Zanzibar 2020 MATUKIO KATIKA PICHA NA VIDEO: Yaliyojiri visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu 2020

Zanzibar 2020 MATUKIO KATIKA PICHA NA VIDEO: Yaliyojiri visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu 2020

Safi sana, wananchi wamechoka utawala wa kiraia wanataka masultan warudi kuwatawala na kuwanyanyasa tena huku wakiwakata mapanga na kuwatoa mautumbo wazanzibari. Subirini tu, ipo siku mtakuja vuna mnachopanda.
Hivi ni nani alikwambia masultani walikuwa wanawanyanyasa, kuwakata mapanga na kuwatoa matumbo wazanzibari? Wewe ni mmoja kati ya mnaoamini kuwa Beit al ajaib (Beti la jaibu) wakati linajengwa watu walikuwa wanawekwa wazima wazima kwenye nguzo zake!

Mbona jengo liliwahi kuporomoka na hakuna hata ushahidi wa mifupa iliyopatikana kwenye hizo nguzo? Kikubwa Zanzibar inabanwa kwasababu bila ya hivyo ingekuwa mbali sana kimaendeleo pamoja na mambo mengine.
 
Hao wanajeshi wa JWTZ wanatafuta nini huko Visiwani?
Kama hao ni askari wa JWTZ basi inadhihirisha kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika kwa kuwa askari wa JWTZ hawapaswi kutumia silaha zao kwa raia na kama wanazitumia Zanzibar wakati bara hawazitumii, wanatoa ujumbe kwamba Zanzibar raia wake hawana haki sawa ya uraia sawa na Watanganyika na silaha za JWTZ zinaweza kutumika dhidi yao
 
Taarifa zilizo tufika huko Pemba, mabomu kila kona wakati huko Kangagani walio kufa ni 3 na watu kujeruhiwa vibaya.

Na Unguja baadhi ya maeneo kama daraja bovu kunarindima mabomu, huku maeneo ya Kikwajuni kuzimiwa umeme na kura zikipigwa katika kituo cha kupigia kura usiku huu.

Habari zaidi zinakuja.
 
Ni ujinga na upumbafu kuwatukana wanajeshi wanaokulinda, waliwalinda wazazi wako wakati wanakutafuta kutoka kwenye maungo yao.

Hao jeshi wanasimamia sheria tuliyojitungia(kwa kutumia vyombo vyetu kadiri ya katiba), kwa nini uwatukane sasa. Hao jeshi wanatembea na silaha za moto.

Maalim na Tundu Antisipas Lissu msiwadanganye watoto wetu, tunaumia sisi wazazi na ndugu. Lissu watoto wake amewaacha Ulaya, Maalim sijui wa kwake wako wapi.
Mkuu,

Kwahyo sheria inasema ukiwatukana wanajeshi basi upigwe????
 
Back
Top Bottom