Uchaguzi 2020 Matokeo Rasmi ya Jumla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2020

Uchaguzi 2020 Matokeo Rasmi ya Jumla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2020

watu waporadhi kupoteza muda kwende kwenyemikutano kilasiku kipindi chote cha kampeni lakini muda mchache tu wakwenda kupiga kura hawaendi.
alafuwanakuja hapa kulalamika.
wabongo wengi unafiki ni hulka yetu.
 
Una kila haja ya kujua nguvu ya kura yako. Usiache kupiga kura kwa sababu mgombea wako ameshindwa.
kama kura yangu ingekuwa na nguvu kiasi hicho ningeshaona mabadiliko mda mrefu sana, sasa badala yake imekuwa kama najifurahisha tu hasa ya mwaka huu ndio nalaani sana kiasi chakuhisi nilipoteza sana mda wangu😠
 
MATOKEO RASMI YA JUMLA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 29,759,699

Wapiga kura waliojitokeza Kura ni 15,910,950

Idadi ya kura halali ni 14,830,195

Idadi ya Kura zilizokataliwa ni 261,755

Kura Walizopata Wagombea

Dkt John Pombe Magufuli wa CCM ni Kura - 12,516,252

Leopard Lucas Mahona NRA ni Kura 8787

John Paul Shibuda ADA- TADEA ni Kura 33,086

Muttamwega Mgaywa SAU ni Kura 14,922

Cecilia Augustino Mmanga (Demokrasia Makini) ni Kura 14,556

Maganja Yeremia Kurwa (NCCR) ni Kura 19,969

Lipumba Ibrahim Haruna (CUF) ni Kura 72,885

Philipo John Fumbo (DP) ni Kura 8,283

Membe Benard Kamillius(ACT) ni Kura 81,129

Queen Curthibert Sendiga (ADC) ni Kura 7627

Twalib Ibrahim Kadege (UPDP) ni kura 6194

Rungwe Hashim Spunda (CHAUMMA) ni Kura 32,878

Mazrui Alfan Mohamed (UMD) ni Kura 3721

Seif Maalim Seif (AAFP) ni Kura 4,635

Lissu Tundu Antiphas Mughwai (CHADEMA) ni Kura 1,933,271

ANGALIZO; Watanzania wenzangu TUJITAHIDI KUJUA UMUHIMU WA KUJITOKEZA NA KUPIGA KURA (NGUVU YA KURA YAKO). KUPIGA KURA NI MAAMUZI TOSHA YA KUCHAGUA MTU MWAMINIFU UNAYEMTAKA NA UNAYEMUAMINI ATAKAYESIMAMA KWA AJILI YA KUSIMAMIA MASLAHI MAPANA YA TAIFA.

KATIKA UTAFITI WA UCHAGUZI MWAKA HUU UNAONYESHA KWAMBA
Jumla ya watu Milioni 29,754,999 walijiandikisha kupiga kura

15,910950 Ni idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura
14,830195 Kura halali za wapiga kura
261755 Idadi ya kura Zilizoharibika

12,516,252 Ni idadi ya kura alizopata mgombea wa CCM yaani JPM

1,933,271 Ni idadi ya kura alizozipata mgombea wa CHADEMA yaani TL

Kuna haja pia ya kutoa elimu ya kujitokeza Kupiga kura kwa wananchi.

Kama walijiandikisha Million 29+

Na waliopiga kura ni million 15+

Ina maana kuna watu million 17 hawakupiga kura.

Hata kama kuna sababu kadhaa za watu kutojitokeza kama vifo, kuhama, masomo, vyuo kufungwa, kulazwa hospital, lakini idadi yao imekuwa kubwa sana.

Uchambuzi Mwingine Mfanano: Mwenendo wa Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020

Ni masaa takribani 48 tangu wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watimize haki na wajibu wao kikatiba, wa kuchagua viongozi wao katika ngazi ya kitaifa, jimbo na kata. Hatua ya upigaji kura ilikamilika tar 28 Oktoba mwendo wa saa kumi jioni na kupisha hatua za kuhesabu, kujumlisha kura pamoja na kutangaza matokeo katika ngazi ya urais, ubunge na udiwani nchi nzima.

