Mkuu naona unajaribu saana ku divert issue..hamna mtu anayelalamika majibu kutopatikana kwa wananchi..issue ni kwamba iweje wizara iwatumie voda peke yake?? na pili kwanini voda icharge watu wakati wizara ina budget maalum ya kutangazia wanafunzi kama wanavyofanya kwenye magazeti? Unachoshindwa kuelewa wewe ni nini ??
Bwana Kapinga mie nakuelewa sana na hakuna issue ninayodivert hapa ila najaribu kukuelewesha manake imekuwa ni kawaida sasa watu kuanza kulalamika na kulaumu hata kama hana uelewa wa jambo analolalamikia! Kwamba kwa nini wizara imewatumia Voda peke yao hilo mimi wala wewe hatuwezi kulisemea labda kama hayo makampuni mengine ya simu yakiongea au kupeleka malalamiko yao TCRA ndio tutajua ukweli isije kuwa kuna terms ambazo walishindwa kutimiza.
Kuhusu kuwa na bajeti ya kutangaza matokeo kwenye magazeti hilo sio kweli kabisa. Nina uhakika hakuna hata chombo kimoja cha habari kinacholipwa kwa ajili ya kutangaza matokeo. Ila huo ni ubunifu wao ili waongeze idadi ya wateja wa magazeti yao. Lete hoja nyingine tujadili!