Uchaguzi 2020 Mathematically, haiwezekani kwamba Magufuli ameshinda kwa kura bandia!

Uchaguzi 2020 Mathematically, haiwezekani kwamba Magufuli ameshinda kwa kura bandia!

Ni mjinga peke yake atakayeelewa kilichofanyika.ila kwavile nyie ndio wenye nchi na mmeamua iwe hivyo ngoja tuone mwisho wenu.
 
Kuna waliosema safari hii wamedhibiti wizi aina Yoyote niliwaamini sana,
Ccm hawana huruma hata kidogo,
Wanapiga ngumi bila kupumzika.
 
Kuna scenario nyingi ila mojawapo ni kuwa kila kituo kilikuwa na kura zake prefilled already na walichofanya ni kureplace kabisa na zile kura zoote zilizopigwa kwenye vituo husika. Basically hakukuwa na uchaguzi.

Na hili liliwezekana tu kwa kuwa vituo vingi CHADEMA hawakuweka mawakala kabisa (poor organisation na/ama ukosefu wa fedha), au mawakala walizuiwa kuingia ndani, au mawakala walitolewa nje wakati wa majumuisho au mawakala wa CHADEMA walitishwa na kuhongwa fedha au mawakala walikuwa dhaifu sana (low reasoning capacity) na wakatii kinachofanyika bila kuhoji

Kuna mengi ya kujifunza ila hakuna haja ya Upinzani kushiriki tena chaguzi kwa matumaini ya kuambulia viti vichache ili Ruzuku kiduchu ipatikane
Mkuu kula bia nitalipa. Watu hawalielewi hili. Kula zote mbunge na raisi sio zile zilizopigwa ni zile zilikuwa drafted tayari. Huu ni wizi wa kijinga kuwahi kutokea. Iba weka margin hata ya 3k kwa mbunge. Sasa mbunge anapata 120,00 vs 3,000 raisi 360, 00 vs 1000. Hawa usalama ni utopolo kabisa
 
To cut to the chase, Lissu kapata kura ambazo hazifiki hata 2 million. Kama Lissu ni mshindi, maana yake Magufuli amejaziwa kura za bandia zaidi ya 10 million. Registered voters ni chini ya 30 million. No one knew before the fact what the voter turnout would look like.

Magufuli angejaziwa kura za bandia 10 million halafu turnout ikawa 25 million na Lissu akapata kura hata 15 million tu, fraud scheme ingepasuka kwa aibu kubwa. Nani atafanya kosa kama hilo?

Alternatively, kama kura halali za Magufuli ni chache kuliko za Lissu, maana yake voter turnout haikufika hata 4 million. This too doesn’t make any sense!

The only way to argue that Lissu won is to show that some of Lissu’s votes were thrown out or counted as Magufuli’s.

Ushauri wa bure kwa wafuasi wa Chama Cha Demokrasia ya Maendeleo (Chadema): Katika kuchangia, tambueni kuwa matusi sio substitute ya nguvu ya hoja; jengeni hoja mshawishi watu.

Jibu:
Kabla ya uchaguzi tulikuwa tunajua au tume ilikuwa inajua kwamba kura zitapigwa takribani 30 Million. Sasa kama tunataka kuweka kura bandia, tunaweza kupunguza kura kadhaa kutoka kwa jamii. Kuna njia nyingi tu, hizi mbili ni moja wapo.

Namna moja wapo ya kupunguza kura, tunaweza kuweka majina tofauti ya wapiga kura, kwa mfano unaitwa Juma Alhaji, tunaweza kuandika kwa makusudi Juma Halhaji. Pili, tunaweza kuchanganya majina na vituo, kwa mfano, unatakiwa kupiga kituo cha Mwembe chai, tunatuma jina lako Ukonga. Kwa mfano, tukiweza kuchanganya au kuaribu watu mia kwa kila jimbo, tunaweza kupata Kura 8M(80,155 vutuo vya kupiga kura x kura zilizo haribika) Tanzania nzima.
Kuna hesabu pia, unaweza kupiga kujua ni kiasi gani watu watapiga kura kutokana na sensa ya nyuma. kama unataka hizo hesabu ninaweza pia kuonesha hapa.

