A
Anonymous
Guest
Wakazi wa Matosa - Goba DSM, hususan eneo la Shule ya Msingi More Light, tumekumbwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji kwa takribani mwezi mmoja sasa.
Kila tunapouliza, tunaelezwa kuwa bomba linaloleta maji kutoka Uzalamoni limeharibika, hata hivyo, inashangaza kuona kuwa bomba hilohilo linaendelea kupeleka maji katika eneo la Matosa Secondary ambapo wenzetu wanapata maji kila siku.
Kwa upande wetu, maji yakitoka ni mara chache sana takribani mara mbili kwa wiki, hasa siku za Jumamosi na Jumapili. Hali hii inaleta usumbufu mkubwa kwa Wakazi wa eneo hili.
Aidha, kuna malalamiko kuwa hali hii inachangiwa na biashara ya kuuza maji inayofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wenye visima, wakishirikiana na baadhi ya wahusika wanaodhibiti ufunguaji wa maji katika eneo hili.
Tunaomba mamlaka husika zituangalie kwa haraka na kutusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili. Haki ya kupata maji safi na salama ni ya kila mwananchi.