CCM ilishachokwa kitambo, Mfumo wa chama kimoja uliathiri vipawa na mawazo mbadala, Mwalimu na wenzake waliunga mkono vyama vingi miaka ya 1992 ili kuruhusu mbadala na kuifungua Tanzania. Miaka 29 baadae tunarudi tena nyuma.
Haya ndio madhara ya kukosa mwelekeo.
Kutoka vyama vingi vya kulazimisha hadi kukua kwa vyama na kuwa na nguvu. Baada ya CCM kutishwa na nguvu ya vyama imetumia Dola kuhujumu. Hatujui tunataka nini.
Kutoka mijadala ya Kitaifa ili kuamua mambo yetu kama nchi hadi amri na kuumizana, kutesana na kubezana. Kwani kama vyama havitakikani si kuwe na mjadala tu kama ulivyoitishwa wa kuanzishwa vyama vingi? Huu unyemela wa Dola kuitweza CCM na kuuwa vyama vyengine unavuruga misingi ya taifa iliyojengwa kwa hii miaka 29 ya vyama vingi.
Kutoka chaguzi za ushindani hadi kupora kwa kutumia Dola. CCM inatumia Dola kulivuruga Taifa. Chaguzi za Mitaa, 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020 imetia fora. Kama Taifa tunarudi tulikotoka.
Kutoka kujitawala kwa kukubaliana hadi kulazimishana na kuvurugana.
Kutoka kutafuta uhuru wa mkoloni Mweupe hadi kutengeneza Ukoloni wa Wenyewe kwa wenyewe. Ukoloni Mweusi.
Kutoka kustaarabika kuelekea giza la makusudi.
Kweli HATUKUI na HATUPEI? Ina maana Elimu zetu zimeshindwa kutumia njia ya kistaarabu kufanya mambo yetu na kujiamulia? Huu uwoga wa CCM wa nini? na Kwa nini vyombo vyetu vya Dola vikubali kuingizwa kwenye kadhia hii?
Hii "transformation" isio rasmi kutoka Demokrassia hadi Udikteta nani kabariki hili? Kinachoendelea Tanzania hakina mwelekeo wa kweli na kimekosa ustaarabu.
Nani wa kuibua mjadala wa Kitaifa leo? Vyama vinafungwa mikono na midomo. Wasomi wako haney moon ya Pili baada ya Uhuru wa bendera sasa wanafaidi Uhuru wa Kujitawala wa CCM.
MADHARA
Watu wanaanza kufikiria njia mbadala za kuitafuta Demokrasia na Dola inandaa njia mbadala za kukabiliana. Hapa ndipo Uafrika wetu unapojitokeza na kubezwa. Yaani Utulivu, umoja wetu, mshikamano unawekwa rehani kwa kukosa maarifa. CCM imejimilikisha kila kitu hadi maamuzi na maoni ya wananchi.
Tunataka nini kama si laana ya Uhuru wetu? Kuna haja gani ya kutumia misuli ya kidola kuwanyamazisha Watanzania baada ya kuwa tuliamua wenyewe kutumia Demokrasia kuendesha mambo yetu?
Dola haipaswi kuwa mtumwa wa CCM kwa mambo ambayo yapo kisheria na Kikatiba.
Kutoka Uhuru wa Maoni hadi Ugaidi
Kutoka Uhuru wa Mikusanyiko hadi msamiati wa Inteligensia ya Polisi
Kutoka Mshikamano wa Kitaifa hadi chuki na Uadui.
Tubadilike kwa maaslahi ya Tanzania