MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

Kufail kidato cha nne kuna impact ya kwenda A level na hii inakuwa reflected hata idadi ya wanafunzi Islaam kuingia kwenye vyuo vikuu. Matokeo yake kuna kuwa na waislam wachache tena wenye shahada za pass ambao hawawezi kujenga hoja wanakimbilia ooooh hatupewi nafasi! Utampaje nafasi mtu mwenye Pass uache mwenye first class ama upper second. Hebu amkeni nyie mitaala yenu mpunguze Juzuu watoto wa Islaam kwenye shule wafaulu

............ hatupunguzi ! zile zile thelathini ! hatubabaishwi na mila zenu, ya Dunia ni ya kupita tu ! hata kaburi ukiitia mable na maru maru bado utaoza tu ! Tunamuogopa Mwenyezi Mungu kuliko nyie watu na yeye peke yake ndie ajuaye ametupangia nini ! wewe huwezi kuongeza wala kupunguza !
 
Wakuu hii inauma sana, tukumbuke kuwa kufeli kwa vijana wetu hawa wa kiislamu ni kufeli kwa vijana wetu wote wakitanzania. Hapa hakuna cha waislamu wala wakristo wote ni vijana wa Kitanzania na hata zikija statistics still zitaleta results kuwa vijana wa kitanzania wanastruggle kwa education na wala hazitasema waislamu ndio wanastruggle. Personally naona there is a need for the top education commentators to sit and share any strategic plans with Muslim leaders and Scholars for this matter. Future ya Tanzania inahitaji sana educated youngsters na haswa wa Kiislamu ili kuwe na sharing of productive values, thoughts and loyalty of this Nation. WE WILL FALL, RISE AND SHARE EVERYTHING IN UTOPIA!. Ngoja nikatafute Henineken ninywe maana nchi inanichanganya hii na nataka watoto na wajukuu zangu wawe namaisha mazuri baadae sasa kama kuna watu wanashabikia Islamic schools to fail then sijui huko mbeleni kutakuwa na society ya aina gani jamani! badala ya kufurahia wafaulu! ahh!
 
Matokeo kidato cha IV wanafunzi hawakuwa serious. Nasema hivi kwa maana kwamba mbona wapo waliofaulu huo huo mtihani walofanya wengine.Hii inanikumbusha kwamba kila mtu atavuna alichopanda.Sasa wewe upande mahindi utategemea kuvuna karanga ama mahindi?Jibu automatically nikipanda mahindi nitavuna mahindi.Mwanafunzi wa sasa hivi yupo tayari kukuimbia mashairi ya bongoflaver bila kusahau hata verse moja,ila mlete kwenye book-keeping atakuambia mwalimu wao sio mzuri.Huo ni uongo na visingizio kwa baadhi ya wanafunzi.Tunapotoa visingizio kuwa serikali ni mchawi wetu hapo sikubaliani hata kidogo.Wanafunzi wa kidato cha IV wanataka serekali ifanyeje?Kama utasema walimu hawafundishi ama hawafai utakuwa unawakosea haki. Wanafunzi wa O-LEVEL acheni mchezo someni jamani.Wazazi wenu wanataabika ili muende shule na pengine hata mlo pale nyumbani hautoshelezi ili wewe mwanafunzi uende shule.Please kuweni serious na book.
 
Matokeo kidato cha IV wanafunzi hawakuwa serious. Nasema hivi kwa maana kwamba mbona wapo waliofaulu huo huo mtihani walofanya wengine.Hii inanikumbusha kwamba kila mtu atavuna alichopanda.Sasa wewe upande mahindi utategemea kuvuna karanga ama mahindi?Jibu automatically nikipanda mahindi nitavuna mahindi.Mwanafunzi wa sasa hivi yupo tayari kukuimbia mashairi ya bongoflaver bila kusahau hata verse moja,ila mlete kwenye book-keeping atakuambia mwalimu wao sio mzuri.Huo ni uongo na visingizio kwa baadhi ya wanafunzi.Tunapotoa visingizio kuwa serikali ni mchawi wetu hapo sikubaliani hata kidogo.Wanafunzi wa kidato cha IV wanataka serekali ifanyeje?Kama utasema walimu hawafundishi ama hawafai utakuwa unawakosea haki. Wanafunzi wa O-LEVEL acheni mchezo someni jamani.Wazazi wenu wanataabika ili muende shule na pengine hata mlo pale nyumbani hautoshelezi ili wewe mwanafunzi uende shule.Please kuweni serious na book.
 
