Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

-bwa ha ha ha ha sasa hivi FMES anakuja......mzee malecela kama ni mtindo wa nywele basi ni afro.....kapitwa na wakati.....

FMES Aliaga kwamba anakwenda kupumzika!!! sijui kwa kazi gani...
 
Naona small towns za Tz kumekucha. Hongereni Chadema. Naanza kuamini kwamba mwisho wa enzi umekaribia.


heheheheheh kwa hiyo ya Biharamuro tuuu mkuu!!!!!!!!!

Anyway Hongera Chadema
 
Huenda Ole Sendeka na Mpendazoe wamefurahia sana sana.
 
achana na huyo kaona misalaba kwenye avatar yako kimemkera.....
anyway
hivi mmegundua hata wana CCM wenyewe hawaipendi CCM?am sure masatu kafurahia ushindi wa CHADEMA

Hahaaaa imetulia hiii,

Ila nina uhakika wengi ndani ya CCM watakuwa wamefurahia CCM kudondokea pua, hasa wale ambao hawakufurahishwa na uongo wa kunganganiza mtu asiye raia kugombea! well kule wasubi huwa wana msemo wao hivi

''Bhasubi twimanye''
 
Hivi zile 'breaking news' za Mwananchi zinafanya vipi kazi? zimekosa sponsor?
 
Mkandara,
Lakini hii ya Biharamulo naona ilikuwa tofauti kidogo maana hata hao wapinzani wengine hawajapata kura kabisa kwahiyo issue ya kugawana kura hapa haikuwepo. Na kumbuka vyama vyote vyenye majina i.e TLP na CUF walisimamisha wagombea.
Alaaa! basi makosa yangu inabidi nianze kuamini uwezo wa Chadema kusimama pekee, kumbe CUF na NCCR-Mageuzi pia walisimamisha wagombea?..
Heee, Imekuwaje hawana hata asilimia moja!
 
Hongereni Chadema ! Nampa pole msimamizi wa uchaguzi Biharamulo kwa kupoteza kazi kulingana na tamko la Makamba. Shame on you Judge Lewis Makame kwa kushindwa kusoma alama za nyakati - what a pity !!
 
Alaaa! basi makosa yangu inabidi nianze kuamini uwezo wa Chadema kusimama pekee, kumbe CUF na NCCR-Mageuzi pia walisimamisha wagombea?..
Heee, Imekuwaje hawana hata asilimia moja!

Ni aibu mkuu wangu. Chadema ilipata kama 50% na ushee na CCM 49% na ushee. Ni kama vile vyama vingine havikuwepo. Vimegamana chini ya 1%. TLP walikuwepo na hata mzee mzima CUF alikuwepo.
 
Alaaa! basi makosa yangu inabidi nianze kuamini uwezo wa Chadema kusimama pekee, kumbe CUF na NCCR-Mageuzi pia walisimamisha wagombea?..
Heee, Imekuwaje hawana hata asilimia moja!

labda wamepata asilimia zero point ........ Hihiiii ina maana hata ndugu zao hawakuwapigia kura? Mhhh, huwezi shangaa sana maana kama wa mbali hawakupi kwa kufahamu ubovu wako, basi wa karibu ndiyo kabisaaa
 
Malecela is no longer a factor. Ana malizia tu muda wake kwenye siasa but he has no where else to go in terms of power and influence. Mzee anatakiwa apumzike.
 
malecela is no longer a factor. Ana malizia tu muda wake kwenye siasa but he has no where else to go in terms of power and influence. Mzee anatakiwa apumzike.


true.... He would earn more respect if he does the msuya stuff
 
Malacela should now know that CRIME DOESN'T PAY!
 
Ni aibu mkuu wangu. Chadema ilipata kama 50% na ushee na CCM 49% na ushee. Ni kama vile vyama vingine havikuwepo. Vimegamana chini ya 1%. TLP walikuwepo na hata mzee mzima CUF alikuwepo.

