Uchaguzi 2020 Matokeo Rasmi ya Jumla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2020

watu waporadhi kupoteza muda kwende kwenyemikutano kilasiku kipindi chote cha kampeni lakini muda mchache tu wakwenda kupiga kura hawaendi.
alafuwanakuja hapa kulalamika.
wabongo wengi unafiki ni hulka yetu.
 
Una kila haja ya kujua nguvu ya kura yako. Usiache kupiga kura kwa sababu mgombea wako ameshindwa.
kama kura yangu ingekuwa na nguvu kiasi hicho ningeshaona mabadiliko mda mrefu sana, sasa badala yake imekuwa kama najifurahisha tu hasa ya mwaka huu ndio nalaani sana kiasi chakuhisi nilipoteza sana mda wangu😠
 

Tumechagua maendeleo tunaenda na John Pombe Magufuli
 
Kuna haja gani kila miaka nikapige kura isiyo na impact yoyote kwa nchi yangu zaiΙ—i nakuwa kama najidanganya mwenyewe, mbona bora niache tu

Wenzako hawaelewi correlation kati ya kujiandikisha na kutokupiga kura vs kuheshimiwa uhuru wa kuchagua! Wao wanadhani tutajazana vituoni kama mazuzu wakati nguvu ya boksi la kura haiheshimiwi!

Nadhani mkuu unakumbuka awamu ya mwisho ya JK watu walivyoingia mitini na kuachana na kupiga kura, kama Taifa tusipofanya jambo kuna feedback tunawapa watoto wetu na tushingae heshima ya kupiga kura ikipotea!
 
Kwenye vita ya Uganda niliambiwa kuna watu walijitolea kwenda kupigana, je kwa Tz ya sasa kuna raia anaweza jitolea kweli?

Uzalendo wa nchi yetu uko wapi?
UKIWAONA HAWA KATIKA MAANDAMANO, ANDAMANA!!
---------------------------------

1. Ukimuona Dudley, mtoto wa kwanza na Freeman Mbowe na wadogo zake wakiongoza maandamano nawe andamana. Freeman Mbowe pekee hatoshi, yeye hawezi kupigwa risasi hata moja. Nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani nchini inamlinda, ni jicho la Dunia anatazamwa, hakuna risasi inayoweza kuelekezwa kwake hata moja. Pale Mkwajuni Kinondoni risasi ilimkwepa Mbowe ikamuua Akwiline Akwelina. Wazazi wake wanalia hadi sasa, hakuna kitu. Usipowaona watoto wa Freeman Mbowe usiandamane!!

2. Ukimuona Alicia Magabe na watoto wake wa damu andamana. Alicia ni mke wa Tundu Lissu ambae Urais wa Lissu unamhusu zaidi kuliko mimi na wewe. Ukimuona Tundu Lissu peke yake usidanganyike kuandamana. Lissu ndie aliegombea Urais kwa Chama kikuu cha upinzani akiungwa mkono na ACT Wazalendo, huyu ni icon ya uchaguzi, ndie mwanamkakati ktk maandano hayo. Dunia yote ipo kwake, akifa hakuna cha kujificha, mission INATIKI.

Hakuna Askari mpumbavu anaweza kulenga shabaha ktk mwili wa Lissu, risasi zitaelekezwa kwako. Utakufa na si ajabu usifahamike, taarifa zako hazitofika popote, utakufa kama Mbwa, utazikwa siku inayofuata ktk kabuli la futi mbili au usizikwe kabisa. Usipomuona Alicia na wanawe, usiandamane!!

3. Ukimuona Bi Fourtuna Salehe na Bi Aweina Sinani na watoto wao katika maandamano andamana. Hii ni familia ya Maalim Seif ambayo inasemwa kuwa imepelekwa Oman mafichoni tayari. Wanasema watu wameuawa Zanzibar lkn hakuna jina la mtoto wa Maalim Seif wala wa mtoto wa Jussa hata moja. Usiwe mjinga, hukuzaliwa kuwa chambo, hukuzaliwa kwa ajili ya Urais wa Maalim au Lissu. Wakiwa Marais wewe haitokusaidia chochote. Usipomuona mtoto wa Maalim Seif, wake zake na familia yake jilalie zako nyumbani hauna cha kupoteza.