Tume ya taifa ya uchaguzi - chombo chenye mamlaka kisheria kuratibu shughuli za uchaguzi - tayari imeanza kutoa matokeo ya awali ya kura kwa ngazi ya urais. Mpaka makala hii inapoandikwa leo - ambapo matokeo ya majimbo yote 264 yalikuwa yametangazwa na tume ya uchaguzi - Dk. John Pombe Magufuli, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi ameongoza kwa kupata 84.40% ya kura halali akifuatiwa na Tundu Antipas Lissu wa CHADEMA akiwa na 13.04%.

Matokeo haya yanashabihiana na matokeo ya tafiti huru mbali mbali mbali zilizofanyika kipindi cha kampeni kilichoanza mwezi Agosti na kukoma siku moja kabla ya kupiga kura. Moja ya tafiti hizi ni ile ya kurayamtandaoni.com ambayo ilikamilika huku Dk. John Pombe Magufuli akipata 80.8% akifuatiwa na Tundu Antipas Lissu wa CHADEMA akipata 13.6%. Kura hiyo ambayo ilikuwa wazi kwa mtu yeyote mtandaoni, ilishirikisha zaidi ya watu 47,000 ambayo ni sawa na sampuli ya takribani 1.6% ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura.

Taarifa mbalimbali za waangalizi rasmi wa uchaguzi huu zimechapishwa katika vyombo vya habari mashuhuri likiwemo shirika la habari la BBC ambalo limechapisha habari ya taarifa ya Ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki. Ujumbe huo ulioongozwa na rais wa zamani wa Burundi, Silvestre Ntibantunganya, umeshuhudia kuwa uchaguzi mkuu wa Tanzania ulifanyika kwa kufuata taratibu. Ndg. Ntibantungaya aligusia hali ya usalama katika maeneo mbalimbali, kampeni zilizofanyika kwa uhuru, uratibu wa weledi wa shughuli ya upigaji kura.

Ahsanteni sana mliojitokeza kupiga kura.

View attachment 1616252View attachment 1616254

Tumechagua maendeleo tunaenda na John Pombe Magufuli
 
Kuna haja gani kila miaka nikapige kura isiyo na impact yoyote kwa nchi yangu zaiɗi nakuwa kama najidanganya mwenyewe, mbona bora niache tu

Wenzako hawaelewi correlation kati ya kujiandikisha na kutokupiga kura vs kuheshimiwa uhuru wa kuchagua! Wao wanadhani tutajazana vituoni kama mazuzu wakati nguvu ya boksi la kura haiheshimiwi!

Nadhani mkuu unakumbuka awamu ya mwisho ya JK watu walivyoingia mitini na kuachana na kupiga kura, kama Taifa tusipofanya jambo kuna feedback tunawapa watoto wetu na tushingae heshima ya kupiga kura ikipotea!
 
Kwenye vita ya Uganda niliambiwa kuna watu walijitolea kwenda kupigana, je kwa Tz ya sasa kuna raia anaweza jitolea kweli?

Uzalendo wa nchi yetu uko wapi?
UKIWAONA HAWA KATIKA MAANDAMANO, ANDAMANA!!
---------------------------------

1. Ukimuona Dudley, mtoto wa kwanza na Freeman Mbowe na wadogo zake wakiongoza maandamano nawe andamana. Freeman Mbowe pekee hatoshi, yeye hawezi kupigwa risasi hata moja. Nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani nchini inamlinda, ni jicho la Dunia anatazamwa, hakuna risasi inayoweza kuelekezwa kwake hata moja. Pale Mkwajuni Kinondoni risasi ilimkwepa Mbowe ikamuua Akwiline Akwelina. Wazazi wake wanalia hadi sasa, hakuna kitu. Usipowaona watoto wa Freeman Mbowe usiandamane!!

2. Ukimuona Alicia Magabe na watoto wake wa damu andamana. Alicia ni mke wa Tundu Lissu ambae Urais wa Lissu unamhusu zaidi kuliko mimi na wewe. Ukimuona Tundu Lissu peke yake usidanganyike kuandamana. Lissu ndie aliegombea Urais kwa Chama kikuu cha upinzani akiungwa mkono na ACT Wazalendo, huyu ni icon ya uchaguzi, ndie mwanamkakati ktk maandano hayo. Dunia yote ipo kwake, akifa hakuna cha kujificha, mission INATIKI.

