Dah Leo tumetoka kumzika rafiki yangu kipenzi Bado mdogo tu na alikua na potential kubwa tu ya kufanya mengi maishani, nimekaa nimewaza Sana nimekumbuka baadhi ya matukio ambayo nikikumbuka nabaki kumshukuru Mungu Kwa ulinzi wake mpaka muda huu, ntaleta kisa kimoja kimoja inform of episodes mpaka viishe...
Episode 1
Hii ni kipindi Cha nyuma kidogo Bado nipo o level, form three hapo, Kuna kipindi ndo tunarudi kuanza kidato Cha tatu tukakuta Kuna shule Moja inaitwa galanos walikua wameifunga sikumbuki Kwa sababu zipi basi wanafunzi wake wakawa allocated kwenye shule mbalimbali, hivo na sisi shuleni kwetu tukakuta wanafunzi karibia 30 kwenye kidato chetu wametupiwa hapo.....
Kwenye Hawa wanafunzi wapya Kuna jamaa alikua anaitwa Tino jamaa alikua mpole kinoma haongei na mtu Wala nini, Sasa shule yetu boys tupu kuanzia kidato Cha kwanza mpaka Cha sita hakuna urembo huko, Kila madarasa Wana mabweni Yao kasoro bweni Moja lilikua linaitwa changanyikeni huko tulikua tunakaa wabishi, kama huna roho ya chuma huko huwezi kuishi, Kila siku utakutana na tranka la mtu limepigwa butterfly( kubinuliwa upande zote mbili wanaacha pale kati kwenye kufuli) mtu kashaibiwa..... Huko changanyikeni wanakaa vidato vyote vurugu tupu yani
Sasa bwenini Kuna jamaa alikua anasoma ECA form five kama sikosei alikua anaogopeka balaa maana alikua anakula Bangi vibaya Sana, alafu alikua mkorofi basi tu, huyu jamaa alikua na ubabe wa kijinga Sana, Tino tulikua tunakaa nae bweni Moja changanyikeni japo nilikua Sina mazoea nae ukizingatia ndo walikua wamekuja kutoka galanos, Sasa Tino Kila siku akipita bwenini kwenda kwenye kitanda chake Hilo jamaa la form five linampiga kwenzi kichwani Kwa nguvu maana lilikua linakaa kitanda Cha juu, watu watacheka basi tu mambo ya kishule shule mi nikawa namuonea huruma Tino sema Sasa ntafanya nini.....
Ikawa kama ratiba jamaa litampiga kwenzi tu karibia Kila siku watu washazoea watacheka tu, mpaka siku Moja yaani from nowhere Tino kaingia bwenini na kipande kikubwa Cha tofali, kamkuta jamaa yule anayempigaga makwenzi yupo u kageukia upande mwingine anaongea na washkaji, bila hata taarifa aisee kampiga tofali la kichwa jamaa akazima pale pale, aisee watu wakaanza kukimbia hapo hatuelewi Kila mtu anashangaa maana tushazoea Tino ni jamaa mpole Sana, kelele zile badae akaja mwalimu wa zamu jamaa wakambeba mpaka hospitali akaja kupewa rufaa hospital nyingine alikaa wiki 3 mpaka kupona, Tino nae akapewa suspension ya mwezi mmoja
Sasa wamekuja kurudi Kila mtu anamuonea Tino huruma wanajua jamaa atakuja kumuua, siku Tino kamfata jamaa bwenini anaongea Kwa kujiamini Sana
Tino : " bro mi najua sikuwezi hata tukipigana utanipiga tu, ila ushanipiga Sana nikavumulia, ukiamua kunipiga hakikisha kabisa unaniua, maana hata ukiniumiza vipi mimi ntakuvizia umelala safari hii lazima nikuue"
Yule bro alifyata mkia hakuwahi tena kumgusa dogo, Sasa sijui ikawaje nikaanza urafiki na Tino, jamaa alikua kabadilika kweli afu watu wanamuogopa kiaina baada ya kufanya lile tukio, badae tukaja kuwa washkaji kweli
