatizo na kutoa uamuzi kisheria unaoiwezesha serikali na watu wake kufanya kazi?
Zaidi ya yote haya, nina mashaka sana ktk utekelezaji wa serikali ambayo bunge zima lina wapinzani lakini nafasi ya Mtawala (RAIS) imeshikwa na chama tawala!.. hapa uundaji wa serikali utakuwa vipi ikiwa serikali leo hii ina madaraka makubwa kuliko Bunge..Je, huyu rais na serikali yake watawajibishwa vipi na Bunge ambalo halina nguvu wala mamlaka ya kumwajibisha rais na mawaziri wake!...
Humu ndani ya JF kuna mada nyingi sana zinazotupa picha mbaya sana ya Katiba ya nchi yetu na sielewi ni kipi kinachotakiwa kuwepo ili Katiba iweze kutungwa UPYA!.. majuzi tu kuna waziri kasema nje ya bunge kwa uhakika kuwa Katiba haiwezi kubadilika.... na kweli hiyo ndio IMETOKA!...sheria imewekwa na mtu mmoja tu kuondoa muswada bungeni!..Ebu nambie tutafika?
By Nthelezi Nesaa | Published Today | Nthelezi Nesaa | Unrated
Na HabariTanzania.com
Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kutamka maneno hayo hapo juu mwishoni mwa miaka ya 90 wakati wa awamu ya pili iliyoongozwa na shehe Ali Hassan Mwinyi maarufu kama mzee Ruxa.
Mwalimu aliyasema hayo kwa hasira na mfadhaiko baada ya kuwa vinaripotiwa visa vya wizi,ujambazi na kila aina ya ufisadi serikalini na Mwinyi asichukue hatua. Baya zaidi wakati ule safu hii inakumbuka, kiunganishi kikuu, kwa mujibu wa tuhuma za wakati ule, ilikuwa ni ikulu yenyewe ambapo bi mkubwa alituhumiwa kutumiwa na marafiki zake na wafanyabiashara wachafu kuliibia taifa.
Bahati nzuri wakati ule waswahili walikuwa hawajazoea pesa. Maana malalamiko yalituama juu ya kupata vidala dala kadhaa na viwanja vya nyumba. Mwalimu kama ada hakuacha kusema. Alizidi kumuonya Mwinyi mpaka wapambe wa Mwinyi wakasema Mwalimu alikuwa anamuonea wivu Mwinyi kwa maendeleo aliyokuwa amefikia. Wenye akili walijiuliza Mwalimu angemuonea wivu Mwinyi kwa lipi iwapo ndiye aliamua kwa makusudi kumuachia nchi.
Wakati ule Mwalimu alikuja na kombora jingine. Baada ya kuona wafanyabiashara wa kihindi wameigeuza ikulu kijiwe cha kufanyia dili, Mwalimu alisema Ikulu siyo sehemu ya kufanyia biashara patakatifu pa patakatifu
Tufupishe simulizi tuje kwenye mantiki ya maneno ya gwiji huyu. Je hali ya nchi yetu kwa sasa ikoje? Kusema ukweli inanuka kuliko wakati wa Mwinyi. Kama ni harufu basi wakati wa Mwinyi ulikuwa mchafuko mdogo wa tumbo kuliko huu uoza wa mwili mzima.
Tutatoa sababu. Nani anaweza kubisha kuwa kwa sasa nchi yetu inakabiliwa na kashfa nyingi tena kubwa ambazo kwa bahati mbaya wakubwa wanazifutika chini ya busati. Tukumbushane. Ilianza kashfa ya rada, ndege,Richmond, BOT, sasa tunasikia na Bwana mkubwa na bibi yake mpenda pesa walikuwa wakifanyia biashara patakatifu pa patakatifu chini ya jahazi liitwalo ANBEN!
Kinachoumiza zaidi ni kwamba waliofanya uchafu huu ni wale wale waliofikishwa patakatifu pa patakatifu na Mwalimu mwenyewe! Kama ni usaliti basi huu ni mchafu kuliko hata ule wa Yesu na ndugu yake Yuda. Awamu ya tatu na inavyoonekana ya nne, ni awamu zitakazoingia kwenye historia kama awamu ya maanguko makubwa ya taifa letu.
Tutatoa sababu. Awamu ya kwanza maarufu kama ya ubinafsishaji, ilifanya kazi ya kuuza mali za umma kwa bei ya kutia mashaka wengine husema karibu na bure au tajiri kalewa. Baya zaidi wakati wananchi walipojaribu kuisaidia kwa kuionya hivyo sivyo walijibiwa kwa nyodo na matusi kibao!
Awamu ya tatu iliasisi urafiki na kujuana kutumika kama vigezo vya kuteuana. Hatuichukii au kuitwisha lawama kwa vile imeishafutika. Hasha. Nani alijua sababu za mtu aliyekuwa hafai kwenye cheo cha uwaziri mkuu kama waziri mkuu mstaafu kukalia kiti hicho pamoja na shutuma kwa miaka kumi? Sababu zilikuwa wazi kuwa alikuwa anafahamiana na Rais na isitoshe wake zao walikuwa wakitoka kabila moja. Huu ni upuuzi kiasi gani.