Magufuli angejaziwa kura za bandia 10 million halafu turnout ikawa 25 million na Lissu akapata kura hata 15 million tu, fraud scheme ingepasuka kwa aibu kubwa. Nani atafanya kosa kama hilo?

Jibu:
Sio rahisi kura kuzidi, ukitumia Hesabu na strategy vizuri. Hata mimi nashangaa sana kura kuzidi kwa bahadhi ya vituo, nadhani ni uzembe! Nimezungumzia hii kwa ufupi hapo juu .

Alternatively, kama kura halali za Magufuli ni chache kuliko za Lissu, maana yake voter turnout haikufika hata 4 million. This too doesn’t make any sense!

Jibu:
Inaweza kuwa baadhi ya kura toka upande wa pili zimepelekwa upande mwingine. Kuna namna ya kufanya hili zoezi.

The only way to argue that Lissu won is to show that some of Lissu’s votes were thrown out or counted as Magufuli’s.

Jibu:
Sio rahisi kuonesha hivyo, maana wamesha changanya kura, pia hii sio " kipimo bora" kwenye tatizo kama hili. Hii ni kwasabu, upande wa pili wana lalamika baadhi ya wasimamizi wao walizuiwa na wengine kutekwa.

Kwenye tatizo kama hili, njia ya kufanya kujua ukweli, ni kutafuta kituo ambacho kulikuwa na security camera. Tunaweza kuhesabu watu walio ingia kupiga kura na kuowanisha na idadi ya kura zilizo patikana kwenye hicho kituo. Kama idadi ya watu kwenye line ikiwa ndogo kuliko idadi ya kura, basi tunaweza kusema kulikuwa na wizi.

Ubarikiwe
 
Magufuli baada ya kuumbuliwa madhambi yake yote kwenye kampeni akaapa kufa na wapinzani na ndio akafanya hayo aliyoyafanya.

Magufuli ni mtu wa visasi sana na hilo halina ubishi wowote, he is of the vengeful character.

Hayo matokeo yaliyotangazwa na hako ka tume nani anaweza kuyathibitisha kwa sababu yalianza kupikwa toka vituoni hadi kwenye makao makuu ya hiyo tume na mlolongo mzima ni ccm tupu.

Hayo matokeo ndio Magufuli alivyopanga na kuwakabidhi tume wayatangaze hivyo yalivyo na hayo mahesabu anayoleta huyu mleta mada yanaonyesha tu alivyo mbumbumbu.
 
To cut to the chase, Lissu kapata kura ambazo hazifiki hata 2 million. Kama Lissu ni mshindi, maana yake Magufuli amejaziwa kura za bandia zaidi ya 10 million. Registered voters ni chini ya 30 million. No one knew before the fact what the voter turnout would look like.

Magufuli angejaziwa kura za bandia 10 million halafu turnout ikawa 25 million na Lissu akapata kura hata 15 million tu, fraud scheme ingepasuka kwa aibu kubwa. Nani atafanya kosa kama hilo?

Alternatively, kama kura halali za Magufuli ni chache kuliko za Lissu, maana yake voter turnout haikufika hata 4 million. This too doesn’t make any sense!

The only way to argue that Lissu won is to show that some of Lissu’s votes were thrown out or counted as Magufuli’s.

Ushauri wa bure kwa wafuasi wa Chama Cha Demokrasia ya Maendeleo (Chadema): Katika kuchangia, tambueni kuwa matusi sio substitute ya nguvu ya hoja; jengeni hoja mshawishi watu.
umeandika utumbo ......
 
Ulikwenda vizuri na mada yako huko juu, ambako mtu angekaa chini na kujadili vizuri wazo lako hilo.

Haya ya mwisho kwa nini uliyaona kuwa muhimu hadi uyaweke kwenye mada inayojadilika?

Njia mbalimbali zimetumiwa na serikali, ndio, serikali na sio CCM kuvuruga uchaguzi. Hilo tu linatosha kuifanya hiyo "Mathematically" yako kutokuwa na maana yoyote katika matokeo haya.

Unajaza manamba ya hovyohovyo kwenye 'program' halafu unatarajia upate jibu sahihi katika matokeo? Wewe ni 'mathematician' wa aina gani aiseee!

