Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
Palikuwa na mfanyabiashara mmoja mashuhuri, mwenye busara na maarifa ya kipekee katika biashara. Siku moja, alipanga safari ya kwenda nchi ya mbali kwa muda usiojulikana. Kabla ya kuondoka, aliwaita watumishi wake wa karibu , watu aliowategemea kwa uaminifu na uwezo wao wa kiutendaji.
Kwa kila mmoja, aliwapa sehemu ya mali yake kulingana na uwezo wake wa kiakili na wa kiutendaji,
Mwenzake, aliyepokea milioni mbili, naye hakubweteka. Alitumia busara na bidii yake kuikuza, na ndani ya muda alizalisha faida ya milioni mbili zaidi.
Lakini wa mwisho, aliyepokea milioni moja, alitafakari sana. Hofu ikamjaa , hofu ya kupoteza, hofu ya kushindwa, hofu ya kulaumiwa. Badala ya kufanya jambo lolote la maana, alichimba shimo nyuma ya nyumba yake, akaificha ile hela ardhini. Akaendelea na maisha kana kwamba hakupokea chochote.
Miaka ikapita. Hatimaye, mfanyabiashara akarudi kutoka safari. Aliwaita watumishi wake kuwasikiliza na kutathmini alichowaachia. Yule wa kwanza alikuja mbele kwa ujasiri, akasema,!
"Bwana, uliniamini kwa milioni tano. Nimezifanyia kazi, na sasa nazirudisha pamoja na nyingine tano."
Mfanyabiashara akatabasamu,akasema,
"Hongera! Umeonyesha uaminifu kwa kidogo, sasa nitakuaminisha na mambo makubwa zaidi. Karibu kwenye furaha ya bwana wako."
Wa pili naye akaja, akasema,!
"Bwana, milioni mbili ulizonikabidhi nimezizalisha, sasa ni nne."
Mfanyabiashara akampongeza vilevile!
"Umefanya vizuri sana. Uaminifu wako unaonyesha kuwa uko tayari kwa majukumu makubwa zaidi."
Lakini yule wa mwisho alifika kwa mwendo wa polepole, uso wake umejaa huzuni na mashaka. Akasema kwa sauti ya kujitetea,
"Bwana, nilijua wewe ni mtu mkali, mwenye matarajio makubwa. Niliogopa sana kupoteza ulichonipa, kwa hiyo nikaamua kuihifadhi ardhini. Hii hapa, chukua yako, kama ulivyonikabidhi."
Mfanyabiashara akamwangalia kwa macho ya masikitiko na kusema,
"Wewe ni mtumishi mvivu na mwoga. Ulichagua njia rahisi , ya kukwepa jukumu. Laiti ungeiweka hata benki, ingeweza kuzaa kidogo. Kwa sababu hiyo, nitamnyang’anya hiyo milioni moja na kumpa yule aliyekuwa na kumi."
Kisha akaongeza kwa hekima!,
"Kwa maana mwenye nacho ataongezewa, mpaka azidi kuwa navyo; lakini asiye nacho, hata kile kidogo alicho nacho atanyang’anywa. Kwa sababu gani? Kwa sababu alikataa kutumia fursa aliyokuwa nayo."
Mafundisho tunayopata hapa leo :
Kama ilivyo kwa wale watumishi, kila mtu anapewa vipaji, nafasi, au rasilimali kulingana na uwezo wake. Haijalishi ni kidogo kiasi gani cha msingi ni jinsi tunavyovitumia. Hatufanani katika kile tulichopewa, lakini sote tuna wajibu wa kukiendeleza.
Usilalamike kwa ulichonacho; angalia jinsi ya kukikuza.
Wale waliotumia walichopewa kwa uaminifu walizawadiwa zaidi, wale wanaofanya kazi kwa bidii na kuonyesha uwajibikaji huaminiwa zaidi na kupewa nafasi kubwa za mafanikio.
Kuwa mwaminifu kwa kidogo, utapewa makubwa.
Mtumishi wa mwisho alishindwa si kwa sababu hakuwa na uwezo, bali kwa sababu aliruhusu hofu imtawale. Hofu ya kushindwa ilimzuia kuchukua hatua yoyote ya maana,changamoto tunayokutana nayo wengi wetu,tunapoogopa kupoteza, tunaishia kupoteza zaidi kwa kutofanya chochote.
Kuchelewa kwa sababu ya woga ni kushindwa kabla ya kuanza.
Mfanyabiashara aliponyang’anya yule wa mwisho kile alichopewa na kumpa aliyefanikiwa zaidi, alifundisha somo kwamba fursa huendelea kwa wale wanaothubutu. Dunia haimsubiri yule asiye tayari kutumia nafasi.
🌱 Fursa haifai kwa yule anayeihifadhi tu, bali kwa anayeikuza.

- Wa kwanza akapewa milioni tano.
- Wa pili akapewa milioni mbili.
- Na wa tatu, milioni moja tu.