Ukiachana na kuteuana kwa kujuana, awamu ya tatu iliasisi mchezo unaoanza kuota mizizi wa kutawala kwa maneno badala ya vitendo. Mkapa alizoea kuiita awamu yake ya ukweli na uwazi wakati kimatendo ilikuwa ni uongo na ufichi. Rejea uongo wa mchana wa Mkapa kwenye mradi wa wakubwa wa kununua rada ambayo imetokea kuwa kashfa na donda kwa wananchi. Rejea ununuzi wa ndege mbovu lakini aghali ya Rais.
Sasa tuangalia hali ya sasa. Kwanza hakuna ubishi kuwa tangu awamu ya nne iingie imeingia na kashfa na kimtindo. Kwanza wakubwa hawakutangaza mali zao angalau tuweze kulinganisha wapi wameongeza na kwa nini na wapi wamepunguza ingawa kwa nchi ya bwerere kama Tanzania kupunguza hakupo.
Rejea kashfa ya Richmond ambayo pamoja na kuja na viini macho vya Taasisi ya Kukuza Rushwa ( TAKURU), bado watanzania wanajua kuwa wakubwa tena walioko kwenye ulaji mkubwa walivuta chao na kutuachia hilo shipa ambalo hata sasa hakuna anayejua kinachoendelea. Wao badala ya kutusuta na kutudanganya kama alivyokuwa akifanya Mkapa wameamua kuja na mtindo wa kuunda uchunguzi kiini macho na kusafishana!
Ukiachia Richmond, ANBEN, WAMA, EOTFL, kuna kashfa ya upotevu wa matrilioni kwenye wizara mbali mbali na hakuna mtu hata mmoja aliyekwishafikishwa mahakamani. Pia kuna hili baba lao la Benki kuu (BOT) ambapo vyombo vya habari vinasema kuwa ni kuanzia dola milioni 130 hadi 800 milioni! Jamani kwa ka nchi kama haka maskini hii siyo pesa ndogo. Lakini pamoja na ukubwa wa pesa hii nani anajali?
Maana kwa taarifa toka bungeni,serikali ilitaka hata kuwazuia wabunge wasijadili wizi huu? Hapa kwanini ka nchi kasinuke tena sana sana?
Kuna sakata la wakubwa kuuziana nyumba za watu wasio na nyumba. Nani anajali kutoa majibu? Hapa kwanini ka nchi kasinuke?
Kuna hili baba lao jingine. Madawa ya kulevya. Watu mbali mbali wamemtaka Rais aweke wazi kama anayo majina ya vigogo wa mihadharati awataje na kama hana aseme. Lakini mtukufu kaamua kuuminya! Juzi juzi alipokufa Amina Chifupa ambaye inasemekana alikuwa akipambana na madawa hayo, ndipo tunasikia tena nadhiri mpya! Hapa kwanini ka nchi kasinuke? Mpaka watu wenu waanze kufa ndipo mtasikia na kufanya mambo ya maana badala ya "rongo rongo" uchwara!
Ukirejea kwenye kupeana vyeo, hapo ndipo utashika kichwa na kujiinamia kama umepigwa ngumi ya tumbo. Nani mtu mwenye akili alitegemea mtu kama Lowassa anayejulikana kwa tamaa zake angekuwa waziri mkuu wa nchi? Ama kweli Kikwte kajua kutuchoka na kututumia!
Serikali licha ya kuwa kubwa, imejaa marafiki na watu wenye rekodi mbaya sana za kila aina ya ujambazi kwenye ofisi za umma.. Safu hii siyo ya kwanza kuliongelea suala hili. Hili limegeuka wimbo kutaka serikali ipunguzwe. Nani anasikia? Kwanini ka nchi kasinuke?
Kwa machache hayo katika mengi, tuhitimishe kusema kuwa nchi yetu isiposafishwa itaoza na kumongonyoka na kupotea. Viongozi waanze kujenga utamaduni wa kuwasikiliza wananchi badala ya kuwaburuza na kuendelea kufanya makosa. Wahusika watoe majibu yenye mantiki tena kwa wakati badala ya kunyamaza. Maana hilo siyo jibu. Nchi yetu inanuka sana sasa. Kila tunapobadili uongozi tunazidi kuzama je ni kwanini?
Nchi imeanza kukosa hata maana. Wakati wakubwa wanashindana kuchuma na wageni hasa wa kihindi nao hawako nyuma. Wako nyuma yao. Maana kila uchafu unaofanyika serikalini nyuma yake lazima wawepo wahindi. Kwanini? Je wananchi wetu wataendelea kuwa mashahidi wa jinai hii. Chonde chonde ka nchi kananuka sana. Wahusika safisheni ka nchi. Na patakatifu pa patakatifu pasigeuzwe patakakitu pa patakakitu.
Tuonane wiki ijayo inshallah.