4. Ukimuona Anna Bwana, Wiza na Josina ktk maandamano yaliyoitishwa na wewe ungana nao, andamana kwa moyo mkunjufu kabisa. Hii ni familia ya Zitto Kabwe, akiwa peke yake muache aendelee na kazi yake. Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Chama cha upinzani (KC), ni jicho la Dunia hawezi kupigwa risasi taratibu za kuzuia maandamano zinamtambua na kumlinda. Usipomuona mke wake, watoto na ndugu zake wengine achana na kazi hiyo haina faida itakupeleka kuzimu bure.

5. Ukimuona Askofu Bagonza na mkewe, na watoto wake wote ktk maandamano andamana. Akiwa peke yake muombee kwa Mungu, usijiunge nae. Ukimuona Lema na watoto wake, Sugu na mke wake na watoto zake, Msigwa na wadogo zake kutoka Iringa, Heche na mkewe na watoto wake andamana.
Ukiwaona wao peke yao usiandamane, Ubunge na Urais wao hauna maana yoyote kwako. Maisha yako ni ya kwako peke yako, pambana!!
#USIANDAMANE!!
 
N
Hisabati inaweza kuwa tatizo kubwa zaidi ya elimu ya uraia...
Ni kweli, lakini ndivyo utafiti unavyoonyesha. Ukweli utabaki kuwa pale pale kuna kila sababu za wanachi kuwa na mwamko wa kujitokeza na kupiga kura. Kura ina maamuzi makubwa sana.
 
Hii ndiyo kauli ya ushindi, tutashangilia mwaka 2025 baada ya kutimiza ahadi zilizoahidiwa.

"Wabunge wateule, Wawakilishi wateule na wadiwani Wateule wa CCM tayari waaze kufanya uchambuzi wa ahadi zilizotolewa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar pamoja na Ilani ya CCM na mara moja waaze kufuatilia kero na Watengeneze utaratibu mzuri wa kufuatilia na kusikiliza kero za wananchi na kuzijibu"
Noma nomaaaa [emoji23][emoji23][emoji23]View attachment 1617005

Sent from my G-PADLITE using JamiiForums mobile app
 
CCM mmeshavuruga hata mkipanga vipi mahesabu na matukio hayakubaliani,mlikosea,mipango iliharibika maana mpaka leo makaratasi ya kura za ushindi wenu yamejaa barabarani.

Kama ni mimi basi ningepanga na hakuna aibu ingelitokea ,Tayari unaowapiga kura wa nchi nzima,tayari unaowaliojiandikisha kila kituo ,sasa mngelipanga matokeo ya wizi kwa idadi husika ya kituo ,kwa hivyo kusingekuweko na haya makosa ya wizi wa kihesabu uliotokea.
yaani hayo mafuko ya rambo mliojaza kura za wizi zingeliendana na kituo mnakolipeleka

Chukua kituo kimeandikisha wapiga kura 100, 90 mpeni magufuli 5 lisu na zingine waliobakia ,kwa vile mlizibiti vituo mifuko yenu ingekwenda kumiminwa tu wakati kura za waliokuja mnaziweka pembeni kiaina.Kwa hivyo kura zitaendana na idadi ya kituo,lakini mnachukuwa watu mnawapa karatasi za kura mara kumikumi ,mtu anajaza anakuja kutumbukiza,lazima idadi itapita ya waliojiandikisha kituoni.

Msijifanyie mambo ulizeni kwanza,mnaona sasa aibu iliyowakuta kama mimi ndio Magufuli tume yote naikata vichwa,wameniabisha.
 
Ahadi ni moja tu, Tanzania iwe kama ulaya [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my G-PADLITE using JamiiForums mobile app
 
Wagombea urais wale wanawake wawili hasa yule anayesuka nywele anastahili kupewa nyadhifa fulani...
 
Sasa kama mnasema kura nyingi zimetapakaa barabarani, kinachowashinda kwenda mahakani na kuzitumia kama shahidi ni kipi?

Tumeona mgombea wa jomb la Kawe, Halima Mdee akidai kukamata kura za kughushi, cha ajabu akazichoma moto. Huoni kama hapo amepoteza ushahidi? kama anaamini ni za kweli kwanini asizitunze ili ziwe kama evidence mahakamani.

Tumeona mgombea wa jimbo la Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameshika kura eti za wizi, anadai ameshinda ..kama anao ushahidi mbona ka mute? Na kaenda mbali zaidi kuwa ataandaa maandamano kuanzia kesho tarehe 02.11.2020

Tumeona aliyekuwa Meya wa Ubungo, Boniface ambaye alikuwa mgombea kupitia CHADEMA akidai ameshika kura za wizi, je, kaenda wapi sasa?

Suala siyo kulalamika, suala ni kuwa na hoja za maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…