Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
TRA Tanzania
Matokeo ya Written Interview TRA Engineer II yanapaswa kupangwa kwa kada tano tofauti.
Mitihani ya usaili wa kuandika (Written Interview) kwa nafasi ya Engineer II ilikuwa tofauti kwa kila kada, lakini matokeo yake yamechanganywa.
Kwa mtazamo wangu, hali hii inaweza kusababisha makosa katika uchaguzi wa waliofaulu. Kutunga mitihani tofauti kwa kada tofauti halafu kuchanganya matokeo bila kuyatenganisha kwa kada, kuna uwezekano mkubwa wa kuwachagua wanafunzi wa kada moja yenye watu wengi waliofaulu ili kujaza nafasi za kada nyingine ambazo hawakuzisomea.
Mifano ifuatayo inaweza kutokea:
1. Kuna uwezekano wa kuita watu wa Mining Engineering kwenye nafasi za Textile Engineering.
2. Au kuna uwezekano wa kuita watu wa Mechanical Engineering kwenye nafasi za Mining Engineering.
3. Au kuna uwezekano wa kuita watu wa Textile Engineering kwenye nafasi za Mining Engineering.
Ni rahisi kugundua kuwa hizi ni kada tofauti kabisa, lakini hali hiyo inaweza kutokea kutokana na tofauti ya idadi ya watu waliofaulu kwenye kada fulani na alama ya mwisho (cut-off mark) iliyotumika kuchagua watu wa kwenda kwenye oral interview.
Unaweza kukuta alama ya mwisho uliyoweka kuwa kigezo cha kuwaita watu kwenye oral interview ndiyo alama ya juu kabisa kwa washiriki wa kada nyingine.
Kwa mfano, unaweza kukuta watu wa Mining Engineering wote walipata kati ya alama 95 hadi 90, kisha ukachagua 90 kama alama ya mwisho ya kwenda kwenye oral interview. Lakini kwa upande wa Textile Engineering, alama 90 inaweza kuwa ndiyo alama ya kwanza ya ufaulu (top scorer).
Hali hii inaweza kutokea kwa sababu mitihani ilikuwa kwa mfumo wa namba tu, na matokeo yaliyotangazwa yapo kwa mfumo wa namba bila kuonyesha kada.
Lakini pia si hilo pekee, hata idadi ya nafasi za kazi ilitofautiana kwa kila kada, hivyo hata selection ratio inapaswa kuwa tofauti.
Rejea Tangazo:
POSITION: ENGINEER II (12 POSTS), ambapo walitangaza nafasi kwa kada tano tofauti kama ifuatavyo:
1. Textile Engineering – 3 posts
2. Chemical and Processing Engineering – 3 posts
3. Mining Engineering – 3 posts
4. Oil and Gas Engineering – 2 posts
5. Mechanical Engineering – 1 post
Ni muhimu pia kukumbuka kwamba kila kada ilikuwa na idadi tofauti ya waliohudhuria kwenye interview. Kada kongwe zina wahitimu wengi zaidi kitaifa, hivyo zilikusanya washiriki wengi zaidi kuliko kada mpya.
Mlolongo wa kada zenye wahitimu wachache zaidi kitaifa ni kama ifuatavyo:
Oil and Gas Engineering, Textile Engineering, Chemical and Process Engineering, Mining Engineering, kisha Mechanical Engineering.
Mpangilio huu umezingatia idadi ya wahitimu waliopo katika kila kozi.
Kwa kuwa mitihani ya interview ilikuwa tofauti kwa kila kada, matokeo yalipaswa kupangwa na kutenganishwa kulingana na kada.
Hili lingewezesha uchaguzi sahihi wa waliofaulu kwenda kwenye oral interview bila kuchanganya kada.
Ikiwa matokeo yanachanganywa na watu wanachaguliwa kwa kuangalia tu waliopata alama nyingi zaidi, kuna hatari kubwa ya kuwaita kwenye oral interview watu wengi wa kada moja waliofaulu zaidi: kwa mfano Mechanical Engineering waliofaulu kuliko kada zote kwenye nafasi za kada nyingine kama Mining Engineering au Textile Engineering walio faulu zaidi kwenye nafasi za kada nyingine kama Mining Engineering.
Kwa kuwa matokeo yaliyotangazwa yapo kwa mfumo wa namba pekee (bila kuonyesha kada), kuna haja ya kuwa makini zaidi katika hatua zinazofuata ili kuepusha mkanganyiko na kuhakikisha kila nafasi inajazwa na mtaalamu sahihi wa taaluma inayotakiwa.
Huu ni ushauri wangu kulingana na jinsi nilivyoona matokeo yaliyotolewa jana.
Selection ratio (ambayo hufuata idadi ya waliohudhuria kwenye interview) na idadi ya waliofaulu (ambayo inategemea aina ya mtihani wa kada husika pamoja na idadi ya waliohudhuria kwenye interview) vinapaswa kuzingatiwa kwa umakini.
Nafasi ya kazi ya Engineer II na idadi ya nafasi kwa kila kada:
Baadhi ya matokeo ya usaili wa nafasi ya Engineer II ambayo hayajapangwa kwa kufuata kada wakati mitihani ilikua tofauti kwa kila kada: