Matokeo ya kauli "Maisha yenyewe mafupi" huwa ni mabaya

Matokeo ya kauli "Maisha yenyewe mafupi" huwa ni mabaya

snap

Member
Joined
Jan 4, 2016
Posts
65
Reaction score
65
"Maisha yenyewe mafupi" Sio ajabu kujibiwa hivyo kila Ukileta thread za kuonyesha madhara ya vitu mbalimbali vinavyoharibu na kudhoofisha miili yetu. Tumekuwa watu wakujifariji sana Lakini pale yakikutokea yakukutokea ndo utakapoona umuhimu wa maisha na afya kwa ujumla. Kwa kifupi matokeo ya hiyo kauli huwa ni mabaya sana. Ndo pale utakapoanza kuja na thread za kuomba msaada na njia za kujinasua.

Tubadilike afya ni utajiri mkubwa sana acha nature ifanye kazi yake.
 
Ni sawa na mtu anayemtegemea mungu kwa kila kitu!

Nina jirani yangu hapa anaumwa, kila baada ya lisaa anaomba mungu (maombi yale ya kilokole) muda wote anasema amelogwa wala siyo ugonjwa wa kawaida.

Namwambia aende kituo cha afya, majibu yake anasema damu ya yesu itamponya.
 
Yesu haponyi wajinga waliokosa maarifa
 
"Maisha yenyewe mafupi" Sio ajabu kujibiwa hivyo kila Ukileta thread za kuonyesha madhara ya vitu mbalimbali vinavyoharibu na kudhoofisha miili yetu. Tumekuwa watu wakujifariji sana Lakini pale yakikutokea yakukutokea ndo utakapoona umuhimu wa maisha na afya kwa ujumla. Kwa kifupi matokeo ya hiyo kauli huwa ni mabaya sana. Ndo pale utakapoanza kuja na thread za kuomba msaada na njia za kujinasua.

Tubadilike afya ni utajiri mkubwa sana acha nature ifanye kazi yake.
Uko sahihi kwa 100%, nakumbuka kuna kipindi niliizoea hiyo kauli nikawa naandamwa na ajali za mara kwa mara na hadi sasa hivi nimeshapona zaidi ya ajali kumi na.

Nilipoielewa hii kauli;

Proverbs 18:21

"Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake."

Nikaacha kuitamka na namshukuru Mungu siandamwi tena na ajali.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Kuna dereva boda mmoja nimemsikia akilalamika kuwa anasikia kifua chake kina maumivu kama vile amebebeshwa jiwe na maumivu hayo hayaondoki, lakini kila baada ya muda jamaa anavuta sigara. Nikamwambia maumivu hayo ni dalili za mwili zinakuambia uache sigara.
 
Kwa kuwa mleta Mada ana mawazo finyu a anafikiri mwili na viungo kupata madhara au kupoteza maisha ni sababu ya kupoteza maisha. Kila binadamu Hana uhakika wa kuiona kesho yake isipokuwa ni kujiaminisha tu. Wangapi wamepata ulemavu bila kutegemea, kali ya ponda mali kufa kwaja ni ya miaka mingi na bado Ina matokeo mpaka leo. Je unajua kwanini Kuna kulia na kucheka
 
Back
Top Bottom