Mkandara,
Kwani katika kitabu cha Jumbe analilia Zanzbar kujitenga au anachohoji makubaliano sahihi ya muundo wa muungano?
Huku ukikumbuka kuwa wakati Muungano ukiasisiwa Jumbe alikuwa ndo mshauri nambari moja wa Mzee Karume, hivyo anaujuwa muungano kuliko mimi na wewe...na aliamua kuandika kitabu hicho baada ya Nyerere kumkashifu na kum paint kama msaliti wa Zanzibar...hoja ya Jumbe katika kitabu hicho,ambacho hata watoto wa shule za msingi wanakisoma(kwa tafsiri ya kiswahili na Ali Saleh "Alberto"),ni kuwa Muundo wa muungano uliokusudiwa haukuwa wa serikali mbili bali ni serikali tatu na hii si kuvunja muungano bali ni kuwa na muundo muafaka kwa pande zote. Kama ukioana wazanzibar wanalia basi hawalii kuvunja muungano, kitu ambacho ni ujinga kufikiria,bali wanalia kuwa na muundo bora wa muungano wenye manufaa kwa pande zote...na hili,kama Jumbe alivyosema, ni suala la kukaa kukubaliana lakini Mwalimu alikukuwa mbishi kwa kuwa alikuwa ana dhamira chafu ya kuimeza na kuifuta Zanzibar kama taifa huru.Pili, Jumbe ameonyesha mpaka mapungufu ya katiba ya Tanzania ambayo imeundwa ktika mfumo uleule wa katiba ya TANU,ambayo anasema wazi kuwa ndo inayochangia matatizo makubwa,yanayoitwa kero za muungano,ambazo hazitakwisha kama katiba hiyo haijaandikwa upya...na kwa kuthibitisha kuwa Jumbe hakuwa akipayukwa, hata leo utaona kilio cha vyama vya upinzani vikitaka katiba mpya...kwa kuwa hii ya sasa ipo kimfumo wa chama kimoja(Tanu sasa CCM).
N.b,
book tittled: Partner-ship