Nakubaliana nawe mkuu kwa shule zenye walimu lakini kwa shule ambazo hazina walimu ni jukumu la serikali kupeleka walimu na vitabu. Walimu hasa na si VODAFASTA
 
Speculating......mh,
Eng Nsiande

I am not speculating Engineer, lakini ingekuwa ni vyema zaidi watu kuzungumzia kwa nini kuna failure kubwa sana Form IV kuliko wanavyofanya sasa - pointing fingers at Islamic schools.
 
Sababu za kufeli zipo nyingi ingawa mwanafunzi inabidi aplay part kubwa ili afaulu.
Usiwalaumu tu wao.
Jaribu kufanya karesearch kadogo, utaelewa hapo.
 
Nilikuwa natazama interview TBC leo machana.
Idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani ni 350,0000 na waliofaulu na kupata sifa za kujiunga na form five ni 40,000 tu. Hivyo kwa mahesabu yangu ni kama 10% hivi ndo wamefaulu na siyo 50% kama media zinavyo eleza.

Where is Shukuru kawambwa now days?

Kuna usemi kuwa picha zinaongea kuliko maneno. Let's visualize the results. Source of data michuzi blog.
Kwa hiyo kwa graph hizo hapo 89% wameshindwa. 11% ndio wanaohesabiwa kuwa wamefaulu. Hata hivyo katika hao 7% huenda wakaambulia kwenda kusomea kuwa walimu wa shule za kata kwani combination huenda hazikubali!!
 

Attachments

  • frm4-results2010.jpg
    frm4-results2010.jpg
    16.6 KB · Views: 45
  • frm4-results2010-2.jpg
    frm4-results2010-2.jpg
    13.7 KB · Views: 41
hao 11 ni wale wenye div 1-3 wenye uwezo wa kuendelea kwa hiyo watakaopata vyeti vya 4m 4 ni asilimia 50 :car:
 
