MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

Hakielimu: Siasa zimeathiri matokeo kidato cha nne Saturday, 29 January 2011 08:55

Fidelis Butahe

KUSHUKA kwa kiwango cha ufaulu kidato cha nne mwaka 2010 kwa asilimia 22 ni matokeo ya serikali kuruhusu propaganda za kisiasa katika mipango ya elimu, imeelezwa.

Hayo yalielezwa na Taasisi ya HakiElimu ikishirikiana na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) katika mkutano na waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam, jana.

Walieleza kwamba serikali imekuwa ikipanga mambo mengi ya elimu yakiongozwa na propaganda za kisiasa jambo ambalo halitekelezwi kikamilifu.Wakatoa mfano kuwa serikali iliwahi kutoa ahadi ya kujenga nyumba za walimu 21,000 lakini hadi unafika mwisho wa kipindi kilichokadiriwa ni 260 tu zilikuwa zimejengwa.

"Wanaweza kueleza kuwa wanajenga nyumba za walimu 21,000 lakini mpaka kipindi walichopanga kinamalizika wamejenga nyumba 260 tu," Alisema Ofisa Utetezi wa sera za elimu wa TEN/MET, Florence Francis.

Kutokana na hali hiyo, alishauri kwamba siasa isiingizwe katika sekta ya elimu kwa kuwa italiangamiza taifa.Francis alisema elimu ya Tanzania haitafika katika kiwango cha juu kama masuala ya siasa yataendelea kuchanganywa na elimu.

"Binafsi naona bora kuwa na sheria kuwa kila mtanzania, awe na fedha au asiwe nazo apeleke mtoto wake kusoma katika shule za serikali za Kata, kwa sababu vigogo hawaoni hasara ya shule hizi kwa kuwa watoto wao hawasomi huko," alisema Francis.

Alisema kuwa umefikiwa wakati kwa wananchi kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya kamati za shule na kuwasilisha matatizo yao sambamba na kufuatilia maendeleo ya watoto wao."Umefikia wakati wa serikali kutimiza ahadi zake, mpango wa MMES na MMEM ni mzuri, lakini wanaweza kueleza kuwa wanajenga nyumba za walimu 21,000 lakini mpaka kipindi walichopanga kinamalizika wamejenga nyumba 260 tu," alisema Francis.

Januari 25 Baraza la mitihani (Necta) ilitangaza matokeo ya kidato cha nne uliofanyika Oktoba, 2010 yanayoonyesha kuwa kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa asilimia 22 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2009 huku wasichana wakiwa wanaoongoza kwa kufanya vizuri.


Mkurugenzi wa Hakielimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hakielimu, Elizabeth Missokia alisema licha ya kuwa idadi ya watahiniwa waliofanya mtihani huo kuongezeka kwa asilimia 43, bado mazingira yanawagandamiza watoto wa masikini na kwamba wengi wao ndio waliofeli mtihani huo."Maelfu ya wanafunzi walioshindwa mtihani wametokea katika shule za kata ambako ndiko kwenye wananchi masikini zaidi.

Kwa mwenendo huu tutawakomboaje watu masikini wa nchi hii ambao ni wengi," alisema Missokia.Alisema tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo shule za serikali zilikuwa zikiongoza, hivi sasa mambo yamebadilika ambapo shule hizo zimekuwa zikifanya vibaya.

Kwa sababu hiyo akahoji ni kwa nini serikali isijifunze kuendesha shule zake kama zinavyoendeshwa shule za binafsi."Shule binafsi hazipati ruzuku ya serikali. Kwa nini uwekezaji wa serikali katika elimu usiendane na matarajio ya wananchi, walipa kodi," alihoji Missokia.Alisema kuwa hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa ili kuboresha sekta ya elimu kwa kuwa kila mwaka mikoa inayofanya vizuri ni ile ile.

"Tumesikia wasichana kuwa wamefanya vizuri, tujiulize ni wasichana wangapi waliofanya mtihani ule? Wavulana waliofaulu ni asilimia 56.28 na wasichana ni 43.47, waliopata daraja la I-III, wasichana ni asilimia 7.81 na wavulana ni 14.62.

Hii ni tofauti kubwa," alisema.Aliongeza " Haiwezekani kujifariji kwa kuangalia ufaulu wa wasichana wachache wakati huo huo fursa za walio wengi zikibinywa, malengo ni kuwaendeleza wote, wasichana kwa wavulana."Alizitaja sababu zilizochangia kushuka kwa ufaulu kuwa ni pamoja na uhaba wa walimu, mazingira duni ya kujifunzia, uhaba wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia pamoja na hamasa ndogo ya wanafunzi.