Mkuu, I am having hard time understanding what you’re trying to convey. Your argument appears to be a combination of some new unsubstantiated election fraud claims and a programming GIGO rhetoric.

Jaribu kufafanua na kuwa more specific tukuelewe!
 
Hapo peke yake umeonesha una uwezo mdogo sana wa kufanya analysis manake umeangalia upande mmoja wa "kujaza" na sio upande wa "kupora"!

Umeshindwa kufahamu kama inawezekana Jiwe kujaziwa kura bandia zaidi ya 10 million basi pia inawezekana Tundu Lissu kuporwa kura zaidi ya 10 million!

But to make it logical, kwavile jumla ya kura za Jiwe na TL ni almost 15 Million, hapakuwa na haja ya kumwekea Jiwe kura za bandia zaidi ya 10 Million bali all you need to do ni kuiba kura 5M za TL na kuzihesabia upande wa Jiwe, kisha unaongoza zingine fake kwa Jiwe, na end result itakuwa Jiwe kapata kura zaidi 12M na TL roughly 2M na finally kuonesha hoja yako kwamba zingefika kura 25M ni hoja inayothibitisha uwezo wako mdogo wa kuchambua mambo!!

Najua yupo Lofa atakayeuliza unaiba vipi zaidi ya kura 5M! Kama hilo ndo swali lako, kamuulize Jecha aliiba vipi kura zoooooooote na kufuta matokeo ya uchaguzi!

Umefikia argument hiyo kwa sababu mawazo yako yaliganda kwenye kura za bandia za kwenye mabox bandia bila kuelezea uwezekano wa wa kura za X kuhesabiwa upande Y hasa kwa vituo kadhaa ambavyo havikuwa na mawakala wa upinzani!

That being said, hoja yako HAINA MASHIKO!!!

Wewe kama una uwezo wa kusoma na kuelewa, nikushauri usome tena kwa makini nilichoandika kisha upitie tena andiko lako.

If you have a comprehension issue, I am afraid, we may not be able to extend a helping hand here!
 
Narudia, una uwezo mdogo sana wa kuchambua mambo!! Kwani ni nani aliyekudanganya kura zinaibiwa kwa option ya kutumia kura fake peke yake?!

Lakini kwa upande mwingine, hata ukitumia Kijerumani au Kigiriki bado haiwezi kufanya hoja zako ziwe na mashiko manake nimeona kila anayekuonesha kwamba ulichoandika ni upoyoyo baso lazima umpigie Kimalkia 🤣 😆😆😀😂😂!!!
 
Nilikuwa wakala wa kusimamia kura.ni mjinga tu pekee ndio haamini kama magufuri aliongezewa kura.narudia tena .ni mjinga tu pekee ndio anaamini magufuri napata kura 12 million kwa halali

Uzuri wa jukwaa hili hata kenge anaweza kujaribu kuwaaminisha viumbe wengine kuwa yeye ni mamba!
 
Vipi kama kura hazikuhesabiwa bali kulikuwa na matokea tayari? Hakuna lisilowezekana ikiwemo la JPM kushinda kweli
 
To cut to the chase, Lissu kapata kura ambazo hazifiki hata 2 million. Kama Lissu ni mshindi, maana yake Magufuli amejaziwa kura za bandia zaidi ya 10 million. Registered voters ni chini ya 30 million. No one knew before the fact what the voter turnout would look like.

Magufuli angejaziwa kura za bandia 10 million halafu turnout ikawa 25 million na Lissu akapata kura hata 15 million tu, fraud scheme ingepasuka kwa aibu kubwa. Nani atafanya kosa kama hilo?

Alternatively, kama kura halali za Magufuli ni chache kuliko za Lissu, maana yake voter turnout haikufika hata 4 million. This too doesn’t make any sense!

The only way to argue that Lissu won is to show that some of Lissu’s votes were thrown out or counted as Magufuli’s.

Ushauri wa bure kwa wafuasi wa Chama Cha Demokrasia ya Maendeleo (Chadema): Katika kuchangia, tambueni kuwa matusi sio substitute ya nguvu ya hoja; jengeni hoja mshawishi watu.
Msimamizi mmoja ananiambia kuwa kapiga kura zaidi ya mia mbili yeye pekee yake.
 
Back
Top Bottom