Shuleni sasa balee imekick on, alafu hakuna wasichana, kuna shule ya pembeni tulikua tumetenganishwa na shamba tu kufika shule kwao, shule ya kata Haina mabweni, Sasa sijui nao walikua wanawaza nini, asilimia kubwa ya wanafunzi wavulana utakuta wanatokea kijijini hapo, wasichana wengi ndo wanatokea mikoa tofauti na baadhi kijijini hapo
Kwa kua walikua hawana bweni wasichana walikua wanatumia hostel za kanisa katoliki, wavulana wanasoma day, Sasa huko ndo Kila mtu alikua anaenda kuponea asilimia kubwa ya wajanja walikua Wana madem hio shule ya jirani, Tino nae alikua mtu wa madem nakumbuka nae alikua na wasichana kama wawili huko, Sasa mi hapo Sio mtu wa madem kivile, japo Kuna muda tamaa zinakuja ila Sasa sijui kwanini nilikua sihangaiki Sana na mambo hayo kipindi hiko, hostel za kanisa ikifika usiku balaa tupu, panageuka sodoma na gomora huko, wanafunzi Wana uchu walishaweka walinzi ila wapi watu hawasikii wapo radhi hata kupigana na mlinzi
Kuna muda Hali ikawa mbaya asubuhi nje ya hostel kukuta condoms ikawa kawaida alafu ni eneo la kanisa, paroko akaona isiwe tabu akanyoosha mikono juu akaifunga Ile hostel akawapa muda hao wasichana Kila mtu atafute pa kwenda, baada ya muda option pakawa hamna ikabidi tu wakapange mitaani, unakuta chumba kimoja wanajichanga hata wanne wanapanga mtaani
Huko ndo ikawa balaa Sasa, Hawa watoto wakawa wanaliwa bila huruma yaani Kuna watu wakawa kama wamehamia huko, kikaja kikao Cha Kijiji maana wanakijiji walikua wamechoshwa na hizo tabia, ikatolewa order mpaka tukaja kutangaziwa mstarini ni marufuku kuonekana kwenye mageto ya wanafunzi wa kike ukionekana kitachachokutokea utajua mwenyewe..
Sasa wanafunzi bana nao hawasikii, jioni hio hio kuna walikutwa huko aisee walichezea stiki kutoka Kwa wanakijiji mpaka wakakoma, jamaa kijijini wameunda task force inapiga doria balaa, Sasa mob physiology na ujinga wa wanafunzi, nao wakaunda kikosi wakatoka nje ya shule Kuna wanakijiji wakawapiga, ikawa bifu rasmi Sasa wanafunzi na wanakijiji.... Hapo shule Haina fence walimu wanajua wanafunzi lazima tu waende kijijini hivo wakaweka tahadhari tuwe tunatembea kundi kubwa kama tunaenda kijijini
Sasa Kuna ijumaa Moja, tunamalizia masomo saa 6 mchana, Tino kanifata kunishawishi twende kijijini Kwa demu wake, huyo msichana wake anakaa na rafiki yake kama vipi na mimi aniunganishie Kwa huyo mwenzake, hapo napiga mahesabu na hili bifu na wanakijiji naona hapana aisee, nikakataa!!! Jamaa ananishawishi tu, naona hapana, kazini Sasa wakaingia shetani na hiki kichwa kidogo wakaanza kunipa ushauri wa kijinga, kwanza hapo kulikua kumepoa kama wiki mbili hakuna ugomvi na wanakijiji, basi bana sijui nikawaza nini nikamwambia mshkaji poa twende, MAKOSA!!!!!
Tumejiandaa pale hao tumetoka nje ya shule mpaka magetoni, Tino hapo ndo sterling mi hapo Bado Domo zege, Tino yupo na msichana wake badae wakaanza kunipigia kampeni huku kwenye Jimbo lingine yule mwenzake Hana noma Wala nini, Tino akawapa Hela sijui wafate nyama maana jirani walikua wamechinja sio bucha rasmi Ili tufanye mpango wa msosi, wao wakatoka vidume huku tumejiachia tu Tino ananiambia ulikua unaogopa nini mambo si ndo haya, hapa nawaza Leo na mimi nitoe gundu aisee....