Kawabwa(18).jpg





Zaidi ya walimu 15,000 waliohitimu stashahada na shahada ya elimu (BAED) katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini, wanazurura mitaani baada ya serikali kushindwa kuwapangia kwa wakati shule za kufundisha.
Hali hiyo inakuja huku shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini hasa za kata zikikabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa siku kadhaa sehemu mbalimbali nchini, umebaini kuwa maelfu kwa maelfu ya wahitimu hao hivi sasa wanazurura mitaani huku wengine wakijaribu kutafuta ajira nyingine baada ya kuisubiri kwa muda mrefu serikali iwapangie vituo vyao vya kazi bila mafanikio.
Wengi wa walimu hao walihitimu stashahada na shahada zao Juni na Julai, mwaka jana na walitarajia serikali ingewapangia shule za kufanyia kazi kuanzia Septemba, mwaka jana ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu katika shule mbalimbali nchini.
Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda huo bila mafanikio, wengi wa walimu hao sasa wameanza kukata tamaa na hivyo kuamua kujitosa kusaka ajira nyingine kwenye shule za sekondari binafsi pamoja na mashirika na makampuni mbalimbali.
Mbali na shule binafsi, makampuni, mashirika na taasisi nyingine, pia yameanza kuwachangamkia wasomi hao ambao wengi wao wamesomeshwa kwa kodi za wananchi kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Baadhi ya makampuni yanayoonekana kunufaika na wahitimu hao ni ya simu za mkononi ambayo kila kukicha yamekuwa yakipanua wigo wa shughuli zake ili kukabiliana na ushindani mkubwa wa kibiashara wa mitandao hiyo hapa nchini kwa sasa.
“Tumesubiri posting (vituo vya kazi) zetu mpaka sasa tunaelekea kukata tamaa. Serikali haijatupangia na imekaa kimya. Hali hii inatutia wasiwasi na kuanza kuhaha kutafuta ajira sehemu nyingine. Hatuwezi kuishi nyumbani tukiendelea kuwa wategemezi wa wazazi na walezi kwa kipindi chote hiki,” alisema mmoja wa wahitimu hao ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Kwa mujibu wa mhitimu huyo wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT) cha jijini Mwanza, tayari baadhi ya wahitimu wenzake wa shahada ya elimu katika chuo hicho wamepata ajira sehemu mbalimbali.
Zaidi ya walimu 500 walihitimu mafunzo yao katika chuo hicho na kufanya mahafali Novemba 27, mwaka jana. Mhitimu mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu Mlimani (UDSM), ambaye pia hakutaka jina lake litajwe, pia alitoa malalamiko yanayofanana na mwenzake wa SAUT.
“Siyo siri, wengi tumeanza kukata tamaa maana hatupewi hata taarifa za nini kinaendelea kuhusiana na posting zetu. Hali hii inatufanya tushindwe kuelewa hatma ya maisha yetu baada ya kuhitimu masomo,” alisema.
Mhitimu mwingine wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Dar es Salaam (Duce), ambaye pia hakuwa tayari jina lake lichapishwe gazetini, alisema tangu walipohitimu walimu zaidi ya 900 Julai, mwaka jana na kufanya mahafali Novemba, mwaka jana, walitarajia wangepangiwa vituo vya kazi.
Hata hivyo, alisema kwa upande wao imekuwa tofauti na imewafanya waanze kuangalia ustaarabu mwingine wa kuomba kazi sehemu nyingine.
Aliitaka serikali iwape taarifa ili wajue hatma yao maana wamekaa mitaani na kuchoka.
“Wengi niliohitimu nao wako tu majumbani na wanahangaika kutafuta ajira maeneo mengine,” alisema huku akisisitiza kuwa wanashangaa kwa kuwa haijawahi kutokea kwani wahitimu wenzao walikuwa wakimaliza tu wanapangiwa vituo vyao vya kazi. Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kuhusiana na suala la walimu hao kutopangiwa vituo vya kazi, aliitaka serikali kulichukulia kama ni la maafa. Mukoba alisema anashangaa kuona walimu hao wakiachwa kuendelea kuzurura mitaani huku shule nyingi za serikali zikiwa na uhaba mkubwa wa walimu.
“Serikali inapaswa kulichukulia suala hili kama maafa sawa na inapotokea janga la mafuriko ambapo hufanya kila liwezekanalo kupata fedha, mahema na chakula kwa ajili ya kuokoa maisha ya waathirika na ndivyo serikali inavyotakiwa kufanya sasa kwa walimu hao,” alisema.
Alisema kimsingi suala la walimu hao kutopangiwa sehemu zao za kazi linakisononesha mno chama chao kwa kuwa nao ni sehemu ya raia wa Tanzania.
Mukoba aliongeza kuwa walimu zaidi ya 16,000 wamehitimu masomo yao, lakini jambo la kushangaza wameachwa mitaani bila ajira huku shule nyingi za serikali zikikabiliwa na uhaba wa wataalam hao na haijulikani fedha kwa ajili ya mishahara yao zimekwenda wapi.
Hata hivyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alipotafutwa jana kwa simu yake ya mkononi namba 0787 400700, ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa. Lakini Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Magdalena Kishiwa, alipohojiwa juu ya suala hilo, alijibu kwamba zoezi la kuwapangia walimu hao wapya vituo vya kazi linaendelea na likikamilika watajulishwa.
Alipoulizwa kama haoni kuchelewa huko kwa serikali kutasababisha walimu wengi ama kuajiriwa na shule binafsi au mashirika na makampuni mengine na hivyo kuifanya serikali iendelee kukabiliwa na uhaba wa walimu licha ya kulipiwa gharama za masomo yao kupitia Bodi ya Mikopo, alisita kutoa jibu na kisha kukata simu yake ya kiganjani.
Alipopigiwa tena, alisema alikuwa katika kikao na kutaka apigiwe baada ya saa moja, lakini baada ya mwandishi kufanya hivyo, namba yake ilikuwa haipatikani.
Iwapo walimu hao hawatapangiwa vituo vya kazi mapema, ipo hatari ya kukutana na wenzao katika soko la ajira ambao wanategemea kuanza kuhitimu mafunzo yao kuanzia Juni, mwaka huu licha ya serikali mara kadhaa kutamka kuwa imelenga kupunguza tatizo la uhaba wa walimu nchini.