Alisema kuwa ili elimu haiwezi kuboreshwa kwa kuendelezwa kwa watu wachache wanaopata fursa za kipekee kwenye shule chache huku elimu ya jamii pana ikiwa mashakani."Hakuna haja ya kulumbana wala kuingiza siasa katika elimu, bali serikali itekeleza mipango na sera zilizopo na kuboresha mapungufu kwa kushirikiana na wadau," alisema Missokia.

Alisema kuwa ili kuboresha elimu kusiwe na njia za mkato bali ni kuwa na njia za kuwekeza kwa umakini katika elimu.Alisema ahadi zilizotolewa na rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu zifanyiwe kazi."Rais alitoa ahadi ya kuipa kipaumbele sekta ya elimu, kuboresha maslahi ya walimu, Wizara ya Tamisemi nayo iliahidi kuboresha mafunzo ya walimu, nyumba za walimu zitajengwa, maabara zitaongezwa, umeme utafika mashuleni ili kuboresha shule za serikali.

Ni matumani yetu kuwa ahadi hizi zitatekelezwa," alisema Missokia.Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, aliwaambia waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo kuwa wasichana wamefanya vizuri zaidi kuliko wavulana.Kwa mujibu wa matokeo ya mtihani wa mwaka jana, kati ya shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 40, saba ni shule za seminari na huku Shule ya Seminari ya Uru inaongoza shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 40. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa shule kumi za mwisho ni mchanganyiko wa shule za serikali na watu binafsi.

Joseph Mungai naye anena
Waziri wa zamani wa Elimu na Utamaduni, katika Serikali ya awamu ya tatu, Joseph Mungai amesema matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yamesababishwa na Serikali ya awamu ya nne kuyatupa baadhi ya mambo mazuri yaliyokuwemo kwenye mpango MMES.

Mungai ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Mkoani Iringa kwa nyakati tofautitofauti na Waziri katika awamu ya kwanza na ya pili kabla ya kuwa Waziri wa elimu mwaka 2000 hadi mwaka 2005, aliyataja baadhi ya mambo hayo ni kuwepo na mizania kati ya upanuzi wa elimu ya sekondari na upanuzi wa mafunzo ya walimu wa sekondari.

Alitaja sababu nyingine ambazo zilizochangia wanafunzi wengi waliohitimu kidato cha nne kushindwa mitihani kuwa ni upanuzi wa elimu ya sekondari bila kufuata mpango wa maendeleo ya elimu hiyo yaani MMES."Nafikiri kwa maoni yangu, haya matokeo ya sekondari yanatokana na kupanua elimu ya sekondari bila kufuata mpango wa elimu ya sekondari," alisema Mungai na kuongeza:"Kulikuwa na mpango wa MMES niliuacha pale (Wizara ya Elimu) tulikuwa tumepanga mambo mengi na ilikuwa yaende hatua kwa hatua.

Mojawapo ni kwamba ilikuwa baada ya miaka mitano, kuanzia 2005, idadi ya wanafunzi wanaokwenda elimu ya sekondari ndiyo wafikie asilimia 50.

Alisema baada ya mafanikio makubwa katika elimu ya msingi kutokana na utekelezaji wa MMEM na MMES ambao ulipaswa kuanzia mwaka 2005 na mwaka huo ndipo vilianzishwa Vyuo Vikuu vya Elimu vya Mkwawa na Chang'ombe kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa walimu wa sekondari.

Alisema Mkwawa na Chang'ombe vilianzishwa kwa lengo la kuweka mizainia kati ya upanuzi wa elimu ya sekondari na upanuzi wa mafunzo ya walimu wa sekondari.

Mungai aliongeza kwamba walikuwa wameongea na Vyuo hivyo baada ya kuanzishwa, kwamba wanafunzi wa mwaka uliokuwa unaonza wafundishwe zaidi mbinu za ufundishaji ili baada ya mwaka huo waende kusaidia kufundisha sekondari kupunguza uhaba wa walimu.

"Tulitaka wanafunzi walioingia mwaka wa kwanza wakati Vyuo hivyo vinaanzishwa, mkazo uwekwe zaidi kwenye mbinu za ufundashaji," alisema Mungai.

Mungai alisema serikali iliharibu pale ilipoendeleza mpango huo kwa kujenga shule ya sekondari kila kata huku zikikabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu. "Sasa kuna baadhi ya shule katika kata zina mwalimu mmoja au wawili... Ilifika wakati Wizara walilazimika kuanza kupanga upya walimu, haikuwa mbaya lakini tatizo ni kwamba baadhi ya shule zilikuwa zinafanya vizuri lakini walimu wake walipoondolewa na kuhamishiwa sehemu nyingine, shule hizo ziliathirika pia," alifafanua.