Hakuna Askari mpumbavu anaweza kulenga shabaha ktk mwili wa Lissu, risasi zitaelekezwa kwako. Utakufa na si ajabu usifahamike, taarifa zako hazitofika popote, utakufa kama Mbwa, utazikwa siku inayofuata ktk kabuli la futi mbili au usizikwe kabisa. Usipomuona Alicia na wanawe, usiandamane!!

3. Ukimuona Bi Fourtuna Salehe na Bi Aweina Sinani na watoto wao katika maandamano andamana. Hii ni familia ya Maalim Seif ambayo inasemwa kuwa imepelekwa Oman mafichoni tayari. Wanasema watu wameuawa Zanzibar lkn hakuna jina la mtoto wa Maalim Seif wala wa mtoto wa Jussa hata moja. Usiwe mjinga, hukuzaliwa kuwa chambo, hukuzaliwa kwa ajili ya Urais wa Maalim au Lissu. Wakiwa Marais wewe haitokusaidia chochote. Usipomuona mtoto wa Maalim Seif, wake zake na familia yake jilalie zako nyumbani hauna cha kupoteza.

4. Ukimuona Anna Bwana, Wiza na Josina ktk maandamano yaliyoitishwa na wewe ungana nao, andamana kwa moyo mkunjufu kabisa. Hii ni familia ya Zitto Kabwe, akiwa peke yake muache aendelee na kazi yake. Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Chama cha upinzani (KC), ni jicho la Dunia hawezi kupigwa risasi taratibu za kuzuia maandamano zinamtambua na kumlinda. Usipomuona mke wake, watoto na ndugu zake wengine achana na kazi hiyo haina faida itakupeleka kuzimu bure.

5. Ukimuona Askofu Bagonza na mkewe, na watoto wake wote ktk maandamano andamana. Akiwa peke yake muombee kwa Mungu, usijiunge nae. Ukimuona Lema na watoto wake, Sugu na mke wake na watoto zake, Msigwa na wadogo zake kutoka Iringa, Heche na mkewe na watoto wake andamana.
Ukiwaona wao peke yao usiandamane, Ubunge na Urais wao hauna maana yoyote kwako. Maisha yako ni ya kwako peke yako, pambana!!
#USIANDAMANE!!
 
N
Hisabati inaweza kuwa tatizo kubwa zaidi ya elimu ya uraia...
Ni kweli, lakini ndivyo utafiti unavyoonyesha. Ukweli utabaki kuwa pale pale kuna kila sababu za wanachi kuwa na mwamko wa kujitokeza na kupiga kura. Kura ina maamuzi makubwa sana.
 
Noma nomaaaa [emoji23][emoji23][emoji23]
EltZtB1W0AA1U4w.jpg


Sent from my G-PADLITE using JamiiForums mobile app
 
Hii ndiyo kauli ya ushindi, tutashangilia mwaka 2025 baada ya kutimiza ahadi zilizoahidiwa.

"Wabunge wateule, Wawakilishi wateule na wadiwani Wateule wa CCM tayari waaze kufanya uchambuzi wa ahadi zilizotolewa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar pamoja na Ilani ya CCM na mara moja waaze kufuatilia kero na Watengeneze utaratibu mzuri wa kufuatilia na kusikiliza kero za wananchi na kuzijibu"
Noma nomaaaa [emoji23][emoji23][emoji23]View attachment 1617005

Sent from my G-PADLITE using JamiiForums mobile app
 
CCM mmeshavuruga hata mkipanga vipi mahesabu na matukio hayakubaliani,mlikosea,mipango iliharibika maana mpaka leo makaratasi ya kura za ushindi wenu yamejaa barabarani.