Kutokana na habari hii nikwamba muanzishi wa thread ameshazijua sababu kwamba kwanini wengine washinde na wangine wengi hasa kutoka shule za serikali wafeli
 
JUZI Rais Jakaya Kikwete alizindua awamu ya pili ya Mpango wa Mendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES-II) wenye lengo la kuboresha mazingira ya utoaji elimu hiyo.

Huu ni mwendelezo wa awamu ya kwanza ya MMES iliyoanza rasmi 2006 baada ya Serikali ya Awamu ya Nne kuingia madarakani. Katika hatua hiyo ilianzishwa kampeni nzito ya kufungua shule za sekondari za kata nchi nzima.

Lengo MMES-II utakaotekelezwa kuanzia 2011 hadi 2015 ni kuboresha elimu ya sayansi, mazingira ya kufundishia, kuboresha makazi ya walimu sambamba na kujenga maabara katika shule za sekondari za Serikali nchini.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Serikali, mpango huo utatekelezwa kwa msaada wa Benki ya Dunia (WB) ambayo imekubali kutoa dola za Marekani 150 milioni na tayari imetoa dola 49 milioni, huku Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) ikiwa imekubali kusaidia mpango huo.

Hata hivyo mpango huu umezinduliwa wakati mfumo wa elimu nchini ukiendelea kudorora kutokana na mazingira ya kufundishia kuendelea kuporomoka kwa sababu ya kukosekana kwa walimu wa kutosha katika shule nyingi za sekondari na hasa za kata.

Ukweli ni kwamba, hali halisi inaonyesha kuwa shule nyingi za sekondari za kata hazina walimu. Baadhi ya sekondari za kata zina mwalimu mmoja ambaye ndiyo mkuu wa shule na mwenye jukumu la kufundisha madarasa yote, sawa tu na hali ilivyo katika shule nyingi za msingi za vijijini.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba kutokana na kukosekana kwa walimu, shule nyingi za kata zinaajiri walimu bila kuzingatia sifa, maadamu mtu kamaliza kidato cha sita ili kuziba pengo.

Si hivyo tu licha ya tatizo hilo la walimu kuwa kubwa, mwaka huu Serikali imetangaza kuwa kati ya walimu 17,684 walohitimu na kufauliu katika vyou mbalimbali vya elimu nchini, 9,226 tu ndiyo wamepata ajira na kati hao 187 wanakwenda kufundisha vyuo vya elimu. Hii inaonyesha kuwa bado kuna tatizo kubwa katika kuboresha sekta hii muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.

Kwa ujumla, tunapongeza mipango ya Serikali katika kubioresha elimu, lakini tuna mashaka na utekelezaji wake ambao unaonyesha wazi kuwa unafanyika kisiasa zaidi badala ya kufanywa kisayansi.

Kwa mfano, katika awamu ya kwanza ya MMES tuliona nguvu kubwa iliyotumika kuhamasisha na kuwalazimisha wananchi kujenga shule za kata na kabla hazikamilika na kufanyika maandalizi mazuri ya kutoa elimu inayolingana na hadhi ya sekondari, shule zilifunguliwa kila mahali hivyo kushusha hadhi na kiwango cha elimu hiyo.