Tatizo lingine ambalo Mungai alisema limechangia matokeo mabaya ni mlundikano wa masomo kwa ngazi hiyo ya sekondari huku baadhi ya masomo yakiwa yanafundishwa kwa kiwango hafifu kutokana na walimu kutoyamudu. "Tulitengeneza Programu ya kupunguza wingi wa masomo katika shule za sekondari tukaondoa masomo ya michepuo kama ufundi, kilimo na biashara na tukaweka mkazo kwenye hisabati ili hisabati liwe na hesabu za biashara.

Hilo nalo liliondolewa," alisema. Alisema ili kuboresha elimu hiyo ya sekondari kuna haja ya kufanya marejeo ya Mpango mzima wa MMES pamoja na kuweka mkazo kwamba shuleni ni mahali pa mwalimu kufundisha na mwanafunzi kusoma.

"Nilipoingia Wizara ya Elimu nilikuta Pass rate (Kiwango cha kufaulu) kilikuwa asilimia 19 lakini kwa kuweka mkazo kwamba shuleni ni mahali pa mwalimu kufundisha na mwanafunzi kusoma na kufuta Umtashumta na Umiseta ingawa nalaumiwa mpaka leo, kiwango cha kufaulu kilipanda hadi asilimia 62 mwaka 2005."Lakini hebu angalia leo kiwango cha kufaulu darasa la saba kimekuwa kikishuka kila mwaka," alisema.
 
HTML:
hilo ni la muda mrefu hata sasa watu bado hawaoni matunda ya elimu kumekua na kundi kubwa la unemployment elimu yetu haimwandai kijana kwa ajira binafsi

Point taken.......................soko binafsi linahitaji uwekezaji mkubwa tena wa makusudi...............yawepo mabenki ya kuhudumia wajasiria mali tena kwa masharti nafuu na riba ndogo sana zisizozidi asilimi mbili.........................................

vinginevyo we are sitting on an unemployment time-bomb..............................
 
Matokeo yanafanana na mwenye jina.

Siyo suala la kufurahia bali linatupa mtihani mgumu wa kutafakari mustakabali wa taifa hili chini ya chama cha mapinduzi. Wakiongelea elimu mara nyingi sana watatutajia idadi ya shule na shule zenyewe ndizo hizi. Tena bora hii hata kuna division one, two na Three nyingine ni balaa.

Majengo bila vifaa vya kufundishia, walimu wenye ari na uwezo wa kutosha, Mitaala yenye kukidhi haja na mfumo rafiki wa kupata elimu hakuna tunachokifanya. Mbaya zaidi tunakimbilia kupewa waziri mwenye Phd wizara nyeti kama hii wakati hata wizara yenye mambo machache na kukimbizana na makandarasi ilimshinda. Tutafika kweli???????? wanyonge ndio tutakaoumia maana hawa ndio hufaulu na kuishia kwenye shule hizi na mwisho wa dreams zao zinaishia hapa. Shame on the government
 
Hivi ni shule zipi za kiislamu zinazofundisha kujitolea mhanga?.........msaada tafadhari
 
Matokeo yanafanana na mwenye jina.

Siyo suala la kufurahia bali linatupa mtihani mgumu wa kutafakari mustakabali wa taifa hili chini ya chama cha mapinduzi. Wakiongelea elimu mara nyingi sana watatutajia idadi ya shule na shule zenyewe ndizo hizi. Tena bora hii hata kuna division one, two na Three nyingine ni balaa.

Majengo bila vifaa vya kufundishia, walimu wenye ari na uwezo wa kutosha, Mitaala yenye kukidhi haja na mfumo rafiki wa kupata elimu hakuna tunachokifanya. Mbaya zaidi tunakimbilia kupewa waziri mwenye Phd wizara nyeti kama hii wakati hata wizara yenye mambo machache na kukimbizana na makandarasi ilimshinda. Tutafika kweli???????? wanyonge ndio tutakaoumia maana hawa ndio hufaulu na kuishia kwenye shule hizi na mwisho wa dreams zao zinaishia hapa. Shame on the government

Cha kuhuzunisha shule ipo JIJINI ambako kuna Rais, waziri wa Elimu, katibu wa waizara husika, mabosi lukuki lakini inapata ziro 314
 
