MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu


Bwana Kapinga mie nakuelewa sana na hakuna issue ninayodivert hapa ila najaribu kukuelewesha manake imekuwa ni kawaida sasa watu kuanza kulalamika na kulaumu hata kama hana uelewa wa jambo analolalamikia! Kwamba kwa nini wizara imewatumia Voda peke yao hilo mimi wala wewe hatuwezi kulisemea labda kama hayo makampuni mengine ya simu yakiongea au kupeleka malalamiko yao TCRA ndio tutajua ukweli isije kuwa kuna terms ambazo walishindwa kutimiza.

Kuhusu kuwa na bajeti ya kutangaza matokeo kwenye magazeti hilo sio kweli kabisa. Nina uhakika hakuna hata chombo kimoja cha habari kinacholipwa kwa ajili ya kutangaza matokeo. Ila huo ni ubunifu wao ili waongeze idadi ya wateja wa magazeti yao. Lete hoja nyingine tujadili!
 
Jaribu kufuatilia products za Seminary after kutoka huko ndo uje na conclusion yako. otherwise mchawi mchukie lakini haki yake umpatie. Hawa waalimu wao mara nyingi ni watu highly qualified na mazingira wanayosomea si rahisi sana mtu kufeli. Beside madarasa yao ni madogo na wanaochaguliwa kuingia ni watoto wenye uwezo mkubwa darasani....mi si msemaji wao though argument yangu ni based na expirience ndogo ya kuchangamana na wana Maua Seminary, naweza sahishwa.
 
 
lkn mbona wanapokua vyuoni buwa bogas? huwa 0 na hushindwa waliopata div 3?
 
Kiwango cha kumpima mwanafunzi yoyote kama ameelewa kinachotumika dunia nzima siyo mapambanisho ya hoja. Ni Exams pekee.

Wee! vipi?.Exam ni kipimo cha uelewa na akili ya mtu.Aliyefaulu vizuri masomo yake matarajio ni kuwa huku mitaani afanye vizuri katika mambo mengine.Hata ukimpa wizara atakuwa mzuri kuchambua mambo yanayohusika na wizara yake.
Exam kupata C,B,A tu haina maana yoyote.

 

Hizi ndizo akili zenu, hamsomi mkifikiria C = A, For ur information Kupata A kwenye Exams siyo sawa na kupata C. ninakushahuri kama una mtoto anasoma makazanie afahulu vizuri. Achana na madrasa
 
Eheee eheeee hawa jamaa banaa kila sehemu wanagongwa nyundo
 
Hizi ndizo akili zenu, hamsomi mkifikiria C = A, For ur information Kupata A kwenye Exams siyo sawa na kupata C. ninakushahuri kama una mtoto anasoma makazanie afahulu vizuri. Achana na madrasa

Ha ha ha ha watasikia basi wakiisha kunja zile suruali zao
 

Mnapambana kwa hoja zipi? Wapi? na kwa malengo gani? Hivi kumbe siku hizi kuna mapambano katika shule za sekondari nje ya mitihani ya taifa?
 

mnapopambana nao kwa hoja juu ya nini? michezo? general knowledge? ubishi wa kidini? sayansi?
 
lkn mbona wanapokua vyuoni buwa bogas? huwa 0 na hushindwa waliopata div 3?

Sina hakika na unachokisema ila mm na evidence waalimu wangu chuo kikuu zaidi ya watano walikuwa wanaseminary na wote wanasifika kwa ifundishaji mzuri na kutumia lugha ya kufundishia kwa ufasaha...
 
Mnapambana kwa hoja zipi? Wapi? na kwa malengo gani? Hivi kumbe siku hizi kuna mapambano katika shule za sekondari nje ya mitihani ya taifa?
Si kule kwenye viwanja vya Biblia!.
Hata kwenye wizara pia inayoongozwa na watu wa seminary ni ufisadi mtupu!.

 
Tatizo lako Muhogomchungu hujafanya uchunguzi wa kutosha kuhusiana na hizi shule za seminari. Kwa taarifa yako kwanza tu mwanafunzi kusurvive mpaka form four ujue ana uwezo wa hali ya juu mno, manake kila mwaka kuna alama zinazomwezesha kuingia darasa linalofuata, asipozifikisha anaondoka. Kwa hiyo kuna chekecheo la hali ya juu. Kwa hiyo ukiona mwanafunzi amefanya mtihani wa form four ujue hawezi kufeli hata kidogo.
Hii ni tofauti na shule zingine ambazo mchele na pumba vinawekwa pamoja kwa hiyo lazima matokeo ya mwisho yawe mchele na pumba vilevile.
 
ok, lkn bada ya necta kuona wazenj hawa wamefaulu na kukaribia tu kama seminary, necta iliruka, ikashtuka, ikavalia njuga. jee na huku smeinary ndio hivyo

Shule za seminari ni nyingi sana, na siyo zote zinazofanya vizuri angalia link ya mfano wa seminari zinazofanya vibaya, sababu ya shule za seminari zinazofanya vizuri iko wazi kabisa. Wao wana mfumo wa kuwapima wanafunzi mara kwa mara, ndiyo maana kama ilivyo changiwa kabla, wanafunzi wanaonza kidato cha kwanza wanaweza wote wasimalize kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya shule kimojawapo ikiwa kushindwa majaribio (tests), shule nyingi za seminari zinazofanya vizuri zina wanafunzi wachache, hivyo uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi ni mdogo 1: <40, upatikanaji wa vitabu vya kiada na ziada, walimu wenye ujuzi na mazingira mazuri ya shule. Jambo hili NECTA inalijua. Ila ikitokea Songea seminari ikifanya vizuri mtihani wa 2011, naamini NECTA watakuwa na kila sababu ya kufuatilia sababu, kwani matokeo yako ya mwaka huu ni mabaya.
http://admin.udsm.ac.tz/necta2010/CSEE2010/p0882.htm
 
.
ok, lkn bado najuliza hawa ndio wanaopta f1 class vyuoni?
 
Hizi ndizo akili zenu, hamsomi mkifikiria C = A, For ur information Kupata A kwenye Exams siyo sawa na kupata C. ninakushahuri kama una mtoto anasoma makazanie afahulu vizuri. Achana na madrasa

Hapa hueleweki unakusudia kufafanua nini?.Au ndio nyinyi mliohitimu seminary?
 
Hapa hueleweki unakusudia kufafanua nini?.Au ndio nyinyi mliohitimu seminary?

Hauwezi kunielewa leo ijumaa unafikiria kwenda msikitini, nafikiri tu discuss J3
 


Umezungumzia habari za Ushahidi, lakini katika Ushahidi wako ulichoweza kuthibisha ni kwamba High View walikuwa wanafanya Cheatings ili wafanane na Seminary kimatokeo
 
Binafsi namsifu sana Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani wa sasa, Dr Ndalichako. Amepunguza sana uvujaji na wizi wa mitihani. Kazi bado ngumu lakini mafanikio yameanza kuonekana kwa wanafunzi kupata matokeo halisi ya walichokifanya. Tulifika mahala wazazi wajinga kwa kushirikiana na baadhi ya wamiliki wa shule kuchangishana ili kununua mitihani hii kwa ajili watoto wao.
Tumuunge mkono Mama Ndalichako kwenye mapambano haya. Tulishafika kubaya kama tulivyo kwenye ufisadi sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…