Mkuu CUF nadhani hawakusimamisha mgombea ila walimuungamkono wa TLP pamoja na NCCR ambapo kwa ujumla vyama hivyo ndo tuseme vimepata kura 184?

Ila hiyo 49% ya CCM lazima ni chini ya hapo, kumbuka hapa mtoa data alisha sema ameshuhudia watu wengi wasio jua kusoma na kuandika, ambao wamefika bila watu wao, na hivo kuwa wanatapeliwa kura zao.. kwahiyo hapo kuna kura kibao tu zitakuwa zimepotea kwa njia hiyo.

Lakini pia kuna milioni 60 ambayo pia tumeambiwa iligawiwa jana kama njugu kwa wajumbe wa nyumba kumi kumi..

Ila nilicho furahi, mtoa data kasema kweli kwamba wana B'mlo pesa watachukua, fulana watavaa kura wanajua wa kumpa!

natamani watanzania wote tungejifunza toka kwa ndugu zetu hawa, ili hawa wanao kuja na visenti wakati wa uchaguzi tuna vilamba lakini kura hatuwapi!
 
Tatizo viongozi wetu sijui ni tamaa. I'm sure mzee anapesa za kutosha tu lakini sijui bado anatafuta nini. What's the point of doing something where you can no longer progress forward? Yeye the only thing he had left to look forwad to ni huo uraisi & there is no chance in hell that will ever happen.
 
Sina kadi ya chama chochote cha siasa na wala sihitaji. Lakini ukweli ni kuwa VICHWA vilivyoko CHADEMA ni noma.

Kama CCM wanataka kutawala nchi hii muda mrefu lazima waache fix-uchwara za kuvalisha watu flana za kijani na kutengeneza wheel-cover zenye maandishi ya "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania" wakati ukweli ni kuwa CCM wamejenga matabaka ya matajiri na masikini katika nchi hii. Vinginevyo siku zao (CCM) zinahesabika!!!

Tunachoomba tu ndugu zetu wa Kijani-Njano, siku mkilala mumepigwa mwereke, musituletee vita. Hatutaki vita sisi.
 
Ni kweli CCM ilishinda chaguzi ndogo za Kiteto, Busanda, na Mbeya Vijijini. Pamoja na huo ushindi kitu kilichokuwa wazi ni kwamba CHADEMA walionyesha ushindani wa kuitoa jasho CCM.

Tukumbuke kwamba CCM ilikuwa inasaidiwa na NEC, Polisi na kutumia resources za umma kwenye kampeni. Kuna mawaziri waliacha ofisi wakaenda kusaidia kupiga kampeni wakitumia magari ya serikali. Kuna cases nyingi za jinai zilikuwa reported na hakuna kilichofanyika mpaka leo. Mfano, Kiteto akina Mtalemwa na wenzake walipigwa sana lakini polisi hawakufanya kitu. Kule Busanda kuna viongozi wa serikali za mitaa walikamatwa wakinunua shahada, mpaka leo hakuna kitu. Kuna magari yalionekana yakipakua magodoro kule Busanda NEC na Polisi hawakufanya chochote.

Kwa tathimini yangu hilo gap dogo la kura ni dalili nzuri kwa CHADEMA kwamba wakiweka wagombea wazuri na wakatumia vyema poor resources walizonazo, wanaweza kushinda viti vingi uchaguzi ujao wa 2010. Uchaguzi wa mwakani kutakuwa hakuna kusaidiana, kila mmoja anapambana kivyake jimboni kwake. Hao mawaziri kila mmoja atakuwa jimboni kwake akipiga kelele kivyake na Polisi hawatamwagwa wengi kwenye jimbo kama ilivyo sasa kwamba uchaguzi mdogo ukija Polisi wanamwagwa sehemu moja na hivyo kuongeza woga na sometimes hutumika kwa manufaa ya CCM.
 

Asante kwa kunishahihisha mkuu. Mimi nadhani sasa vyama ni CCM na Chadema tu, but I could be wrong. Kuna vyama vitaanza kufa a natural death. Ila big up kwa wana b'mulo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…