Kwetu waislamu madarasa mwiko.....sisi kwetu madrasa tu na tunataka madrasa iwemo kwenye katiba ya tz km elimu ya muhimu.....tunataka serikali ya kikwete iweke kwenye katiba mpya mahakama ya kadhi na oic km kikwete na chama chake cha mafisadi walivyotuwekea kwenye ilani yao mahakama ya kadhi........pamoja na sisi kufeli sana bado sisi waislamu ndiyo wajanja na ndiyo tunaongoza nchi mtake msitake.......
 
chakusikitisha na kukera zaidi eti shule inauhaba wa madawati jamaani this is too much....yani wale ndugu zetu wa kijijini walalamikie vifaa na sie wa mjini pia loooh ...hebu tumsubirie labda makamba anaweza kupata walau moyo wa huruma khs mustakabari wa skuli yake ....pia ni changamoto kwetu vijana,wazee,wasomi,kwa wasio wasomi na wengne wote ambao tupo ndani ya jf kutoa solutions ya kuimprove matokeo ya wapendwa wetu,
 
Hapo tu ndipo nnashida napo!

nawasalimu wanamember wenzangu wadadavuaji wa mambo..yani cjui macho yangu yameona vibaya au ni vipi?ni hivi katika gazeti la jana la nipashe-28th january 2011 nimeona kama kuna picha la skuli ya makamba katika darasa mojawapo,je waungwana mazingira kama haya ni mazuri na yatachangia matokeo mazuri au mwenyejina yusuph makamba anaona fahari kwa hayo matokeo,na ningemwona mwenye busara kama hayo matokeo angetolea ufafanuzi kama anavyokuwa mwepesi wa kufafanua mambo huku akinukuu vifungu vya holy bible na holy quran...wanajf ninachoomba kwa mwenye gazeti la jana anipatie picha ya hlo darasa la makamba sec. School...nawasilisha mada
 
Matokeo yanafanana na mwenye jina.

Siyo suala la kufurahia bali linatupa mtihani mgumu wa kutafakari mustakabali wa taifa hili chini ya chama cha mapinduzi. Wakiongelea elimu mara nyingi sana watatutajia idadi ya shule na shule zenyewe ndizo hizi. Tena bora hii hata kuna division one, two na Three nyingine ni balaa.

Majengo bila vifaa vya kufundishia, walimu wenye ari na uwezo wa kutosha, Mitaala yenye kukidhi haja na mfumo rafiki wa kupata elimu hakuna tunachokifanya. Mbaya zaidi tunakimbilia kupewa waziri mwenye Phd wizara nyeti kama hii wakati hata wizara yenye mambo machache na kukimbizana na makandarasi ilimshinda. Tutafika kweli???????? wanyonge ndio tutakaoumia maana hawa ndio hufaulu na kuishia kwenye shule hizi na mwisho wa dreams zao zinaishia hapa. Shame on the government

Tatizo la sisi waafrika ni kua viongozi wavimba vichwa pale jengo/barabara au shule inapopewa jina la mtu muhusika bila kuzingatia kuboresha mazingira husika, sasa shule imepewa jina lako inakubidi uzingatie mitaala ya shule pamoja na kuboresha mazingira ili taasisi hiyo ilyopewa jina la mtu muhusika isije ikachafua jina lako na pia iwe ni sifa kwako na kwataifa kwa ujumla. Mimi ukiniuliza Yusufu Makamba kalifanyia nini taifa hili la Tanzania mpaka kupelekea shule kuitwa jina lake! na mpaka sasa hivi hajatamka chochote kuhusu hiyo shule kwa kuboronga kwenye matokeo yaliyotoka hivi juzi.
 
Wapendwa wana JF kufeli kwa wanafunzi hawa ni tatizo la mkuu wa shule,nimeongea na walimu zaidi ya watatu wanasema tatizo ni mkuu wa shule kushindwa kuwajibika,wanasema wanafunzi ni jeuri hawaingii madarasani,wakiwapa adhabu mkuu wa shule anawatetea,pili walimu wanapigwa na wanafunzi wanaviziwa kwenye kale kapori pale karibu na shule,mwanafunzi huyo akipelekwa kwa mkuu hafanywi lolote bali ataambiwa nenda mwanangu mungu atakusaidia,wanasema hata ikitokea mwanafunzi akifukuzwa baada ya siku mbili walimu wanamuona darasani,kwa hiyo walimu wanasema bila kuondolewa kwa huyo mama ambaye ndiye mkuu,zero hazitaisha,yapo mengi ila mda wangu ni mdogo kukaa kwenye pc,asanteni.
 
aSANTE KWA RESEARCH YAKO!
Unashauri nini kifanyike sasa?
 
Matokeo yanafanana na mwenye jina.

