UPDATES: Kwenye tukio la kuuawa watu watatu kwenye kijiji cha Kangagani, jimbo la Ole, kaskazini Pemba, mpasha habari wetu aliyeko kwenye eneo la tukio ametujulisha hivi punde taarifa za waliouawa kwamba wote walipigwa risasi wakiwa majumbani ama vibarazani:
1. Bi Asha Haji Hassan mwenye umri wa miaka 33 ameuawa wakati akitoka nyumbani kwa baba yake kwenda nyumbani kwake. Bi Asha ameacha mume na watoto sita.
2. Yussuf Shaame Muhiddin mwenye umri wa miaka 27 ameuawa wakati akiwa barazani anacheza keramu na wenzake. Hana mke wala watoto.
3. Komba Hamad Salum (maarufu Kipigi) mwenye umri wa miaka 30, naye alikuwa barazani pake wakati alipopigwa risasi na kuuawa. Ameacha mke na watoto watatu.
Kwa upande wa majeruhi, ambapo hadi sasa idadi inayofahamika ni tisa, ni hawa wafuatao:
1. Abbas Haji Nyange (miaka 27), amepigwa risasi wakati akichota maji kwenye mfereji nyumbani kwake. Utumbo umetoka nje, na kwa sasa amewahishwa Hospitali ya Vitongoji.
2. Bakari Khamis Bakari (miaka 55)
3. Mukhtar Yahya Hassan (mtoto wa miaka 16)
4. Khamis Mohammed Mmanga (miaka 40)
5. Hassan Kombo Ali (mtoto wa miaka 13)
6. Abbas Mgau Ali (miaka 22)
7. Mgau Omar Mgau (miaka 35)
8. Hamad Omar Hamad (miaka 20)
9. Ali Hamad Seif (16)
Hadi tunakwenda hewani, bado maiti zote zipo kijijini Kangagani na baadhi ya majeruhi wameshindikana kupelekwa hospitalini kwa sababu ya kutanda maaskari kwenye barabara za kuelekea Chake Chake, Vitongoji na Wete.
Weyani TV itakuwa inakuletea muhtasari wa mwenendo wa mambo kama yanavyojiri na kupokelewa na dawati letu la habari.