Ni kweli watoto wengi wamefika sekondari, lakini hali halisi inaonyesha kuwa wengi wa watoto waliopelekwa katika sekondari za kata hawajaeleimika, kwani miongoni mwao wanashindwa kusoma, ukiachia mbali masomo ya sayansi ambayo kwao ni sawa na usiki wa kiza.

Swali letu ni kwamba, kama Serikali imeshindwa kutoa ajira kwa walimu zaidi ya 7,000 waliohitimu na kufaulu mwaka jana wakati hitaji lipo, tutafanikiwaje kuboresha elimu na kutekeleza MMES-II?

Ni nguvu kiasi gani imepangwa kutumika kuhakikisha kuwa ajira za walimu zinapatikana na malengo ya kuboresha elimu yanafanikiwa?
Kulingana na uhitaji wa walimu unaolikabili taifa wakati huu, hatukutarajia walimu watashindwa kupata ajira, tulidhani walimu wote wangepangiwa kazi huku serikali ikendelea kutafuta walimu wapya.

Lakini kwa hali hii ni kwamba, hata watakaohitimu hawana uhakika wa ajira sawa tu na sekta nyingine ambazo hazina ajira.

Inakuwaje ajira ikosekane katika sekta ya elimu ambayo ina nafasi za kazi na walimu wanahitajika sana?
Inaonekana Serikali haikujipanga ipasavyo kuhakikisha kuwa walimu wote watakaohitimu wanapata kazi ingawa ilitumia fedha nyingi kuwapa elimu na kutangaza kuwa wote watapata kazi!
Hii ni changamoto kwa Rais Kikwete kwamba mafanikio ya MMES-II ni yumkini kama mfumo wa utekelezaji hatuabadilishwa.
Ikumbukwe kuwa elimu ni taaluma haihitaji siasa.
 
Ila mkuu ukiangalia vizuri, kuna shule hapo hapo mjini darasa zima la wanafunzi 100 wamefaulu... yaani hakuna div IV wala ziro.... lakini shule nyingine zina IV na ziro na nyingi ya hizo niza kata.... kwa hiyo ni obvious kwamba walimu ni tatizo kubwa na hilo ni jukumu la serikali hakuna kukwepa!!
 
sababu za kufeli kidato cha nne hizi hapa:
1. Shule za kata
2. Hiki ndo kidato wakati kipo mwaka wa pili serikali ilifuta kufeli kidato cha pili, na kusema kila mwanafunzi atapita tu.

naomba kuicheka serikali nikiwa nimekasirika.

Hahahahahaha ! muda wenu umekwisha sasa upuuuuzi sasa basiiiiii ! tokeni
 
sababu za kufeli kidato cha nne hizi hapa:
1. Shule za kata
2. Hiki ndo kidato wakati kipo mwaka wa pili serikali ilifuta kufeli kidato cha pili, na kusema kila mwanafunzi atapita tu.

naomba kuicheka serikali nikiwa nimekasirika.

Hahahahahaha ! muda wenu umekwisha sasa upuuuuzi sasa basiiiiii ! tokeni

Mkuu Mess, uko sahihi kabisa kwa sababu hizo mbili japo ndani yake kuna mengi na mjumuiko wake ndio umetufikisha hapa tulipo, taifa lisilokuwa na cha kujivunia kwa maendeleo, Elimu chali, Viwandani chali, kilimo ndio usiseme, miundombinu chali n.k. sijui tunakwenda wapi na Elimu yetu hii isiyo elimu.
 
Hii ni aibu kwa taifa la Tanzania na wananchi wake kuwa na tabaka la watu wenye Elimu na uelewa wa namna hii!. Je, ni kweli shule za Kata ndo chanzo cha yote haya!!!! au walimu wa VODA FASTA ndo chanzo cha haya! au zamani watu walikuwa wakiiba sana mitihani na mwaka huu wamezibitiwa wizi??? au morali ya waalimu haipo katika suala zima la ufundishaji kama ilivyokuwa enzi zile hasa kwa shule za Serikali????
Maswali haya na mengine yanahitaji majibu na ufumbuzi, Tutafute suluhisho la hili, Nini kifanyike kuondokana na tatizo hili???.
Hapo chini ni Matokeo hayo kwa kifupi yakionyesha Idadi kwa kila daraja na asilimia zake.

