Mateka aisifu Hamas

Mateka aisifu Hamas

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Mwanamke mzee Muisrael aliyeachiliwa huru na wapiganaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema alikirimiwa na kutendewa wema katika muda wa wiki mbili alipokuwa ameshikiliwa mateka na kundi hilo la wanamapambano wa Palestina.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Yocheved Lifshitz, ajuza wa miaka 85, amesema Hamas ilimpatia daktari wa kushughulikia afya yake na kufanya kila njia kuhakikisha anapata dawa zake.

Ameongeza kuwa wapiganaji wa Hamas walishughulikia pia mahitaji yake. Bi Lifshitz amesema: "tulikula mkate, jibini nyeupe na matango, kama wao."

Bi Kizee huyo Muisrael ameendelea kusimulia alivyokirimiwa na wanamuqawama wa Palestina akisema: "walituambia wanaiamini Qur'ani na kwa hivyo hawatatudhuru".

Alipoulizwa kwa nini alipeana mkono na mmoja wa wanachama wa Hamas wakati wa kuachiliwa kwake, Bi Lifshitz alisema kwa sababu "walliamiliana nasi kwa wema na walishughulikia mahitaji yetu yote."

Jumatatu usiku, tawi la kijeshi la Hamas la Brigedi za Al Qassam lilitangaza kuwa limewaachilia huru mateka wawili wa Israel - Yocheved Lifshitz na Nurit Cooper mwenye umri wa 79 - kwa "sababu za ubinadamu."
 
Aisee Wayahudi wamemmaindi kichizi huyo mama.

Nimetembelea Website ya Waisrael wanalaumu kuwa kwa nini Serikali haikumanage situation kabla huyo mama hajaongea na vyombo vya habari.
mtando huu hapa: Why did Israel allow a public diplomacy disaster?

Hata Sky news wamenukuu maneno ya huyo mama , wamendika hivi

1698173473066.png
 
Hivi ndivo mtume alivyosema
Na HAMAS wamefanya kwa vitendoView attachment 2791701
Ni sahihi, wameufanya uislam wenyewe kabisa, kwa mafunzo ya mtume. Sio mijitu inafanya hovyo hovyo, inachinja watu wasio na hatia huku ikitaja jina la allah, jitu linaemda kujilipua, linaua watu hawana hatia, wanaupaka matope uislam
 
Kumteka kikongwe kama huyo tu ni ugaidi na ndio tushuhudie wale wanaosema vikundi kama Hamas ni vikundi vya kigaidi sio waongo.

Na huyo kikongwe kwenye mahojiano alisema wakati wa kutekwa alipewa kipigo pamoja na kuporwa mkufu wake na watekaji taarifa ambayo mleta mada kwa sababu za kiimani hajaongelea kabisa.

Kama wewe kweli ni muungwana na mwenye kumuogopa Mungu kiukweli bila unafiki huwezi kabisa kufanya vitendo vya kigaidi kama kuteka watu sanasana unatakiwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto zako kwa maombi zaidi.
 
Inaruhusiwa kuteka kwa nia na madhumuni mazuri
 
Hamas wanatafuta kudanganya dunia kwamba wao ni watu wema,na wana utu na wanajali wazee na watoto ,kitu ambacho si kweli hii ni propaganda ya kutaka kuhadaa dunia kwa upuuzi wao .Shambulio walilofanya October 7 ni lakulaaniwa na mtu yeyote anayejali uhai wa na utu wa binadamu.
 
Kumteka kikongwe kama huyo tu ni ugaidi na ndio tushuhudie wale wanaosema vikundi kama Hamas ni vikundi vya kigaidi sio waongo.

Na huyo kikongwe kwenye mahojiano alisema wakati wa kutekwa alipewa kipigo pamoja na kuporwa mkufu wake na watekaji taarifa ambayo mleta mada kwa sababu za kiimani hajaongelea kabisa.

Kama wewe kweli ni muungwana na mwenye kumuogopa Mungu kiukweli bila unafiki huwezi kabisa kufanya vitendo vya kigaidi kama kuteka watu sanasana unatakiwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto zako kwa maombi zaidi.
Hawa wanaoua watoto kwa miaka 50 sasa tuwaite nani? Waliovamia iraq bila ya sababu na kuua mamilioni ya watu tuwaite nani? Mamilioni ya watu wameuliwa na magharibi hadi babu zako huku africa bila ya sababu, waliopiga bomu la hiroshima hadi wakaharibu vizazi kwa mamilioni waitwe nani? Na huyo mzee wako aliyetekwa amewasifia hao hamas publicly hadi wazungu wanaona aibu na wamekata hii clip hata sky news
 
Kwa hiyo mtume alifundisha hamas wateke, kubaka na kuua raia kwa madhumuni mazuri?!!!
Toa ushaidi mateka alibakwa au kuuliwa na Hamas. Mmetumia nguvu nyingi sana kukaririsha watu kuwa Hamas ni watu wa ovyo kwa stori nyingi zisizokuwa na ushaidi. Sasa angalia m/mungu jinsi anavyotisha. Mnawasafisha Hamasi wenyewe bila shuruti
 
Back
Top Bottom