Tumekaa kama dakika 10 tunaskia kelele Kwa mbali, Kila baada ya muda inazidi kuongezeka kidogo,Tino hapo Yuko kifua wazi kajiachia kama kwake vile, Ile tunatoka kuchungulia aisee Kuna kundi kubwa la wanakijiji wanakuja upande wet wameshika mapanga, wengine mafyekeo yaani vurugu tupu, aisee hapo hakuna aliyejadiliana na mwenzake Kila mtu akashika njia Kwa speed Kali, jamaa nao wakatuungia, tumekimbia mpaka tukapotezana na Tino Kila mtu akawa kivyake jamaa nao wapo nyuma
Ilikua msimu wa kilimo Cha mahindi, mpaka Leo nikiona mahindi yamestawi hua nachukia Sana Yale majani yake, nilikua sijui kama yanakata, Kwa speed niliyokua napita nayo katikati ya shamba majani yalinikata vibaya mno, ila sikuskia maumivu Kwa muda huo.... Hapo naona Kuna mstari mwembamba Sana unatengenisha kifo na uhai, jamaa wakinishika wataniua Hawa, mbele kidogo nikakosea step nikaanguka off balance nikajibamiza upande mmoja wa shavu, nikaona hapo nisopoamka haraka wakinikuta wataniua Hawa, ila naamka nianze kukimbia aisee nilipigwa bonge Moja la fimbo mgongoni nikahisi kama mwili unakufa ganzi, Kuna jamaa nilivyokua nakimbia alikua hanipi distance kabisa alikua nyuma yangu, ile kuanguka akawa ame catch up ndo kunipiga Ile bakora, nayeye sijui wenge au kutumia nguvu nyingi akawa ameanguka ila akawa kama anapiga kelele kilugha kuwaita wenzake
Nguvu zimeisha hapo naskia maumivi balaa nikajikaza nikatoka mbio tena, hapo nakaribia shamba la shule Sasa, nimebakiza nguvu za kufika hapo tu, nikajikaza mpaka nikaingia shamba la shule, ila shule Sasa Bado mbali mpaka upafikie, Sasa wanakijiji nao sio wajinga ukishaingia shambani hawawezi kuingia huko tena, maana huko katikati ndo vijiwe vyote vya wavuta Bangi wanakaa, ikawa ndo pona yangu, tukaja kukutana na Tino badae jamaa kashika panga anataka turudi kijijini, nikawaza huyu atakua anavuta Bangi siku hizi
Naenda kuoga shavu limechubuka, mwili Sasa unawasha Yale majani ya mahindi yamenikatakata, nikawa najiskia kama mkosi yaani, sijawahi kua na tabia hizo Leo siku ya kwanza tu raia wanataka kuniua....
Sasa bana kuja kujua, kumbe Ile siku Kuna shushushu alituona tunaingia kule magetoni, akaenda kuita wenzake wajipange kwanza, Ile kurudi wanakutana na mabinti wanafata nyama, wakaanza kutembezewa kwanza stiki wao huku wanaletwa magetoni ndo zile kelele tukasikia, nikawa nawaza je wangekua kimya kimya? Leo hii mzazi wangu angeletewa maiti Kwa sababu za kijinga kama hizi?
Haikupita wiki Kuna madogo tulikua tunasoma nao wakadakwa huko magetoni, wakapelekwa' uwanja wa damu' Kuna eneo lilikuaga kubwa Sana Lina uwazi mkubwa Sana ukiwa katikati hata ukipiga kelele mtu hawezi kukusikia, wakaanza kusulubiwa Sasa, mmoja sijui ikawaje akachoropoka akafanikiwa kuwakimbia, yule mwingine walipiga mpaka wakajua kashakufa,
Wakamuacha hapo jamaa kazima asubuhi ndo Kuna wanafunzi kupita kwenda shule ndo wanamuona, wakapiga mayowe akaja pelekwa hospital, bahati nzuri hakufa, ila jamaa anasema mara ya mwisho alikua network imeshakata ila anawaskia tu wanaambiana tuondoke huyu kashakufa, haikua poa, jamaa ni kama walimuachia kilema Cha ukichaa, alikua muhuni tu, mara akawa mtu wa biblia Sana Kila saa anatembea anahubiri tu, mara akaanzisha kanisa lake hapo hapo shuleni, haikupita miezi miwili akaanza ulevi tena na Bangi Sana, jamaa mpaka Leo Sina mazoea nae Sana ila ukiangalia social media zake ni kama alikuja kua kichaa tu Toka siku Ile, very sad!!!!
Sikuwahi tena kumtamani Binti wa mtu huko kijijini mpaka nakuja kuondoka huko