Daraja I - 5,363 1.5% Daraja la II 9,942 Asilimia 2.8% Daraja la III 25,083 Asilimia 7.1% Daraja la IV 136,633 Asilimia 38.9% Daraja la 0 174,193 Asilimia 49.6% na Jumla ya wanafunzi 351,214 walifanya mtihani huo.
NB: Kwa kifupi, Daraja la Kwanza hadi la Tatu ni asilimia 11.5 tu na madaraja ya Nne na la Zero (o) yanachukua asilimia 38.9 na aslimia 49.6 sawia. Hii inaashiria nini kwa Taifa la Tanzania?? na hata
Waziri wa elimu sijasikia akitoa tamko na wala Mhe. Dr. Dr. Jk yuko inje ya nchi wala hashitushwi na hali hii anaona ni kawaida tu! Kwani Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana kwa mfumo huu wa kuwa na tabaka la watu wa aina hii ambao watakuja kuwa Madaktari Mhimbili, Bugando, KCMC na watakuwa Specilist wa Ubongo na mifumo ya fahamu!!!!.​
 
Najiuliza sipati majibu
- Shule za kata zinasimamiwa na Wizara ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa
-Shule za zamani kama azania, tambaza, ilboru, msalato, etc the like, zinasimamiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi
-Baraza la mitihani linasimamiwa na wizara ya elimu

Kituko kingine
Mfano DAR ES SALAAM
-Shule za secondary za kata na zile rasmi za zamani (za o-level tu) nyingi mno. pengine zaidi ya 30- kupitia MEMM wamejenga shule nyingi sana za O-level, chanika almost kila street in shule ya kata.
-High school zilizopo ukiondoa Kibasila zote ni zile zile zilizoko eneo la upanga - Jangwani, Zanaki, Azania, Tambaza.


Katika hali hii, kama nilivyo wasikia watu wakihoji, Je baraza la mitihani linaweza kuwa fair katika kutoa alama kati ya shule za kata (zisizo na vifaa na walimu waliobobea na zilizo chini ya Tamisemi) na shule za secondary zilizo chini ya wizara ya elimu ilhali yenyewe iko chini ya wizara hiyo hiyo?

Kwa nini serikali isijenge angalau high school mbili au moja iliyokamilika kila wilaya?
 
Hakuna ROLE MODELS wa kielimu.......vijana wanamsikiliza zaidi na kutamani kuwa kama DIAMOND....ndio priority kwao....wana practise mashairi ya bongoflava kuliko past papers...na Rais kachangia kwa kununua studio ya kisasa ya muziki badala ya vifaa vya maabara
 
Sie kama sehemu ya Jamii na ambao tumepatwa na huu mkasa na tunafahamu chanzo cha Tatizo, tutafute SULUHISHO LAKE!! nini kifanyike???.
 
Mkuu si kweli kwamba matokeo mabaya ni kwasababu ya shule za KATA. La asha, sababu ni kuwa serikali haikupeleka vitu muhimu katika hizo shule yaani walimu, vitabu, maabara, Library na kujenga nyumba za walimu.

Tusiwe wagumu wa kusema ukweli, serikali inahusika na matokeo haya kwa 101%. Na kama yangekuwa mazuri basi kwa wenye akili wangehoji imekuwaje matokeo yakawa mazuri?????!

Hiyo ya kufuta mitihani ya form 2 ni sahihi kabisa, mitihani hiyo ilikuwa inawapa vijana uzoefu wa kufanya mitiahani ya taifa na kujua umuhimu wa juhudi katika masomo.

Usishangae kusikia wahitimu wengine wa form 4 hata hawajui kusoma na kuandika; si wote tunakumbuka yule mkuu wa sekondari aliyelalamika kupokea vijana wa form 1 wasiojua kusoma na kuandika!!!!!!!!!!!

Tanzania yetu kwa pamoja tutaijenga!
 
Back
Top Bottom