Siyo suala la kufurahia bali linatupa mtihani mgumu wa kutafakari mustakabali wa taifa hili chini ya chama cha mapinduzi. Wakiongelea elimu mara nyingi sana watatutajia idadi ya shule na shule zenyewe ndizo hizi. Tena bora hii hata kuna division one, two na Three nyingine ni balaa.

Majengo bila vifaa vya kufundishia, walimu wenye ari na uwezo wa kutosha, Mitaala yenye kukidhi haja na mfumo rafiki wa kupata elimu hakuna tunachokifanya. Mbaya zaidi tunakimbilia kupewa waziri mwenye Phd wizara nyeti kama hii wakati hata wizara yenye mambo machache na kukimbizana na makandarasi ilimshinda. Tutafika kweli???????? wanyonge ndio tutakaoumia maana hawa ndio hufaulu na kuishia kwenye shule hizi na mwisho wa dreams zao zinaishia hapa. Shame on the government

Kawambwa kupewa wizara ya elimu ni mkakati wa jk kuboresha kwao.mwanzo alikuwa ujenzi,na alichofanya kwao kinaonekana,sasa elimu ili aboreshe idara ya elimu huko bagamoyo....jk ni mdini na mwenye upendeleo wazi kwa anakotoka.
 
Kwani matokeo yana uhusiano na jina la shule??
 
Zuia kesi ya Dowans/ICC mahakama kuu, utapata hela za kupeleka kwa wanafunzi. Ukiandamana unabaki na njaa au risasi ya moto.
 
Nadhani Ujumbe Umefika kwa Wahusika next time Tender nadhani tutaziona kwenye Magazeti! Mission Accoumplished.

Sioni haja ya tenda mimi. Nilidhani kama kuna kampuni ya simu inataka kujiunga ili itoe huduma hiyo ni kiasi cha kuwasiliana na NECTA na hilo likafanyika. Ninaamini lengo la NECTA nikutaka kufikia watu wengi zaidi na hivyo mitando ikiwa mingi inakua nia bora kwa NECTA.

Kwani ilishawahi kutangazwa tenda ili gazeti fulani liweze ku-publish matokeo? NI suala la gazeti husika kwenda NECTA na kupata nakala ya matokeo basi!

Mbona matokeo yanawekwaga kwenye tovuti ya wizara ya elimu, UDSM, SUA na kuna wakati hata TANEDU walikua wanaweka, ilitangazwa tenda?

Hata kama wewe una website yako unataka uwe unatoa matokeo utapewa na wala hutatangaziwa tenda. Fungukeni macho wakuuu.

Ninaamini kulipia bandwidth ili utangaze matokeo kwa tuvuti ni gharama kubwa hivyo kama wadau watajitokeza (including JF, MCHUZI NK) wakawa wanaweka hayo matokeo pindi yakitoka for sure NECTA watafurahi sana ... jaribuni mkiambiwa tenda ndo mje mlalame humu ndani.

NADHANI NIMEELEWEKA!
 
Mkuu, ukweli haupingiki kama hizi Seminary si mchezo kwa u-terial,ila na paper au maswali ( posibo) pia huwa wanazipata kirahisi sana,matokeo yake vyouni wanaishia kuwa watumwa wa maprof na tutors kwa kuwa wengi wao hawajiwezi kabisaaaaaaaa. Tumekuta nao wengi tu vyuoni hao waseminary na mifano tunayo, na sisi wa St.Kayumba ndo tulikuwa tunawasaidia hata kuandika presentation hawawezi.Hiyo Shule ya Marian tunaifahamu vizuri tu na yule ticha mkuu wao anayewaoa mabinti wa watu burebure. Hata Mr.Nkumbi tunajua kama alikuwa anatoa paper kwa st Mary's, Loyola,St James nk.
HAYA MAAJABU, ETI MZUMBE NA ILBORU HAINA TOPTEN?????????????????:clap2:

TUULIZE SISI BANA MAISHA YA SHULE ZA KITANZANIA,
 
Katika kuangalia jinsi CCM inavyoua elimu kwa watoto wa wapiga kura wake nimekutana na shule inaitwa Jakaya Kikwate ...sijui iko wapi! Kuna matokeo ya form 4 hapa ambapo kati ya watoto 124 waliofanya mtihani % 61 wamepata sifuri .! na wengine walio baki wameambulia DV 4 ZA KUFA! KILICHONISHANGAZA NI HIYO ASILIMIA YA 0,KUFANANA NA ASILIMIA ALIZOPATA MH JAKAYA KIKWAETE KATIKA UCHAGUZI ....WHAT A KOINSIDENSI!
Nawapa pole vijana hawa lakini huo sio mwisho bado wananafasi ya kupiga kura
 
Back
Top Bottom