Alaaa! basi makosa yangu inabidi nianze kuamini uwezo wa Chadema kusimama pekee, kumbe CUF na NCCR-Mageuzi pia walisimamisha wagombea?..
Heee, Imekuwaje hawana hata asilimia moja!
Ni kweli CCM ilishinda chaguzi ndogo za Kiteto, Busanda, na Mbeya Vijijini. Pamoja na huo ushindi kitu kilichokuwa wazi ni kwamba CHADEMA walionyesha ushindani wa kuitoa jasho CCM.
Tukumbuke kwamba CCM ilikuwa inasaidiwa na NEC, Polisi na kutumia resources za umma kwenye kampeni. Kuna mawaziri waliacha ofisi wakaenda kusaidia kupiga kampeni wakitumia magari ya serikali. Kuna cases nyingi za jinai zilikuwa reported na hakuna kilichofanyika mpaka leo. Mfano, Kiteto akina Mtalemwa na wenzake walipigwa sana lakini polisi hawakufanya kitu. Kule Busanda kuna viongozi wa serikali za mitaa walikamatwa wakinunua shahada, mpaka leo hakuna kitu. Kuna magari yalionekana yakipakua magodoro kule Busanda NEC na Polisi hawakufanya chochote.
Kwa tathimini yangu hilo gap dogo la kura ni dalili nzuri kwa CHADEMA kwamba wakiweka wagombea wazuri na wakatumia vyema poor resources walizonazo, wanaweza kushinda viti vingi uchaguzi ujao wa 2010. Uchaguzi wa mwakani kutakuwa hakuna kusaidiana, kila mmoja anapambana kivyake jimboni kwake. Hao mawaziri kila mmoja atakuwa jimboni kwake akipiga kelele kivyake na Polisi hawatamwagwa wengi kwenye jimbo kama ilivyo sasa kwamba uchaguzi mdogo ukija Polisi wanamwagwa sehemu moja na hivyo kuongeza woga na sometimes hutumika kwa manufaa ya CCM.
Hahaaaa imetulia hiii,
Ila nina uhakika wengi ndani ya CCM watakuwa wamefurahia CCM kudondokea pua, hasa wale ambao hawakufurahishwa na uongo wa kunganganiza mtu asiye raia kugombea! well kule wasubi huwa wana msemo wao hivi
''Bhasubi twimanye''
Duu hiyo niliyoitilia mkazo ndiyo siri ,CHADEMA wasifurahie sana huo ushindi ,Japo nawapa 5.
Wasubi huwa mara nyingi kama sio mara zote mtu mgeni kama siye musubi ni ngumu kushinda kule ,wale jamaa wanangalia mtu wao hawaangalii sana chama.
Nakumbuka vizuri MAGUFULI alibwagwa sana na marehemu Kabuye kwa msemo huo tu ulitosha sana kumutoa Magufuli nje ya ulingo,mpaka mwisho japo sina uhakika mpango ulifanyika kuligawa hilo jimbo ndiyo Pombe akapata kule.
Cha msingi hapa CHADEMA wanahaki ya kufurahia ushindi lakini pia waangalie kama wapinzania wao walikuwa wazawa ,bila hivyo mambo yanaweza badirika mwaka 2010 mpaka mkashindwa kuwaamini wasubi.
True, lakini 2010, Dr. mbassa si atatetea kiti chake? Kumbuka sasa hivi ataingia kwa nguvu na atakuwa anaanza kuonyesha ufanisi. kwahiyo mwakani kwake nadhani itakuwa rahisi zaidi!
Tatizo viongozi wetu sijui ni tamaa. I'm sure mzee anapesa za kutosha tu lakini sijui bado anatafuta nini. What's the point of doing something where you can no longer progress forward? Yeye the only thing he had left to look forwad to ni huo uraisi & there is no chance in hell that will ever happen.
Haa ha haaa ....inanikumbusha ile slogan ya mkewe wakati wakiutafuta urais...first lady anatoka Anna anaingia Anna.....
Safari hii CCM chali.
Tinga tinga limekuwa kibajaji?
Alaaa! basi makosa yangu inabidi nianze kuamini uwezo wa Chadema kusimama pekee, kumbe CUF na NCCR-Mageuzi pia walisimamisha wagombea?..
Heee, Imekuwaje hawana hata asilimia moja!
SISIEMU watasema wameshindwa Biharamulo kwa sababu watu wa huko wana fedha za kununua magazeti, wana umeme wa kuwawezesha kuangalia TV kujua ni nini kinaendelea nchini, hawahitaji vitisho vya kunyimwa vibali vya kuchimbia madini kama Busanda........ wewe subiri utasikia tu hizo spins.
Don't read too much into this. Local politics are not necessarily national politics. Kwa vile jimbo hilo tayari lilikuwa upinzani hivyo aliyeanguka zaidi si CCM bali TLP. Ndio maana ushindi wa Tarime pamoja na ukubwa wake wote ulitafsiri jambo moja tu nalo ni kurudisha jimbo mikononi mwa Chadema.
Hadi hivi sasa katika chaguzi hizi ndogo, Chadema haijaweza kushinda jimbo la CCM. Imeshindwa Tunduru, Kiteto, na Mbeya Vijijini. Na hii utaona tofauti kubwa ya jinsi gani CCM inapeleka nguvu zake. Huwezi kulinganisha jinsi CCM ilivyopania kuichukua Busanda na jinsi ilivyopandia kuichukua Biharamulo.
Jambo kubwa ambalo ni zoezi kwa chadema ni jinsi gani kuweza kushinda sasa kwenye majimbo ya CCM maana sasa hivi hakuna tena uchaguzi mdogo hadi uchaguzi mkuu mwakani.
Ninachokiona sasa ni CCM kuanza kujipanga kuyakomboa majimbo ya upinzani na kuyarudisha CCM.
Na suala la kuungana mimi nilishassema mapema, hakuna ulazima wa Chadema kuungana na chama kingine bali kujijenga ili kiweze kuwa chama mbadala na hili ni kweli kwa CUF vile vile. Endapo kutakuwa na ulazima wa kuungana basi ni muungano wenye kuunganisha fikra, sera, katiba, mitazamo n.k na siyo muungano wa kuiondoa CCM.
mwenyewe anajua. Nadhani sasa safari ya kurejea ccm itashika kasi