Kama ni mimi basi ningepanga na hakuna aibu ingelitokea ,Tayari unaowapiga kura wa nchi nzima,tayari unaowaliojiandikisha kila kituo ,sasa mngelipanga matokeo ya wizi kwa idadi husika ya kituo ,kwa hivyo kusingekuweko na haya makosa ya wizi wa kihesabu uliotokea.
yaani hayo mafuko ya rambo mliojaza kura za wizi zingeliendana na kituo mnakolipeleka

Chukua kituo kimeandikisha wapiga kura 100, 90 mpeni magufuli 5 lisu na zingine waliobakia ,kwa vile mlizibiti vituo mifuko yenu ingekwenda kumiminwa tu wakati kura za waliokuja mnaziweka pembeni kiaina.Kwa hivyo kura zitaendana na idadi ya kituo,lakini mnachukuwa watu mnawapa karatasi za kura mara kumikumi ,mtu anajaza anakuja kutumbukiza,lazima idadi itapita ya waliojiandikisha kituoni.

Msijifanyie mambo ulizeni kwanza,mnaona sasa aibu iliyowakuta kama mimi ndio Magufuli tume yote naikata vichwa,wameniabisha.
 
Hii ndiyo kauli ya ushindi, tutashangilia mwaka 2025 baada ya kutimiza ahadi zilizoahidiwa.

"Wabunge wateule, Wawakilishi wateule na wadiwani Wateule wa CCM tayari waaze kufanya uchambuzi wa ahadi zilizotolewa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar pamoja na Ilani ya CCM na mara moja waaze kufuatilia kero na Watengeneze utaratibu mzuri wa kufuatilia na kusikiliza kero za wananchi na kuzijibu"
Ahadi ni moja tu, Tanzania iwe kama ulaya [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my G-PADLITE using JamiiForums mobile app
 
Wagombea urais wale wanawake wawili hasa yule anayesuka nywele anastahili kupewa nyadhifa fulani...
 
CCM mmeshavuruga hata mkipanga vipi mahesabu na matukio hayakubaliani,mlikosea,mipango iliharibika maana mpaka leo makaratasi ya kura za ushindi wenu yamejaa barabarani.

Kama ni mimi basi ningepanga na hakuna aibu ingelitokea ,Tayari unaowapiga kura wa nchi nzima,tayari unaowaliojiandikisha kila kituo ,sasa mngelipanga matokeo ya wizi kwa idadi husika ya kituo ,kwa hivyo kusingekuweko na haya makosa ya wizi wa kihesabu uliotokea.
yaani hayo mafuko ya rambo mliojaza kura za wizi zingeliendana na kituo mnakolipeleka

Chukua kituo kimeandikisha wapiga kura 100, 90 mpeni magufuli 5 lisu na zingine waliobakia ,kwa vile mlizibiti vituo mifuko yenu ingekwenda kumiminwa tu wakati kura za waliokuja mnaziweka pembeni kiaina.Kwa hivyo kura zitaendana na idadi ya kituo,lakini mnachukuwa watu mnawapa karatasi za kura mara kumikumi ,mtu anajaza anakuja kutumbukiza,lazima idadi itapita ya waliojiandikisha kituoni.

Msijifanyie mambo ulizeni kwanza,mnaona sasa aibu iliyowakuta kama mimi ndio Magufuli tume yote naikata vichwa,wameniabisha.
Sasa kama mnasema kura nyingi zimetapakaa barabarani, kinachowashinda kwenda mahakani na kuzitumia kama shahidi ni kipi?

Tumeona mgombea wa jomb la Kawe, Halima Mdee akidai kukamata kura za kughushi, cha ajabu akazichoma moto. Huoni kama hapo amepoteza ushahidi? kama anaamini ni za kweli kwanini asizitunze ili ziwe kama evidence mahakamani.

Tumeona mgombea wa jimbo la Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameshika kura eti za wizi, anadai ameshinda ..kama anao ushahidi mbona ka mute? Na kaenda mbali zaidi kuwa ataandaa maandamano kuanzia kesho tarehe 02.11.2020

Tumeona aliyekuwa Meya wa Ubungo, Boniface ambaye alikuwa mgombea kupitia CHADEMA akidai ameshika kura za wizi, je, kaenda wapi sasa?

Suala siyo kulalamika, suala ni kuwa na hoja za maana.
 
Back
Top Bottom