Mwanamke mzee Muisrael aliyeachiliwa huru na wapiganaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema alikirimiwa na kutendewa wema katika muda wa wiki mbili alipokuwa ameshikiliwa mateka na kundi hilo la wanamapambano wa Palestina.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Yocheved Lifshitz, ajuza wa miaka 85, amesema Hamas ilimpatia daktari wa kushughulikia afya yake na kufanya kila njia kuhakikisha anapata dawa zake.
Ameongeza kuwa wapiganaji wa Hamas walishughulikia pia mahitaji yake. Bi Lifshitz amesema: "tulikula mkate, jibini nyeupe na matango, kama wao."
Bi Kizee huyo Muisrael ameendelea kusimulia alivyokirimiwa na wanamuqawama wa Palestina akisema: "walituambia wanaiamini Qur'ani na kwa hivyo hawatatudhuru".
Alipoulizwa kwa nini alipeana mkono na mmoja wa wanachama wa Hamas wakati wa kuachiliwa kwake, Bi Lifshitz alisema kwa sababu "walliamiliana nasi kwa wema na walishughulikia mahitaji yetu yote."
Jumatatu usiku, tawi la kijeshi la Hamas la Brigedi za Al Qassam lilitangaza kuwa limewaachilia huru mateka wawili wa Israel - Yocheved Lifshitz na Nurit Cooper mwenye umri wa 79 - kwa "sababu za ubinadamu."